Bado fani ya ushonaji ina soko. Mnaoenda VETA someni hiyo

Upo vizuri sana aisee big up na wakiweza kupata mashine za kushonea kadhaa maisha yanaenda maana naona tunavyolimbizwa kushona uniform za shule za watoto na bei ya vitambaa vyao inapanda kila kulicha..
 
Binafsi ningeshauri serikali ingewapa au kuwakopesha vijana wenye passion ya hii kitu ili waweze kununua vitendea kazi vya kisasa na kufanya kazi nzuri. Hakuna haja yaa kukopesha vikundi vya vijana hela kidogo wasiyoweza kufanyia chochote wakati ingeweza kukopesha mpunga wa kutosha kwa ambao tayari wameshaanza ili baadae watoe ajira kwa wengine.
 
Morogoro sehem gan boss
 
Kwa ninavyofahamu Sido wanatoa hizi Facilities. Mpaka Cherehani wana Meza na vitu vingi wanatengeneza wenyewe, tatizo lililopo ni hio obsession ya Butterfly. Yale mambo ya Unashona Nguo siku 2 ama 3.

Zile Charahani industrial bado sana, na wachache sana ambao wana take advantage ya kushona vitu in bulk.
 
Morogoro sehem gan boss
Area 6 pale kanisa la wasabato njiani Kama unaenda Kola, pandisha na barabara umbali wa mita 200 Kuna hotel sijui lodge ipo njiani,uliza kwa Salma wanaposhona,ni muhindi Salma mwenyewe,..or ongea na bodaboda pale ni buku tu.. number zake nimepoteza..
 
Ni kweli mkuu Mafundi wetu wanashona kienyeji sana na kimazoea, yani CCM wajinga sana Raisi wa nchi anapeleka wasanii nje ya nchi kutalii baadala awachukue Vijana mafundi kushona wakajifunze jinsi wenzetu wanavyofanya kazi za ushonaji kitaalamu, Niliona kwenye TV mafundi fundi nguo wa China na Ulaya wanashona nguo kwa kutumia vifaa kama vya mafundi wetu ila baadhi ya vifaa mafundi wetu hawana ndiyo inaleta utofauti kwenye finishing wao Nguo zao zinaonekana bora kuliko zetu, mfano Fundi wetu akishona Uniform watoto wa shule zinakua tofauti na Uniform aliyoshona fundi wa Nyumbani waKichina
 
Ni kazi inayolipa ukiwa na mashine za kisasa,nina jamaa yangu mmoja hiyo kazi imemkubali mpaka kajenga gorofa tena sio moja na mambo yamemnyookea haswa.Mtaji na wateja ni kitu muhimu sana hapo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…