Bado natafuta mantiki ya kujenga hili Daraja la Kigongo - Busisi kwa Tshs. Bilioni 700

Bado natafuta mantiki ya kujenga hili Daraja la Kigongo - Busisi kwa Tshs. Bilioni 700

Lissu hajainasa hii? Limzee linaifungua Geita na Chato maana ndio kwao,huu ni ubinafsi wa wazi sana mpaka mikutano ya kitaifa inafanyikia kwao hii haijawahi tokea wakati wowote ndio tunaona kwa bwana mkubwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tukisema kuwa Magufuli ni mkurupukaji na alipaswa kuwa Mnyapara wa KUSIMAMIA BARABARA na si kumpa Ikulu wanabisha!!
Watu aina ya Magufuli wanatakiwa kusimamiwa yaani wawe chini ya mtu fulani awatume na kuwasimamia tu.

Haiwezekani 700 Bilioni uziteketeze kwenye Daraja la Busisi ambao halina Tija kabisa. Mbaya zaidi hakuna Bunge la Bajeti lililokaa kupitisha hiyo Fedha. Kweli huyu ni Rais wa ajabu ambaye Tanzania haijawahi kuwa naye!!!
Unalala na kuamka kwa sehemeji yako!

Kwanini usione ni bora kujenga uwanja wa mpira kuliko daraja?
 
Hapo ndipo unafeli! Nilishawahi kukaa hapo masaa 4 nikisubiri awamu yetu ifike. Uamuzi wa kuweka daraja ni wa kishujaa ila sema ubinafsi umewajaa kwa vile huitumii hiyo Njia ndiyo maana unaponda huo uamuzi uliotukuka.
Maisha haya hayana fomula huenda hata hawa wanaopinga kwa sasa ndio wakaja kuwa watumiaji wazuri wa hilo daraja maana daraja ni kwa ajili ya watanzania wote wataokaosafiri kwa njia hiyo kwenda sehemu mbalimbali. Kwani Daraja la Mkapa wanapita watu wa kanda ya kusini peke yao? Au daraja la Mto Malagalasi ni kwa ajili ya watu wa mikoa ya magharibi tu. TENDA WEMA UENDE ZAKO JPM MAANA HATA UKIWALAMBA MIGUU BADO WATAKULAUMU KWAMBA HUJAWALAMBA MAKALIO!
 
Hizi hela wanazopoteza kwenye miradi hii ambayo hairudishi pesa zingewekwa katika kuwapatia vijana active kufanya project zao. Tungepata return nzuri sana ya pesa zetu tunazowekeza.
 
Mzee wa tanzia, kuna siku utatafuta mantiki ya wewe kupumua.
 
Lissu alipita hapo kigongo ferry akaubeza huo mradi lakini mhe Magufuli aliusifia na kueleza umuhimu wake. Ngoja tuone tar 28 wananchi watatuambia.

Mimi ninavyofahamu hilo eneo kwa siku linapitisha magari na watu wengi sana. Kuvuka kwa kivuko inakula kama dk 30 mpaka 45.
Ikifika usiku, unaweza kujikuta unakaa masaa mawili ndipo uvuke. Hilo darala ni muhimu sana kwa mikoa ya Mwanza, Geita, Kagera, Mara na hata nchi jirani kama Rwanda na Uganda.
 
Weka mantiki ya kujenga daraja la Nyerere Kigamboni na lile linalojengwa la Coco Beach salenda pale.
 
Kuna msemo unasema if you want to please everyone go and sell ice cream na kazi ya Uraisi haihusiani na kuuza Ice cream so sio kila mtu will be pleased na matendo yake.

Kumridhisha kila binadamu ht Mwenyezi Mungu hajawahi kuweza na ndio maana pamoja na pumzi za bure tunazovuta na bado kuna wanadamu wamechagua njia za kishetani.

That being said tusitegemee kua kila analofanya Magufuli everyone will be pleased.

Kama hujawahi kupanda kivuko pale then Magugu maji yakasababisha feri isifike upade wa pili ukawa upo katikaji ya Maji roho mkononi huwezi Jua umuhimu.

Kama huwajawahi kukaa 4hrs kusubiri zamu yako kuvuka huwezi Elewa.

Kama hujawahi kufiwa na mgonjwa akiwa anasuburi kuvuka then huwezi elewa uchungu wa waliofiwa just wait for ur turn.

Kama hujawahi kuwaza feri inaweza kuzama ikaleta maafa ambayo thamani yake hailingani na hio 700b then Kichwa yako haipo sawa.

Mentality km hizi huwezi kuta wanazo Maraisi only Low IQ people wenye karoho ka kwann huku na sio huku ht km kinachofanyika ni kitu cha maendeleo na ndio maana Daraja la Maragarasi, Mkapa, Kigamboni na Kilombero yalijengwa ingawa Kulikua na Feri, na walipoyajenga hawakutazama Return of investment walitazama zaidi kutoa huduma na kuokoa maisha ya watu

Anyway waswahili wanasemea jambo usilo lijua ni sawa na usiku wa giza(ya busisi hawayajui)...so for now wacha tuwape benefit of the doubt wasemezane wanavyoweza ila daraja ndo linajengwa there is nothing they can do to stop it zaidi ya kupiga domo.
 
G Sam,

Hadi amalize hiyo miaka 10 kama akishinda, Taifa hili litakuwa vipandevipande kikabila, kikanda na kidini.
 
[QUOTE="HATA UKIWALAMBA MIGUU BADO WATAKULAUMU KWAMBA HUJAWALAMBA MAKALIO!
[/QUOTE]
Hahahahahaha
 
Suluhisho basi ni serikali za majimbo..
Hata ingeelekezwa kwenye barabara, bado mngekuja na kudai, no bora hizo hela wangegawiwa masikini mikopo isiyokuwa na riba[emoji2], nyinyi hamueleweki mnachokitaka.
 
Ccm ndio vibaraka wa mabeberu. Hadi NEC leo wametangaza kuto mtangaza rafiki wa mabeberu.
Hakuna anayeng'ang'ania Ikulu ila hatuna chama mbadala wa CCM, hivyo nchi yetu haiwezi kuongozwa na vibaraka wa mabeberu. Upo hapo?
 
Unaona sasa?

Chato ndio wapi huko? Kuna nini?
Ina maana kile kijiji chenye international Airport kama Gbadolite hukijui? Hakichangii hata bil 200 ya kodi kwa mwaka ila kina kila kitu kushinda Kilwa mnakoendeshea nchi kwa kutumia gas yao!
 
Suluhisho basi ni serikali za majimbo..
Maendeleo yakipangwa kulingana na rasilimali zinazopatikana kwenye majimbo, Unaiangalia singida kwenye nafasi gani[emoji848]?Ni dhahiri bado Mwanza ingesitahili hiyo miradi.
 
Una dhana potofu juu ya serikali za majimbo..
Maendeleo yakipangwa kulingana na rasilimali zinazopatikana kwenye majimbo, Unaiangalia singida kwenye nafasi gani[emoji848]?Ni dhahiri bado Mwanza ingesitahili hiyo miradi.
 
Back
Top Bottom