Badili mtazamo wako kuhusu BMW

Badili mtazamo wako kuhusu BMW

Inspection ya gari inakuja kufanyikia Tanzania na gari kama litakutwa na ubovu utalazimika kulitengeneza kwa gharama zako mwenyewe.

Pia BMW zinazotumika Japan zinatofautiana kidogo na zinazotumika Singapore.
Vp naonaga Be Forward wanauzaga pia na magari ya Singapore...hiyo imekaaje kitaalam kua BF kuuza gari za Singapore hapo BF wanafanya inspenction au ndo ile ile sawa kununua kwenye sites nyingine za Singapore kua hakuna Inspection?

Tofauti ya BMW za Japan na Sinagpore nini? Maana naona kama za Singapore ndo zipo kwenye good condition kushinda Japan japo bei ya Singapore imesimama.

Pia Menu Ya kiJapan kwa BMW inaweza kuifix vp hapo au unabadilisha kabisa ? Maana haina English language
 
Hio kitu hata TRADECARVIEW wanayo sana,kuna gari niliichek be forward CIF yake ni $3700 kule nimeenda gari ile ile nimeikuta ni $ 5300,upuuzi sana.
Hata mimi shuhuda wa hii ishu, gari beforward ni cheap kuliko hio mitandao mengine. Na baadhi ya magari ndio hayo hayo na picha ndio hizo hizo zilizotumika huku na kule zipo. Tradecarview wao ndio kiboko kwa bei za ajabu naona..... nihsakuta BMW 7 series beforward inauzwa $1500 FOB ya 2003 nyeupe, mnyama anaita kabisa ila ingia tradecarview uone bei zao.....
 
Naangaika kupata BMW, 5 Series, AT, RHD, Sedan, Petrol, 2,500CC, Push to start, mileage hisizidi 80,000km, ya mwaka 2008 ama ya 2007 ambayo inakaribia kufanana na ya mwaka 2008 na iwe inatoka Japan na sio Singapole.

Nafuatilia sana Befoward sababu bei zao ni za kawaida tofauti na kwingine lakini bado sijapata yenye kuniridhisha.

je, kuna kampuni zingine naweza kuangalia tofauti na Tradecarview na SBT?
 
GuDume ngoja nisizungumzie wengine.. Nijizungumzie binafsi
Mimi kwanza ni MGONJWA wa magari na gari ya kwanza kununua ilikuwa ni Mitsubishi Gallant mwaka 2001,kisha nikanunua Nissan bluebird... Baada ya hapo nikaingia kwenye TOYOTA chaser, Avante lordly... Niliipenda sana hii mashine TZS 2164, Nikaendelea na TOYOTA nikanunua Balloon GX90 CRESTA T800ABJ... hii mpaka leo ipo... Sifa ya balloon itakumbukwa vizazi vingi... Nikaingia kwenye Ford Explorer V8, nikaingia kwenye Benz V boot, nikarudi kwenye Nissan English Version kisha nikaingia kwenye BMW halafu nikarudi kwenye Nissan kisha BMW
Naomba nikiri wazi bila kificho bila hiyana na bila sifa BMW ni gari bora hasa linapokuja suala la ubora uimara na usalama
 
ipo ndugu... miaka kadhaa nyuma nilikuwa napush hyo 320 turbo diesel ila nikaisukuma baada ya vyuma kukaza since ilikuwa inaumiza kwenye spare parts nimerudi kwenye ulimwengu wa toyota... maana car enthusiast's wa bongo wanakwambia TOYOTA is our god SUZUKI is our jesus sasa jiroge utoke nje ya hizo brand na mfuko umetoboka
Noma sana!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
BIGURUBE acha ulimbukeni bwana. Toyota is one of the most competitive car making company in the world( na kwa sasa inaongoza katika makampuni 10 mkubwa duniani ya kutengeneza magari)
  • 8th place: Honda Motor.
  • 7th place: Fiat-Chrysler.
  • 6th place: Ford Motor.
  • 5th place: Hyundai-Kia.
  • 4th place: Nissan-Renault Group.
  • 3rd place: Volkswagen Group.
  • 2nd place: General Motors.
  • 1st place: Toyota Motor.
wanazalisha gari zenye sifa tofaut kwa sababu tofauti. ulaya na marekani wanatumia Toyota itakuwa wewe tu mswahili wa hapa unajidai eti si magari.... huo ni ulimbukeni tu. labda uwe huzifahamu gari za Toyota.

katika gari imara duniani
20. Toyota FJ Cruiser
19.Lexus LX 570
11.Toyota 4Runner
6.Toyota Land Cruiser FJ 40
5.Toyota Land Cruiser Mkonga

number 1 is Jeep Wrangler,
Mercedes Benz G Class ikiw anamba 7

kama vile haitoshi kuna Toyota Crown Majesta ni moja ya magari ambayo ni ya kifahari

View attachment 686817
View attachment 686819
View attachment 686820
View attachment 686821
View attachment 686822 View attachment 686823

Hi ni Toyota Crown ya mwaka 2013
price
to-2.png
150 000 $

Top speed 250 kph / 155 mph

Speed from 0-100 kph 5.7 seconds

Power 343 bhp / 252 kW

bhp / weight
185 bhp per tonne

Displacement
3.5 litre / 3456 cc

Weight
1850 kg / 4079 lbs

halafu wewe mlalahoi tu huna mbele wala nyuma unakuja kusimama mbele ya wanaume unaponda magari ya toyota? we utawafanya watu wagundue kuwa hufahamu magari na una ulimbukeni. magari yanazidiana uzuri na thamani lakini kwa mtu mwenye akili timamu hawezi ponda magari ya Mjapani hata siku moja. Japan wanauza magari all over the world. wanatengeneza magari kulingana na mahitaji ya watu husika. watu wa aina yako wakue sasa.
GuDume,nimekuvulia kofia mwanaume...hayo maelezo na hizo ndinga kwa picha ni shida tupu
Binafsi huwa naipenda sana Land Cruiser mkonge nje (kama zile za police) tatzo uwezo sina
Pia,gari nyingine ninazozipenda ni pamoja na volts,Brevis,na Athlete Crown...Mungu akipenda na akiniongezea uhai ipo siku nitamiliki gari moja kati ya hayo niliyoyataja!

Amen.....na Mungu akikuongezea umri mpaka ifike miaka hiyo hizo gari ulizozitaja hapo zitakuwa zinaonekana kama vile leo hii tunavyoiona carina....au yale ma..Mark ii na machaser baloon..

I mean wakati huo technology itakuwa imeshakuwa.....pengine ikawa gari likihisi tu makalio ya mmiliki linawaka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
View attachment 686106ni aina ya gari inayoaangaliwa kwa jicho la tofauti sana... Likionekana ni gari ghali na la kifahari huku watu wakitishana sana kuhusu ughali wa vipuri na upatikanaji wake wa shida
Lakini nikwambie tu kitu kimoja hakuna gari imara kama BMW na ukiweza kufuata masharti ya kumiliki gari hutakaa ujutie pesa yako
Kama una uwezo wa kununua Brevis, Nissan Fuga au Klugger... Magari ya kijapan yenye engine kubwa na matumizi makubwa ya mafuta... Hakika HUWEZI kushindwa kununua BMW ya kawaida lakini yenye viwango sawa na hizo gari hapo juu.. Huku ukifurahia ulaji mdogo wa mafuta... Mfumo wa BMW uko tofauti sana... Umejengwa kwenye mfumo wa kuokoa ulaji wa mafuta huku nguvu ya mashine ikiwa ni ileile

Gari nyingi za kijapan hazina body ngumu tofauti kabisa na huyu mnyama BMW... Yani hata unapokaa kwenye seat unahisi kabisa umekaa kwenye mashine ya ukweli... Na ni aghalabu kukuta BMW imepinduka kichwa chini mijuu guu

Hizo magari hapo juu nazo spare zake ni ngumu na ghali kupatikana kama BMW tuu... Tena sometimes unaweza kuipata ya mnyama kirahisi zaidi kuliko hizo nyingine
Kingine ni kwamba BMW wana variety of different styles na kila style ni bakora tofauti na hizi nyingine.... Ukikuta mabrevis yote yanafanana

Badili mtazamo wako BMW ni gari ngumu nzuri na sio ghali kama unavyodhani.. Kuwa tofauti... Miliki mnyama... Pichani hapo juu ni 320td fuel consumption ni km 15 kwa Lita sawasawa na duet tuu... Lakini mkiwa rodini mnyama atatamba
Hapo kwenye red, mkuu ina CC ngapi? Nataka kuagiza mwezi ujao maana sipendi magari ya toyota, nilihitaj gari toka BMW, BENZI au AUDI ila BMW ni 1st choice tangu miez 3 iliyopita nazungukia humu kupata maoni ya watu 80% ni maoni hasi nikataka nipate maoni toka kwa aliyewahi kumiliki, nataka unihakikishie hapo kwenye fuel consumption ni kweli au ni typing error maana kwa kuiangalia ni kama ina 1990CC
 
1800 chukua mnyama huyo yuko makini
 
1800 chukua mnyama huyo yuko makini
Diesel sio? za petrol CC 1900 inaweza kwenda KM ngapi? mimi suala la spare siogopi hata kama taa ni milioni 1 maana silinunui kwaajili ya kuligongagonga hovyo hivyo najua hata nikilipa service ya laki 5 kila baada ya miez 3 sio mbaya pia utanipa namba ya fundi unayemwamini wa haya madubwasha
 
Zote poa lakini diesel the best... Hiyo ya petrol haipungui km 10 kwa liter... Kumbe wewe ni kama mimi tu
 
Zote poa lakini diesel the best... Hiyo ya petrol haipungui km 10 kwa liter... Kumbe wewe ni kama mimi tu
Yes mkuu, BMW inaishi moyoni, hata mimi naona TOYOTA ni usafiri tu sio gari, huo ni mtazamo wangu na hayupo wa kunibadilisha. Naweza kuagiza kupitia site gani? Nimeangalia beforward naona zipo za petrol tu mkuu. Nikiwa na 25 M si inatosha kuliingiza nchini.
 
Inatosha kabisa tena na change inabaki... Check na SBT Japan wanazo za diesel pia check na Gumtreee
 
Inatosha kabisa tena na change inabaki... Check na SBT Japan wanazo za diesel pia check na Gumtreee
Poa mkuu ngoja nianze kupitisha macho huko, hao waoga waache waendelee na toyota (baby walkers), pia wajitahid kuwazuia wapenzi wao kutukodolea macho tukiwa kwenye foleni na kuwaambia baby nataka kama ile.
 
[emoji108][emoji108][emoji23][emoji23][emoji123][emoji123][emoji123]
 
Back
Top Bottom