Badili mtazamo wako kuhusu BMW

Badili mtazamo wako kuhusu BMW

Tatizo mpaka leo VETA awafundishi Automotive Electronics ,mpaka leo sylubus yao ni Ya 1947 pijot na Landlover yenye only 5 wires (wirring nzima ya gari).Ata ukiend KJ Motors ambao ni dealer wa Toyota zipo Toyota mafundi wamechemka ishu za umeme! Tanzania bado tuna safari ndefu kwenye kuzalisha mafundi wa uhakika wa magari ya kisasa,LED TVs,Simu na Vifaa vypte vya kisasa vya Kielectronics mpaka vile vya mahospital....Natamani ningeanzisha darasa juu ya hivi vitu kama ningepata patners so sad pale unaponunua kifaa cha electronic alafu kikifa ujui fundi umpelekee nani
Mkuu, KJ Motors ni dealer wa Toyota?
 
Sawa Mkuu hata simu kuna za Dubai pia kwaiyo nikskia neno Dubai tu najua ni type ya wale wa kuweka kokoto kwenye korosho Mkuu....
sema kwani za Dubai zinauzwa website gani mkuu? Na utajuaje kua hii ni ya Falme za Kiarabu??
Maranyingi showroom za vichochoronj ndio zinauza
 
View attachment 686106ni aina ya gari inayoaangaliwa kwa jicho la tofauti sana... Likionekana ni gari ghali na la kifahari huku watu wakitishana sana kuhusu ughali wa vipuri na upatikanaji wake wa shida
Lakini nikwambie tu kitu kimoja hakuna gari imara kama BMW na ukiweza kufuata masharti ya kumiliki gari hutakaa ujutie pesa yako
Kama una uwezo wa kununua Brevis, Nissan Fuga au Klugger... Magari ya kijapan yenye engine kubwa na matumizi makubwa ya mafuta... Hakika HUWEZI kushindwa kununua BMW ya kawaida lakini yenye viwango sawa na hizo gari hapo juu.. Huku ukifurahia ulaji mdogo wa mafuta... Mfumo wa BMW uko tofauti sana... Umejengwa kwenye mfumo wa kuokoa ulaji wa mafuta huku nguvu ya mashine ikiwa ni ileile

Gari nyingi za kijapan hazina body ngumu tofauti kabisa na huyu mnyama BMW... Yani hata unapokaa kwenye seat unahisi kabisa umekaa kwenye mashine ya ukweli... Na ni aghalabu kukuta BMW imepinduka kichwa chini mijuu guu

Hizo magari hapo juu nazo spare zake ni ngumu na ghali kupatikana kama BMW tuu... Tena sometimes unaweza kuipata ya mnyama kirahisi zaidi kuliko hizo nyingine
Kingine ni kwamba BMW wana variety of different styles na kila style ni bakora tofauti na hizi nyingine.... Ukikuta mabrevis yote yanafanana

Badili mtazamo wako BMW ni gari ngumu nzuri na sio ghali kama unavyodhani.. Kuwa tofauti... Miliki mnyama... Pichani hapo juu ni 320td fuel consumption ni km 15 kwa Lita sawasawa na duet tuu... Lakini mkiwa rodini mnyama atatamba
Hizi gari za kijerumani nikizungumzia Audis, BMWs na Mercedes zina sifa kubwa mbili kuu. Ya kwanza ni safety (usalama) na ya pili ni comfort (raha au starehe). Kwa sifa hizi zimekua chagua la watu wengi hasa wenye vipato vya kati (middle class) na watu maarufu (VIPs) kote ulimwenguni. Magari haya yanatengenezwa kwa matoleo (series) mbalimbali. Mfano kwenye Mercedes kuna yale madogo kabisa wenyewe wameyaita (A class), kuna C class (vijana wengi huendesha haya), kuna E class (vijana wenye kipato na watendaji wa makampuni, wafanyabiashara wenye umri wa makamo n.k), kuna S class (haya ni kwa matajiri, mabalozi, waheshimiwa n.k.). Mara nyingi S class huendeshwa na madereva na boss huketi kiti cha nyuma. Hii ni mifano michache kwa upande wa Mercedes.
Madaraja haya pia yako kwa magari ya BMW. Kiujumla teknoknolojia ya magari haya ya kijerumani haitofautiani sana na ni kweli magari haya yanatumia mifumo ya umeme zaidi na hivyo yanahitaji matunzo na ufuatiliaji wa ratiba zake za matunzo (maintanance) kwa umakini. Mfumo wa mafuta uko vizuri sana kuliko wengi wanavyohisi. Kwa sasa hata vipuri vinavyohitaji kubadilishwa mara kwa mara (consumables) pia vinapatikana kirahisi hapa kwetu na ukikwama sana unaweza kuagiza kutoka Nairobi ama Afrika ya kusini ndani ya siku chache ukavipata. Wafanyabiashara wetu wa spare parts pia huangalia ukubwa qa soko kabla ya kuanza kuagiza spare hizo kwa wingi. Nakumbuka hata Vitz zilipoanza kuletwa nchini miaka hiyo, spare zake zilisumbua kwani gari hizo zilikuwa chache mno ukilinganisha na gari kama Toyota Corolla ambazo nyingi ndio zilitumika kama Taxi.
Changamoto nyingini kwa gari za kijerumani hapa kwetu ni soko la kuuzia pindi utakapotaka kuliuza baada ya kulitumia (resaling). Kwanza hutapata mteja kirahisi kwa sababu naweza kusema kwa zaidi ya asilimia 80 Tanzania ni soko la Toyota na hiyo 20% iliyobaki ndio inayogombaniwa na aina zingine kama Mercedes, Audi, BMW, Nissan, Hyundai, VW, Renault n.k.
Kwa hiyo hapa ndio utaona kwa kifupi kwa nini Toyota bado ni aina pendwa hapa kwetu. Si kwa sababu ya bei la hasha ila kwa sababu nyingi ingawa za msingi nizionazo mimi ni urahisi wa kupata spare za aina nyingi na pia urahisi wa kuuzika baada ya kulitumia.
 
nimekuelewa sana hapo kwenye "reselling" ya hayo magari
 
Wakuu Nje ya Mada kidogo...
Hivi gari za Singapore mnazionaje ukicompare na Japan??
Mi binafsi naona kama zina quality nzuri kwa muonekano wa pichani.ila nyie wajuzi sijui mna overall comments gani
Daah mwanangu mwaka wa ngapi sijui sa hivi naonaga kila siku unawauliza washkaji hizo bmw,audi,vw hujanunua tu aisee?

Jilipue ununue maana kama ni details Yule mshkaji anaitwa PRONDO anakupaga kila siku humu jf aisee.
 
Mfumo wa BMW
uko tofauti sana...
Umejengwa kwenye mfumo
wa kuokoa ulaji wa mafuta
huku nguvu ya mashine ikiwa
ni ileile

hata toyota kuna mfumo wa D4 nguvu nyingi mafuta kidogo hivo usituaminishe bmw ndo most fuel efficiency okay?? au ww ni wakala
 
Sikuandika KUBISHANA na yeyote.. Nimeandika uhalisia wa ninachokijua kwa vitendo.. Mimi sio wakala lakini nimemiliki magari ya pande zote mbili... Na nimekuwa kwenye field ya magari kwa miaka mingi hebu kapitie mada maalum ya magari "]mada maalum ya magari utaelimika zaidi
Hizo D-4 ni mfumo wa karibuni heri hata ungezungumzia VVT na VVT-i
 
we nae hujui kitu d4 au d4d kwa diesel ndo latest mfumo wa uingizaji mafuta na uchomaji kwa toyota sasa ww unataka ulete tena vvti hujui vvti ni zaman thou bado hawajaicha stil wanatengeneza zote zote ....na kusema bmw ngumu kukuta zimepinduka nadhan hiyo ni sifa ya benzi angalia youtube kule nurburgring zinavyolala chali!!
 
afu soma uelewe ....nimeandika toyota kuna d4 nguvu nyingi mafuta kidogo afu ww unasema d4 ni mfumo wa karibuni haha unadhan kuandika d4 ni kwamba sijui ???
 
Daah mwanangu mwaka wa ngapi sijui sa hivi naonaga kila siku unawauliza washkaji hizo bmw,audi,vw hujanunua tu aisee?

Jilipue ununue maana kama ni details Yule mshkaji anaitwa PRONDO anakupaga kila siku humu jf aisee.
Haha mkuu nilitaka nichukue december TRA wameongeza kodi mkuu kwaiyo huu muda ninaojazia ilo ongezeko naendelea kufanya risechi mkuu...

Kuuliza si ujinga! Na asiyeuliza hana ajifunzalo!
Btw nilikua na mpango wa kuagiza A4 ya 2007 sasa TRA wakaongeza kutoka 7m hadi 10m na points kadhaa....sasa ndo nikaona kuliko nitoe 10m kwa B7 ya 2007 bora niongezee 13m nichukue B8 ya 2008...ingawa nikipata ya 2011 itakua ahueni mana kuna uwezekano nikalipa kodi ya 7.9m sema sasa be forward sioni ya 2011 tena...

so umeona sasa point yangu so Mkuu usinilaumu mm TRA wanahusika pia na ucheleweshwaji huu.

Ingawa pia nazitamani bmw za 2011 lakini napata doubt mana zina bei ndogo kishenzi!
 
Aisee nimekuelewa sana mkuu na samahani sana kama ntakua nilikuzingua kwa comment yangu.

All the best chief.
 
Mimi nilidhan Nissan iko cheap kuliko Suzuki..

nissan kama huna hela ya spare OG siyo gari ya kununua itakufia ndan ya mda mfupi sana ... tofauti na toyota na suzuka unachagua ufunge spare ipi kutokana na mfuko wako na bado mashine itadunda fresh barabaran
 
Back
Top Bottom