Badili mtazamo wako kuhusu BMW

Badili mtazamo wako kuhusu BMW

Hao matapeli wa mtandao je? Umewasahau ee?
Ok mkuu wewe unatumia ipi?
Umetumia kwa muda gani sasa?
Siku hizi kuibiwa kwenye malipo ya kimtandao ni suala la bidii yako binafs kuhakikisha unaibiwa. Jaribu kufanya malipo hata ya kalam kwa paypal au namna ya hivyo km trustee wa pesa yako. La kuibiwa ni hiari yako km inakupendeza
 
Sasa Mshana Jr naomba ushauri wako kuhusu service ya BMW

1. Je service nangoja notification from car computer au nazingatia tu km?
2. Kuna haja ya kutafuta fundi specific wa BMW au hata mafundi wa kawaida?
3. Ni vitu gani hasa vya kubadilisha wakati wa service tofauti na oil? Hata huku Kuna kubadilisha filters?

Ni hayo tu ndugu mbadilisha mawazo, waweza ukawa sio fundi ila kutokana na uzoefu wa kuyatumia haya ukawa na majibu

NB: nafikiria ku enhance music system, je nikibadilisha redio ya gari ni replace na new Android radios haitasumbua mfumo wa compyuta ya gari

Mshana Jr sijaona km ulijibu haya maswali matatu ya mkuu alikuuliza. Ikikupendeza kaka yatolee majibu tujifunze

Asante
 
Sasa Mshana Jr naomba ushauri wako kuhusu service ya BMW

1. Je service nangoja notification from car computer au nazingatia tu km?
2. Kuna haja ya kutafuta fundi specific wa BMW au hata mafundi wa kawaida?
3. Ni vitu gani hasa vya kubadilisha wakati wa service tofauti na oil? Hata huku Kuna kubadilisha filters?

Ni hayo tu ndugu mbadilisha mawazo, waweza ukawa sio fundi ila kutokana na uzoefu wa kuyatumia haya ukawa na majibu

NB: nafikiria ku enhance music system, je nikibadilisha redio ya gari ni replace na new Android radios haitasumbua mfumo wa compyuta ya gari
Nitaomba nirudi kwako baadae nikujibu kwa weledi
 
Na hii kiukweli inasababisha ajali ya gari za serikali na madereva wanalaumiwa bure maana mafundi wamekariri tu vitu vichache na vingine hata hawana uelewa nao wakati mwingine....

Niliwahi shuhudia dereva mmoja wa boss kazini kwetu, ile V8 ilikuwa inawaka taa kama tatu za kuashiria tatizo kwenye engine, anapeleka garage maalum ya hayo magari ya 'SU' mafundi wanapuuzia inabadilishwa oil na vingine ila zile taa hazizimi, kuna siku imekwenda safari ana-overtake anashtuka brakes hamna hata kidogo na lile dude lilivyo zito linakolea tu na ni SUV ukivuta handbrake kijinga jinga mnapinduka, tunashukuru hakufa mtu huko ndani siku hyo!

Mafundi wengi wa Bongo ndo wanafanya tunaogopa kununua hizi BMW au VW au AUDI, ila kiukweli hizo gari ukizingia zile warnings inazokupa hutakaa upate shida hata siku moja kwenye spares za engine labda kama we ni mtu wa kugonga gonga gari unapasua pasua taa e.t.c ndo utaumia kidogo

Mafundi wa BMW, Audi, VW mbona wapo bongo wengi tu
Ila ukijifanya unabania matumizi uende mwembeni basi utakuja kulia
 
Nnamiliki hio gari pichan
Cc 1995 piston 4 ina turbo na inatumia diesel
Consumption n nzuri sana km 16 kwa lita

Nikiwa barabaran v8 haijawah nishika
View attachment 686106ni aina ya gari inayoaangaliwa kwa jicho la tofauti sana... Likionekana ni gari ghali na la kifahari huku watu wakitishana sana kuhusu ughali wa vipuri na upatikanaji wake wa shida
Lakini nikwambie tu kitu kimoja hakuna gari imara kama BMW na ukiweza kufuata masharti ya kumiliki gari hutakaa ujutie pesa yako
Kama una uwezo wa kununua Brevis, Nissan Fuga au Klugger... Magari ya kijapan yenye engine kubwa na matumizi makubwa ya mafuta... Hakika HUWEZI kushindwa kununua BMW ya kawaida lakini yenye viwango sawa na hizo gari hapo juu.. Huku ukifurahia ulaji mdogo wa mafuta... Mfumo wa BMW uko tofauti sana... Umejengwa kwenye mfumo wa kuokoa ulaji wa mafuta huku nguvu ya mashine ikiwa ni ileile

Gari nyingi za kijapan hazina body ngumu tofauti kabisa na huyu mnyama BMW... Yani hata unapokaa kwenye seat unahisi kabisa umekaa kwenye mashine ya ukweli... Na ni aghalabu kukuta BMW imepinduka kichwa chini mijuu guu

Hizo magari hapo juu nazo spare zake ni ngumu na ghali kupatikana kama BMW tuu... Tena sometimes unaweza kuipata ya mnyama kirahisi zaidi kuliko hizo nyingine
Kingine ni kwamba BMW wana variety of different styles na kila style ni bakora tofauti na hizi nyingine.... Ukikuta mabrevis yote yanafanana

Badili mtazamo wako BMW ni gari ngumu nzuri na sio ghali kama unavyodhani.. Kuwa tofauti... Miliki mnyama... Pichani hapo juu ni 320td fuel consumption ni km 15 kwa Lita sawasawa na duet tuu... Lakini mkiwa rodini mnyama atatamba
 
Nnamiliki hio gari pichan
Cc 1995 piston 4 ina turbo na inatumia diesel
Consumption n nzuri sana km 16 kwa lita

Nikiwa barabaran v8 haijawah nishika
[emoji123][emoji123][emoji123]ziko chache sana bongo
 
Naipenda sana BMW ila kuna hizi nyingine mbili nao zinanitia wazimu, still in dilemma but it’s not an urgent matter right now.
 
Kweli kabisaa mkuu,ni mwendo wa be forward tu.
Hata mimi shuhuda wa hii ishu, gari beforward ni cheap kuliko hio mitandao mengine. Na baadhi ya magari ndio hayo hayo na picha ndio hizo hizo zilizotumika huku na kule zipo. Tradecarview wao ndio kiboko kwa bei za ajabu naona..... nihsakuta BMW 7 series beforward inauzwa $1500 FOB ya 2003 nyeupe, mnyama anaita kabisa ila ingia tradecarview uone bei zao.....
 
na hili ndo tatizo la wabongo wengi...yani nyny mnajali UNAFUU zaidi kuliko USALAMA...

katka kitu ambacho mjapan amefel ni usalama...aisee ukipata ajali na gari za aina ya toyota usalama wako ndan ya gari unakuwa ni mdogo sana...sijui kwa nn watu hamdhamin UHANIwenu mnadhamini UNAFYU

gari za ulaya...BMW..VW nk ni gari ambazo zina kuhakikishia USALAMA wa maisha yako mara ajali inapotokea..kwa kuanza tu Airbag 8 huko...toyota unakuta Airbag 2 tena zote za mbele aisee

Gari za ulaya hazitak ukanjanja...kila kitu kipo kwenye dash board...yan chochote kinachotokea ktk gari utakiona kwenye dashboard

Nilikuwa na TOYOTA premio..nilipata ajali moja hv...gari iliharibika vbya sana wkt ajali haikuwa kubwa kivile..hapo ndo niligundua toyota ni gari mayai sana!!

Nikaamua kuiuza...nikakamata kitu VW touran(ingawa ukipita humu watu wanaiponda sana)..nna mwaka wa 2 huu nnayo na inapiga kazi fresh...haijawah niletea tatizo lolote..sijawah badili chochote zaid ya service tu(narudia,sijawah badili chochote)na gari napiga nayo To and From kazin daily umbali wa kilometa 40+ huko(sasa kwa toyota ningekuwa nishabadili vingapi)

Gari cc 1500 lakn inakula mafuta kiduchu kuliko hata premio yangu niliyokuwa nayo ya cc 1496

Nilichokigundua Wa TZ wanapenda wamiliki gari ila wanaogopa sana maintenance ya gari

Yani mtu anaona ni bora aweke oil ya ya kuungaunga ya 50 or 60k+( km 3000 ) lkn ukimwambia toa 150k ununue ya km 10000(genuine) huko anaona ni hela nyingi kweli..

Kiufupi tu,gari za ulaya hazitak UKANJANJA..na WABONGO wengi wanapenda sana KITONGA

Na mwisho..hapa kazin nnapofanyia kazi...mm peke yangu ndo namiliki chuma cha ulaya...wengine wote ni toyota tu na mmoja ana nissan...inasababisha hd wenzangu wanaogopa kuniazima gari(maana wanaogopa gharama kam likitokea la kutokea)...NDO YALE YALE...UKITONGA
Sio kutishwa na huo ndo ukweli na mimi mwenyewe ni shuhuda!kuna jamaa namfahamu alikuwa na hyo BMW 320 series iligongwa upande mmoja,taa kubwa ya mbele pamoja na side mirror zikavunjika!Alizunguka jiji zima hela anayo spea akakosa ikabidi gari ipaki mpaka spea ilipopatikana kwa kuagiza toka nje na kwa gharama kubwa!!sasa nambie ingekuwa ni toyota angehangaika kiasi hicho?!chukulia angekuwa na brevis,mark 2 au any toyota brand ambayo ni common in TZ angehangaika?!Ukweli ni kwamba unapoamua kununua gari kwa bongo tofauti toyota hakikisha una connection nzuri ya kupata spea mara itakapohitajika,pia uwe na pesa ya kutosha coz haitakuwa cheap km unavodhani!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sio kutishwa na huo ndo ukweli na mimi mwenyewe ni shuhuda!kuna jamaa namfahamu alikuwa na hyo BMW 320 series iligongwa upande mmoja,taa kubwa ya mbele pamoja na side mirror zikavunjika!Alizunguka jiji zima hela anayo spea akakosa ikabidi gari ipaki mpaka spea ilipopatikana kwa kuagiza toka nje na kwa gharama kubwa!!sasa nambie ingekuwa ni toyota angehangaika kiasi hicho?!chukulia angekuwa na brevis,mark 2 au any toyota brand ambayo ni common in TZ angehangaika?!Ukweli ni kwamba unapoamua kununua gari kwa bongo tofauti toyota hakikisha una connection nzuri ya kupata spea mara itakapohitajika,pia uwe na pesa ya kutosha coz haitakuwa cheap km unavodhani!!
spea zipo nyng tu DSM hapo...tatizo wamiliki hawana INFO ya wapi pa kuzipata

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mkuu gudume labda nimekuelewa ila naomba niongeze jambo moja

Embu naomba ulinganishe gari za toyota na za ulaya zenye hadhi moja/gharama zinazoendana alafu uje hapa

mm katika post ya hapo juu nimesema nilikuwa na toyota premio(13-14m) na sasa nna VW Touran(13-14)

Narudia tena kusema...baada ya kuchukua TOURAN...nilijiona fala sana kumiliki TOYOTA...nilipoteza mda na hela yangu tu ktk toyota

Ukilinganisha Speed...comfortability..Usalama..aisee toyota imeachwa mbali sana
bahati mbaya au nzuri mimi hata gari sina. sijawahi miliki tofauti na wewe ambaye ushamiliki nyngi tofaut tofauti mpaka ukagundua Toyota ni Mbolea.
sijaelewa uliposema kuwa hujaona popote niliposema hizo toyota ni gari moja... nifafanulie.

anyway.... hata ungesema toyota ni ya 3 bado ungegundua inastahili heshima yake.lakini nakupa link pia ikusaidie.
Top 10 biggest automakers in the world
so inawezekana zikawa zina badilishana kwa maana ya kuwa na Vokwagen wanampiku Toyota sikatai wakienda wanabadilishana. ila nachozungumza watu wenye kufahamu na waliomiliki au wanaomiliki magari kiukweli kweli wakisikia una watukana watengeneza magari kama Toyota au Nissan n.k watakushangaa sana na wanaweza kufikiria kuwa wewe ni limbukeni kumbe maskini unaweza kuwa na akili yako tu vizuri. ashakum si matusi. hizo unazosema ni mbolea wali zi categorize ni waungu katika top 20 yao. sasa kama unawabishia au wewe unajua zaidi hilo siwezi kukupinga maana najua waswahili ni wajuvi sana.
anyway.. mimi nakwambia hivi ili usiwafanye watu wagundue.ukikaa kimya hawawezi gundua. halafu nikupe hongera sasa wewe unamiliki gari za mjerumani tu kwa kwenda mbele baada ya kudundua Toyota si kitu. mimi nakukubalia kabisa... kwa wenye magari wanasema kuna tofauti. lakini kiuhalisia huwezi kuwa na toyota Verossa ukailinganisha hata na Toyota Crown. au Toyota Verossa/ Spacio ukailinganisha na BMW. hali ni uongo. Toyota wana gari za kumfaa kila mhusika ukiyaangalia yale ma kilimo kwanza huwezi fananisha na RAV 4. na ndo maana hata marais kadhaa wanatumia those cars kama ambavyo wengine wanaamua kutumia escalade au range rover.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mkuu...tatizo mnauziwa vifaa feki vya toyota ndo maana mnadhani toyota ina vipuri vya bei rahisi...mnavyouziwa k.koo vingi si genuine...jaribu tu kuulizia vipuri genuine vya toyota alafu ulete majibu...
All over the internet watu watakuambia bila kupepesa kwamba Toyota ndio kampuni (na Japan ndiyo nchi) inayoongoza kwa kutengeneza magari reliable yanayodumu...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom