Hizi gari za kijerumani nikizungumzia Audis, BMWs na Mercedes zina sifa kubwa mbili kuu. Ya kwanza ni safety (usalama) na ya pili ni comfort (raha au starehe). Kwa sifa hizi zimekua chagua la watu wengi hasa wenye vipato vya kati (middle class) na watu maarufu (VIPs) kote ulimwenguni. Magari haya yanatengenezwa kwa matoleo (series) mbalimbali. Mfano kwenye Mercedes kuna yale madogo kabisa wenyewe wameyaita (A class), kuna C class (vijana wengi huendesha haya), kuna E class (vijana wenye kipato na watendaji wa makampuni, wafanyabiashara wenye umri wa makamo n.k), kuna S class (haya ni kwa matajiri, mabalozi, waheshimiwa n.k.). Mara nyingi S class huendeshwa na madereva na boss huketi kiti cha nyuma. Hii ni mifano michache kwa upande wa Mercedes.
Madaraja haya pia yako kwa magari ya BMW. Kiujumla teknoknolojia ya magari haya ya kijerumani haitofautiani sana na ni kweli magari haya yanatumia mifumo ya umeme zaidi na hivyo yanahitaji matunzo na ufuatiliaji wa ratiba zake za matunzo (maintanance) kwa umakini. Mfumo wa mafuta uko vizuri sana kuliko wengi wanavyohisi. Kwa sasa hata vipuri vinavyohitaji kubadilishwa mara kwa mara (consumables) pia vinapatikana kirahisi hapa kwetu na ukikwama sana unaweza kuagiza kutoka Nairobi ama Afrika ya kusini ndani ya siku chache ukavipata. Wafanyabiashara wetu wa spare parts pia huangalia ukubwa qa soko kabla ya kuanza kuagiza spare hizo kwa wingi. Nakumbuka hata Vitz zilipoanza kuletwa nchini miaka hiyo, spare zake zilisumbua kwani gari hizo zilikuwa chache mno ukilinganisha na gari kama Toyota Corolla ambazo nyingi ndio zilitumika kama Taxi.
Changamoto nyingini kwa gari za kijerumani hapa kwetu ni soko la kuuzia pindi utakapotaka kuliuza baada ya kulitumia (resaling). Kwanza hutapata mteja kirahisi kwa sababu naweza kusema kwa zaidi ya asilimia 80 Tanzania ni soko la Toyota na hiyo 20% iliyobaki ndio inayogombaniwa na aina zingine kama Mercedes, Audi, BMW, Nissan, Hyundai, VW, Renault n.k.
Kwa hiyo hapa ndio utaona kwa kifupi kwa nini Toyota bado ni aina pendwa hapa kwetu. Si kwa sababu ya bei la hasha ila kwa sababu nyingi ingawa za msingi nizionazo mimi ni urahisi wa kupata spare za aina nyingi na pia urahisi wa kuuzika baada ya kulitumia.