Badili mtazamo wako kuhusu BMW

Badili mtazamo wako kuhusu BMW

Stanley Mitchell had bmw 7 series 735 ya 2011 ni bei rahisi?? unadhan unaweza ipata na bajet yako?? bmw ni kampuni jamani sio aina na gari ukiandika bmw andika ja model yake maana kwa sentensi yako hapo ni sawa na kuwa umeandika umeaandaa milion 13 lakini unasema toyota za 2011 ni bei rahisi wakati hela yako haifiki hata asilimia 10% ya kununua v8 used ya 2010....
 
Stanley Mitchell had bmw 7 series 735 ya 2011 ni bei rahisi?? unadhan unaweza ipata na bajet yako?? bmw ni kampuni jamani sio aina na gari ukiandika bmw andika ja model yake maana kwa sentensi yako hapo ni sawa na kuwa umeandika umeaandaa milion 13 lakini unasema toyota za 2011 ni bei rahisi wakati hela yako haifiki hata asilimia 10% ya kununua v8 used ya 2010....
Mkuu ungekua unafatilia huu uzi kwa makini toka mwanzoni hapa tukiongelea "BMW" tunamaanisha "bmw 3 series e90" ndo mana nikasema just "bmw ya 2011" nikimaanisha 3er ya 2011...

Pia hakuna mahali nimesema toyota ni bei rahisi huezi kuamini sijui bei ya gari yoyote ya toyota labda ist kwasababu sijawai kua interested na toyota yoyote hata iwe prado au v8 uliyoitaja...nafata moyo wangu mm hata uweke iyo V8 kwa bei chee siwezi kuacha German hata iwe kwa bei ghali.... inshort huezi kunikuta naongelea toyota mimi ndo mana nashangaa umesema nimesema mambo toyota wakati ilo neno nina miezi sijawai kulitamka....

Pia iyo milioni 13 sio bajeti yangu ya kununua gari iyo A4...
nimesema hivii iyo 13m ni kodi ya A4 ya 2008, ya 2007 ndo 10m na 2009 kodi yake ni 15.9m, 2010 ni 17m na 2011 kodi ni 13.4m
kwaiyo ujue kua bajeti ni Kodi plus CIF.....

Halafu nilivosema naona ni "bei ndogo" nilimaanisha kwa bajeti yangu na ukilinganisha na mwaka wa gari naona bei ni ndogo
mfano hapo huezi kukuta audi a4 ya 2010 au 2011 ukaipata kwa dola 4,000 ila 3 series ya miaka iyo unaipata kwa dola 4,000 or less
Screenshot_20180131-155414.png
 
Mafundi wengi Tanzania ni magumashi!njaa tu .Fundi wa kweli awezi tumia lisaa limoja kama ana computer kujua tatizo.gari lina Computer system inaitwa Electronic Control Unity amabyo nayo ina software kama vile computer.Tatizo unaweza kuta hao mafundi wana diagnostic kit yenye let say bmw za mwaka 2002 mpaka na 2005 wakati BMW wanayotakiwa waicheck tatizo ni ya 2006! Hapa hizo computer zao azitoona tatizo.pia mafundi wengi hapa Tanzania awataki kujisomea wao ni try and erro.
Kwa sasa unaingi E bay unaweka part no.unalipia kwa Pay pal baada ya siku tatu DHL wanakugongea mlango spea zimeshafika.Mimi na X3 na wala sikosi usingizi wa kuwaza spea sijui nini.Watanzania walio wengi ni maji kufanta mkondo awajiongezi! Wananunua magari kufuata maongezi ya vijiweni,matokeo yake wanakuwa waoga ktk kubadilika
Hata kama una OBD scanner kama mtu hajui jinsi ya kutatua tatizo haita saidia.

Kwa mfano ECM (computer ya gari) itasema tuu kunatatizo kwenye MAF circuit (mass air flow sensor) na kuonesha error code P0101 na kuwasha taa ya check engine light wakati tatizo linaweza kuwa ni vumbi linalofanya sensor isisome vizuri.

Ukisafisha hiyo sensor na alcohol na ku-clear code utakuwa umeondoa tatizo. Sasa utaona limitations za hizo scanner...zenyewe zinakupa tuu eneo ambalo tatizo linaweza kuwa.
 
Kulinunua sio tatizo,tatizo ni kulifanya liendelee kukaa barabarani, upatikanaji wa spea ni mgumu kwa bongo pia ni ghali,unaweza kuwa na pesa lakini ukakosa spea bongo mpaka uagize toka nje!!
Hivi ni kitu gan kinamfanya mtu anunue gari?
1. Upatikanaji wa spea?
2. Uhitaji wa gari?

Maana sielewi, kila gari ikitajwa watu mbioo uoga wa upatikanaji na ughali wa spea. Mara ulaji wamafuta.

We need to change our mindsets atheeee
 
All over the internet watu watakuambia bila kupepesa kwamba Toyota ndio kampuni (na Japan ndiyo nchi) inayoongoza kwa kutengeneza magari reliable yanayodumu.

Wajapan wana highly evolved manufacturing na quality testing process. Wakitoa chuma ni chuma kweli hakikusumbui hovyo.

Pia ni minimalists na hivyo cost za gari zinakuwa chini kwasababu hawana unnecessary complications.

Inexpensive + Reliable - Perfect for the masses hasa waafrika.
True fact mkuu, na ndio maana gari zao zipo allover the world. Pia adaptation imekuwa rahisi kwa gari zao maana gharama za uendeshaji zipo reasonable kwa raia wengi.

European brands zipo na superficial technology pamoja na performance ila zinasumbuaga sana na mazingira ya kwetu huku na usiombe likianza kukusumbua utatoa hela mpaka useme nini hiki?!
Gari ina umeme tu kila mahali yani, kakitu kadogo kanaweza kakakufanya ulipark gari kwa miezi na mara zote inataka uwe na mfuko wa uhakika ili kuweza ku maintain.

Taa za check engine hazitakuacha salama ndio maana waliyoyatumia wanaona heri toyota tu service ya gharama kubwa haizidi laki 6 kwa toyota ila kwa hao jamaa ni si chini ya 2.5 million *****.
 
Mkuu mshana asante kwa kututoa hofu...vipi unazungumziaje hii X3 na X5 as nataka kujilipua na mojawapo...interms of maintanance na fuel consumption.

Please [HASHTAG]#mshana[/HASHTAG] wengine ambao mnayajua..mi niko na nissan kwa miaka kadhaa....ila nataka nihamie humo.
Kama nissan umeimudu sina shaka Beamer utaiweza vyema.
 
kwa Tanzania yetu hii magari yanayoongoza kupendwa,kukubalika na ya gharama ya kati ni
gari za matumizi binafsi
1.Toyota
2.Suzuki
3.Nissan

gari za mizigo mikubwa
1.Scania
2.Mercedes Benz
3.Faw,Howo

gari za mizigo ya kati
1.Mitsubishi
2.Toyota
3.Isuzu

gari ndogo za mizigo
1.Toyota
2.Nissan
3.Suzuki

Gari kubwa za abiria
1.Scania
2.Yu Tong
3.Zongtong, higer etc

gari za kati za abiria
1.Toyota
2.Tata
3.Isuzu and Nissan

gari ndogo za abiria
1.Toyota
2.Toyota
3.Nissan

ukinunua nje ya brand hizi jiandae kisaikolojia kama mkono wako mfupi kama Mimi. kumbuka nunua gari ambayo utaweza kuimudu kuanzia service mpaka vipuri la sivyo gari itakushinda. pia nunua gari ambayo ni rahisi kupata Spear parts zake na bei iwe nafuu kwako. usinunue gari kwa sifa bila kufanya utafiti.
Wengi wanatafta sifa tu, mwisho wa siku wanalialia na magu alivyobana *****.
 
Hizi gari za kijerumani nikizungumzia Audis, BMWs na Mercedes zina sifa kubwa mbili kuu. Ya kwanza ni safety (usalama) na ya pili ni comfort (raha au starehe). Kwa sifa hizi zimekua chagua la watu wengi hasa wenye vipato vya kati (middle class) na watu maarufu (VIPs) kote ulimwenguni. Magari haya yanatengenezwa kwa matoleo (series) mbalimbali. Mfano kwenye Mercedes kuna yale madogo kabisa wenyewe wameyaita (A class), kuna C class (vijana wengi huendesha haya), kuna E class (vijana wenye kipato na watendaji wa makampuni, wafanyabiashara wenye umri wa makamo n.k), kuna S class (haya ni kwa matajiri, mabalozi, waheshimiwa n.k.). Mara nyingi S class huendeshwa na madereva na boss huketi kiti cha nyuma. Hii ni mifano michache kwa upande wa Mercedes.
Madaraja haya pia yako kwa magari ya BMW. Kiujumla teknoknolojia ya magari haya ya kijerumani haitofautiani sana na ni kweli magari haya yanatumia mifumo ya umeme zaidi na hivyo yanahitaji matunzo na ufuatiliaji wa ratiba zake za matunzo (maintanance) kwa umakini. Mfumo wa mafuta uko vizuri sana kuliko wengi wanavyohisi. Kwa sasa hata vipuri vinavyohitaji kubadilishwa mara kwa mara (consumables) pia vinapatikana kirahisi hapa kwetu na ukikwama sana unaweza kuagiza kutoka Nairobi ama Afrika ya kusini ndani ya siku chache ukavipata. Wafanyabiashara wetu wa spare parts pia huangalia ukubwa qa soko kabla ya kuanza kuagiza spare hizo kwa wingi. Nakumbuka hata Vitz zilipoanza kuletwa nchini miaka hiyo, spare zake zilisumbua kwani gari hizo zilikuwa chache mno ukilinganisha na gari kama Toyota Corolla ambazo nyingi ndio zilitumika kama Taxi.
Changamoto nyingini kwa gari za kijerumani hapa kwetu ni soko la kuuzia pindi utakapotaka kuliuza baada ya kulitumia (resaling). Kwanza hutapata mteja kirahisi kwa sababu naweza kusema kwa zaidi ya asilimia 80 Tanzania ni soko la Toyota na hiyo 20% iliyobaki ndio inayogombaniwa na aina zingine kama Mercedes, Audi, BMW, Nissan, Hyundai, VW, Renault n.k.
Kwa hiyo hapa ndio utaona kwa kifupi kwa nini Toyota bado ni aina pendwa hapa kwetu. Si kwa sababu ya bei la hasha ila kwa sababu nyingi ingawa za msingi nizionazo mimi ni urahisi wa kupata spare za aina nyingi na pia urahisi wa kuuzika baada ya kulitumia.
Sio Tanzania tu hata huko yanapotoka hayo magari resale value yake ipo chini sana tofauti na Toyota. Wazungu wenyewe wanakiri yani sio utani. Utanunua gari mpya dola laki moja na hamsini ($150,000) baada ya mwaka mmoja mpaka miwili ya matumizi tu hamna mtu atalinunua hilo gari zaidi ya dolla elfu hamsini ($50,000) na wateja wenyewe wa kutafta na tochi.

Ila njoo kwa Toyota sasa, gari ilionunuliwa dola elfu arobaini ($40,000) ndani ya miaka miwili huwezi kukuta inauzwa chini ya dola elfu ($30,000) na wateja wapo kibao.
 
True fact mkuu, na ndio maana gari zao zipo allover the world. Pia adaptation imekuwa rahisi kwa gari zao maana gharama za uendeshaji zipo reasonable kwa raia wengi.

European brands zipo na superficial technology pamoja na performance ila zinasumbuaga sana na mazingira ya kwetu huku na usiombe likianza kukusumbua utatoa hela mpaka useme nini hiki?!
Gari ina umeme tu kila mahali yani, kakitu kadogo kanaweza kakakufanya ulipark gari kwa miezi na mara zote inataka uwe na mfuko wa uhakika ili kuweza ku maintain.

Taa za check engine hazitakuacha salama ndio maana waliyoyatumia wanaona heri toyota tu service ya gharama kubwa haizidi laki 6 kwa toyota ila kwa hao jamaa ni si chini ya 2.5 million *****.
Umemaliza mkuu.
 
Tatizo ni TRA kwenye ushuru wa magari ya ulaya bei zake zipo juu hatari 2009 VW Jetta $3500 CIF ushuru 18.5milion mpaka unashangaa hawajaa vipi
 
Aaaaah wajerumani wazee wa kufanya complications. Wajanja hawa jamaa.... mi nawakubali kwenye luxury features zao tu. Lakini Engine tumuachie Mjapan.
 
Ila BMW sizipendi coz kuna cku nilipanda ya mdada mmoja akawa ananiringishia[emoji23][emoji23]kuanzia hapo nikaichukia..saivi ipo juu ya mawe kaipaki[emoji16][emoji16]
 
Back
Top Bottom