Bado kuna wazazi wanaendelea kuzaa hata baada ya mtoto wao wa kwanza kuolewa? Mtoto wa mwisho analingana na mjukuu wa kwanza? Huku ni kukosa maadili

Bado kuna wazazi wanaendelea kuzaa hata baada ya mtoto wao wa kwanza kuolewa? Mtoto wa mwisho analingana na mjukuu wa kwanza? Huku ni kukosa maadili

Kwa makabila ya mkoa wa mara baba na mtoto wanaweza kutofautiana miaka miwili. How possible:

Baba akipata mtoto wa kiume uzeeni hulazimika kumuozesha ili ashuhudie wajukuu na humuozesha kwa mature woman, woman akizaa watoto huitwa wa huyo mtoto wa kiume
Aisee..sijakupata vizuri. Siyo wanawake ndiyo wana hizo mila
 
Haipendezi ,wazazi wa zamani walikuwa wanatwanga fasta fasta ,wanapishana mwaka mmoja hadi miwili anazaa watoto wa5 hadi 10. ukipiga gap hapo Mtoto wa kwanza hadi wa mwisho wanapishana miaka 10 hadi 15......Hadi Mtoto wa kwanza anaoelewa/oa lets say miaka 24 hapo mtoto wa mwisho anakuwa na miaka 9 ambapo Mama mtu alishafunga uzazi miaka 9 iliyopita.
Uswahilini ni dhambi kufunga kizazi. Hao uliozaa Mungu akiwapenda zaidi na wewe kizazi ushampa paka!
 
Imani za kizamani eti kuzaa watoto ni baraka
Halafu unaposema uwezo ni kitu relative mwingine uwezo kwake ni kuwapeleka watoto international school ndio anajiona ana uwezo, mwingine akiweza kuwalisha ugali maharage usiku naye anajiona Ana uwezo
Whatever the case 3 children should be a maximum for everybody


Hapana! Unakosea kusema for everybody!!

Tuzae kwa mpangilio na uwezo! You can still have ten kids and afford to take care of all the necessities ikiwa ni pamoja na huduma bora kabisa za afya na elimu, malazi na chakula! Na sio bora huduma!!
 
Katika vitu natamani maishani Basi Ni watoto wengi,, ingelikuwa nimezaliwa enzi za mabibi zangu, nikawa ktk hali nzuri kihuduma na afya watoto 12-15 ningewazaa,,
Ila kwa usasa huu nitajitahidi kufanya nusu yake,

Nikirudi kwenye mada yako umeileta mada as if unajua historia ya wanawake wote ktk uzazi wao, marehemu baba yangu alizaliwa style hii hii maana tayari dada yake alikuwa kashaolewa na kuzaa binti yake hivyo yeye (baba) alizidiwa miaka 2 na mpwa wake,,

Ni kawaida sana kwa mama kuzaa pamoja na binti yake na hii hutokea sana km firstborn akiwa ni wa kike na Kama ujuavyo wanawake wengi vijijini wanaolewa 17-22, Sasa akipata mtoto ktk umri huo na akawa wa kike,, huyo binti nae akikua akaolewa umri km wa mama yake uwezekano wa kukutana clinic Ni mkubwa mno

Wanawake wengi wanachofanya kukwepa maneno ya washenzi km wewe mtoa mada huwa wanatoa mimba kukwepa eti 'aibu'
,Bibi yangu angefanya huu ujinga ni wazi nisingeiona hii dunia,
nasikia unajiita last born, mada ya leo umetumia akili zako za kilast born maana huwa mnadeka na kulalamika ovyo tu,

mwisho kabisa Kama Jambo analofanya mwingine halikudhuru Basi tupunguze shobo na viherehere kwenye maisha ya wengine
 
Sio jambo zuri kuzaa ikiwa mtoto ako tayar kaisha pevuka, ila kuna mda inabid iwe hvyo
Mfano:- mtu nimezaa nikiwa na miaka 18 (ilikuwa bahata mbaya na sikutaka abortion) baada ya hapo nikasema sasa naitaji kurekebisha makosa, nikaamua kutulia kuanza kuandaa life langu kwanza ( nikarudi school) ndio nije nizae tena hapo nakuja kusema sasa naitaji mtoto wa pili nina miaka 35 mtoto wa kwanza kaisha vunja ungo tayari. Unazania nn kitatokea kwa kizazi hiki
Huyo mtoto wa pili wataka kumpata kibahati mbaya ama ushapata mume?
Na huyo mume itabidi umwangalie vizuri asije akala kuku na mayai yake maana ushasema mtoto keshavunja ungo tayari.
 
Habari za wakati huu kaka na dada zangu wote wa hapa jamiiforums.

Ndugu zangu Watanzania;

Bado kuna watu wazima wanaendelea kuzaa hata baada ya mtoto wao wa kwanza kuolewa? Mtoto wa mwisho analingana na mjukuu wa kwanza? Huku ni kukosa maadili.

View attachment 1667340

Siku ya sherehe ya mwaka mpya nilikuwatana na dada mmoja anaitwa Veronica (hili sio jina lake halisi) ambaye nilimaliza naye shule ya msingi mwaka 1999.

Huyu dada nilikwisha kutana naye mwezi kama wa August maeneo ya Banana Ukonga huku Dar. Kwa kuwa tulikuwa hatujaonana miaka takribani 15 tulipiga story nyingi sana za zamani.

Sasa nilipokutana naye tena Ijumaa ya tarehe 01 January 2020 huku Kivule ninapokaa (kwa maana aliniambia anakaa Kata moja na mimi) nilimuona anaongozana na binti mdogo wa miaka kama 9 hivi.

Tena huyo binti wamefanana kweli kweli. Basi tulipoonana tulisalimiana tena kwa furaha sana. Baada ya story kadhaa nikamuuliza, huyu ndio mtoto wako wa kwanza? Akakataa. Akasema hapana, huyu sio mtoto wangu.

View attachment 1667350

Huyu ni mdogo wangu wa mwisho. Mtoto wangu ameenda kwa baba yake kusalimia atarudi shule zikifunguliwa. Sema ndio rafiki yake mkubwa sana huyu (mdogo wake wa mwisho) kwa maana wamepishana mwaka mmoja tu.

Mimi sikuwa na jambo lingine la kumwambia zaidi tu ya kumpa hongera lakini nikawa ninajisemea tu kimoyomoyo "ina maana haya masuala ya mtoto na mama kuzaa kwa pamoja bado yanaendelea katika karne hii ya 21?"

Hii issue nilikuwa ninaiona tu kwa wazee wa zamani ambapo unakuta mtu unakutambulisha "huyu ndio baba yangu mdogo/shangazi yangu tumbo moja na baba" au "huyu ndio mama yangu mdogo tumbo moja na mama" lakini ukijaribu kuwatazama actually wanalingana umri au wamepishana mwaka mmoja tu.

View attachment 1667352

Mimi ni moja kati ya watu wanaokerwa sana na lugha za hawa dada/mama zetu manesi lakini linapokuja suala la kukemea wamama/wababa wanaoendeleza utamaduni huu wa hovyo mimi ninawaunga mkono sana.

Kuna mtoto wa shangazi yangu mmoja yeye ni nurse huko Geita anakwambia mama mtu mzima wa design hii akija kujifungua (wanawafahamu sana kwa maana vijijini watu ni wachache) huwa wanawachamba kwa maneno na lugha chafu mbele ya waume zao.

Kuna mama mmoja aliwahi kufariki mwaka 2006 alipokuwa anajifungua wakati bado tunakaa kule Keko. Sasa wakati wa mazishi watu wamekusanyika na wageni wanataka kujua chanzo cha kifo chake ikawa sasa ni aibu kusema kuwa amelufa kwa sababu ya "complications" za uzazi ilhali binti yake mkubwa ana mtoto wa miaka 2 tayari.

View attachment 1667341

Mimi binafsi ninaona sio jambo la hekima wala busara kwa mama/baba kuendelea kuzaa watoto wengine wadogo ilhali wale "first born" wamekwisha kuwa wababa/wamama wanaokaribia ku-reproduce.

Sio vizuri mama kuonekana ana tumbo kubwa la ujauzito pindi wale "first borns" wanapokuwa wamepevuka akili.

Kwa maoni yako, ni sahihi mama na binti/mtoto kuendelea kuzaa kwa pamoja? Mtoto wa mwisho kulingana na mjukuu wa kwanza?

"HAPPY NEW YEAR 2021"

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.

Maoni ya wadau
=====
Wakubwa wakizaa wewe unadhurika nini?
Mradi hawazai na wewe kuna shida ipi?
 
Kwani wazungu ndio wanazaa watoto wachache peke yao? Nenda Korea, nenda Japan, nenda Qatar huko kote sio wazungu na wana familia ndogo, stable na zenye mafanikio, na future za watoto wao zipo guaranteed
Wewe umeweza tu kuwalisha ugali maharage unajiona una uweeeezoooo, eti uchumi wangu upo stable...
Zaeni mkaijaze nchi...
Km unaweza kufikiri kuwa watoto wawili wataweza kufanya uwe na furaha,
Sasa kwann umuogope anaepata furaha yake kwa kuwa na watoto wengi?
Tuwajal watoto.
 
Uko sahihi, kama uwezo unaruhusu zaa sana tena sana ila pia jaribu kuweka mipangilio katika kuzaa kwako!

Anza mapema kisha maliza mapema ili kujipa muda wewe wa kutafuta na kujenga misingi imara ya familia ili hata kuanzia mwanao wa mwanzo apate muda wa kufundishwa na mwalimu wake wa kwanza maishani (baba & mama)!

Tusijisahau familia sio baba mama na watoto tu , maana kadri muda unavyosogea wajukuu na wakwe wa kike na kiume nao wataongezeka kuwa sehemu ya hiyo familia! So ulezi bado unaendelea!

Otherwise make your grand kids your kids, there is wisdom in that!
Acha uoga mkuu...
Sheria yoyota iliyotofauti na nature ni batili!
 
Back
Top Bottom