Bado natafuta mantiki ya kujenga hili Daraja la Kigongo - Busisi kwa Tshs. Bilioni 700

Hatuna nia mbaya ya kuwasema Watanzania wengine ila kiukweli daraja la Kigongo - Busisi hakuna kiongozi ndani ya nchi hii mwingine yeyote yule ambaye angechaguliwa akubaliane na ujenzi huu. Hili daraja limejengwa ili tu fulani na watu wake waulazimishe uwanja wa Chato uwe mbadala wa uwanja wa ndege wa mwanza! Ni hilo tu!

Zinatumika fedha nyingi za walipakodi pasipo mipangilio mizuri. Hizi kodi tunalipa watanzania wote hivyo ni lazima zitumike vizuri na siyo haya tunayoyaona sasa!

Hata kama wanachato watakasirika kwa sisi kuusema ukweli basi na wakasirike ila kiukweli mambo haya hayakubaliki!

Gharama za ujenzi wa hili daraja ni kubwa mno. Ni mradi wa hasara na unafanyika ili tu matakwa fulani yatimie. Haiwezekani miradi miwili tu ya uwanja wa Chato na daraja la kuufikia uwanja huo kwa urahisi vigharimu Tshs zaidi ya trilioni moja! Hapana!

 
Kwahiyo kwasababu kiongozi fulani kwakuwa ana mamlaka ya kutumia kodi za Watanzania basi azitumie atakavyo hata kama watu watapigika? Hapana!
 
Huyu jamaa ana wivu kweli. Miaka ijayo Mwanza itakua ni moja ya makini makubwa na Population ya watu inaongezeka KILA leo,
Mwanza NI kitovu cha Biashara Kwa mikoa zaidi ya nane!!

Mikoa hiyo INA jumla ya wakazi Milion 15.
 
Kwahiyo kwasababu kiongozi fulani kwakuwa ana mamlaka ya kutumia kodi za watanzania basi azitumie atakavyo hata kama watu watapigika? Hapana!
Daraja lile ni muhimu sana
 
Huu upumbavu wa kujenga miradi ya matrilioni isiyo na faida ni wa kupingwa na kila mtanzania anayejitambua!
 
Kwan hzo kodi zinatumika Uganda? Chato na mwanza sio watanzania , unataka watanzania wa wap?
Kwahiyo kwakuwa ni Tanzania basi tutumie tu hovyo hovyo?
 
Ultimately dictator is no friend to anybody except himself!

A good dictator is only the dead one!
 
Ni heri angelipa madeni ya ndani ili ku stimulate uchumi na kuongeza mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu. Daraja hio sio priority kwa kweli.
 
Hilo daraja litakuwepo kea miaka 600, kila siku likiingiza 10m kwa miaka 600 si ni faida? Hizi ferry zinaendeshwa kea hasara safari mmoja unatumia mafuta ya 5m wakati nauli ni mianne kea kichwa huoni hiyo hasara?
Unajua watu wengine hawajui faida yake na jinsi litakavojilipa.ikiwa siku mmoja litaingiza sh million 10 kwa siku,kwa mwaka ni siku 365 mara 10,000,000=3,650,000,000 ni biliion 3.65

Basi kwa mapato ya daraja hili miaka 50 litaweza kujenga madaraja nchi nzima bila kutegemea serikali.
 
Wajinga ni wengi! Unataka daraja lirudishe pesa hizo kwa nani? Hiyo ni biashara?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…