Bado fani ya ushonaji ina soko. Mnaoenda VETA someni hiyo

Bado fani ya ushonaji ina soko. Mnaoenda VETA someni hiyo

Upo vizuri sana aisee big up na wakiweza kupata mashine za kushonea kadhaa maisha yanaenda maana naona tunavyolimbizwa kushona uniform za shule za watoto na bei ya vitambaa vyao inapanda kila kulicha..
 
Watu walimcheka Magu Alivyosema Charahani 4 ni kiwanda, ila Personally nimewahi kulipa Kodi 3M na turnover close to 100M kwa Charahani moja.

Kkoo fundi Cherehani anapata 1000 kwa vitu vizito kama Pazia hadi 200 kwa vitu vyepesi kama Vijora.

Siku kukiwa na Biashara kawaida Fundi kulaza zaidi ya laki 1.

Mafundi kibao wanaishi kwao, wamejenga.

Issue hapa ni kuondokana na Butterfly na ushonaji wa zamani, kuingia kwenye Juki na industrial Charahani.

Na huyu ni Fundi asie na skills za maana anajua kupinda, Fundi mzuri wa Nguo wanachaji pesa ndefu mno.
Binafsi ningeshauri serikali ingewapa au kuwakopesha vijana wenye passion ya hii kitu ili waweze kununua vitendea kazi vya kisasa na kufanya kazi nzuri. Hakuna haja yaa kukopesha vikundi vya vijana hela kidogo wasiyoweza kufanyia chochote wakati ingeweza kukopesha mpunga wa kutosha kwa ambao tayari wameshaanza ili baadae watoe ajira kwa wengine.
 
Morogoro kuna dada ana kiwanda Cha kushona t shirts,. long sleeves and Short sleeves,same color t shirts,Zina ubora kuzidi Manga or hot basic za China..moja anauza elfu 3 kwa bei ya JUMLA ,anapiga sana hela ana wafanyakazi zaidi ya 10...wenye maduka wanafata t shirt kwake..nishanunua. Tisheti 200 kwake
Morogoro sehem gan boss
 
Binafsi ningeshauri serikali ingewapa au kuwakopesha vijana wenye passion ya hii kitu ili waweze kununua vitendea kazi vya kisasa na kufanya kazi nzuri. Hakuna haja yaa kukopesha vikundi vya vijana hela kidogo wasiyoweza kufanyia chochote wakati ingeweza kukopesha mpunga wa kutosha kwa ambao tayari wameshaanza ili baadae watoe ajira kwa wengine.
Kwa ninavyofahamu Sido wanatoa hizi Facilities. Mpaka Cherehani wana Meza na vitu vingi wanatengeneza wenyewe, tatizo lililopo ni hio obsession ya Butterfly. Yale mambo ya Unashona Nguo siku 2 ama 3.

Zile Charahani industrial bado sana, na wachache sana ambao wana take advantage ya kushona vitu in bulk.
 
Morogoro sehem gan boss
Area 6 pale kanisa la wasabato njiani Kama unaenda Kola, pandisha na barabara umbali wa mita 200 Kuna hotel sijui lodge ipo njiani,uliza kwa Salma wanaposhona,ni muhindi Salma mwenyewe,..or ongea na bodaboda pale ni buku tu.. number zake nimepoteza..
 
Miaka kadhaa iliyopita nilibahatika kutembelea eneo la viwanda vya ushonaji huko Huanghuagang karibu na Ouzhuang & Dongshankou jimboni Guangdong, nchini China nikajifunza mengi. Ila kikubwa zaidi nilichojifunza ni kuwa wachina walichotuzidi ni skills tu kwenye ushonaji. Mashine wanazotumia ni hizi hizi cherehani tuzozijua ila skills zao ndo zinafanya nguo wanazoshona ziwe tofauti na za mafundi wetu. Nguo iliyoshonwa na mchina na iliyoshonwa na mbongo ni rahisi kuzitambua. Hii inahusu pia seremala na fani zingine.

Huu uzi nimeandika baada ya members ndugu Jerry001 , lost files na binti kiziwi ku-comment kwenye uzi mwingine kuhusu fani ya ushonaji. Naungana nao kuwa bado ni fani yenye soko inayoweza kumfanya mtu asilale njaa. Cha muhimu VETA wawe na waalimu wazuri huku vijana nao wakijiongeza na kujibidiisha kuongeza ujuzi. Hii itasaidia kuwa na mafundi wenye kazi nzuri wanaoweza kushindana kimataifa. Tukiwa na mafundi wazuri itapunguza kununua malonya ya kichina.

Pia ninaisihi serikali ije na mipango mizuri kuhusu FABRICS... kodi ipunguzwe kwa viwanda vya fabrics nchini ili kuwe na urahisi wa viwanda vidogo vidogo kumudu kushona nguo na kuuza kwa bei shindani. Kwa sasa nguo za kushona ni ghali kwa sababu ya ughali wa fabrics.
Ni kweli mkuu Mafundi wetu wanashona kienyeji sana na kimazoea, yani CCM wajinga sana Raisi wa nchi anapeleka wasanii nje ya nchi kutalii baadala awachukue Vijana mafundi kushona wakajifunze jinsi wenzetu wanavyofanya kazi za ushonaji kitaalamu, Niliona kwenye TV mafundi fundi nguo wa China na Ulaya wanashona nguo kwa kutumia vifaa kama vya mafundi wetu ila baadhi ya vifaa mafundi wetu hawana ndiyo inaleta utofauti kwenye finishing wao Nguo zao zinaonekana bora kuliko zetu, mfano Fundi wetu akishona Uniform watoto wa shule zinakua tofauti na Uniform aliyoshona fundi wa Nyumbani waKichina
 
Ni kazi inayolipa ukiwa na mashine za kisasa,nina jamaa yangu mmoja hiyo kazi imemkubali mpaka kajenga gorofa tena sio moja na mambo yamemnyookea haswa.Mtaji na wateja ni kitu muhimu sana hapo
 
fdt2.png
 
Back
Top Bottom