Bado natafuta mantiki ya kujenga hili Daraja la Kigongo - Busisi kwa Tshs. Bilioni 700

Bado natafuta mantiki ya kujenga hili Daraja la Kigongo - Busisi kwa Tshs. Bilioni 700

Dunia inavyoenda kasi hivi.

Watu wanatandaza reli baharini kutoka jimbo moja hadi jingine. Wewe unawaza vivuko?

Huu ujinga ndo unanifanyaga nisite kupiga kura baadhi ya vyama maana akili zao hazina tofauti na huyu member wao.
 
Kivipi bwana project kubwa hivo inatakiwa kuwa na business plan pesa ya umma unasema hivo angalia asije mtu akaja kubananishwa kizimbani nakumbuka Chiluba ilimtokea hivo hivo bila kutegemea
Huwezi fungua biashara na ukategemea faida wakati huo huo; hilo daraja hata kuokoa maisha ya wagonjwa ni faida kubwa
 
Wewe ni kiazi watu Wana suffer unazungumzia habari ya mbeleni,natamani maviongozi yote ya ccm yangefia jela tu huko,ndio maana huwa Kuna wanauchumi kufanya cost benefit analysis,kipi kifanyike sasa na kipi mda wa Kati na kipi Cha baadae ,vyote vinafanywa kwa principal za uchumi sio kwa utaratibu wa ndoto za usiku za mtu mmja
Acha kutumia akili za kushikiwa; hakuna kitu kibaya kama kumeza kila neno unaloambiwa na hao waropokaji
 
Ukianzisha kiwanda usimpe mwanaccm kukiendesha, unampa CEO mwenye uwezo hata kutoka nje ya nchi, kama wafanyavyo akina Bakhressa, Mo nk. Fuatilia vizuri viwanda vyote enzi za Nyerere viliuliwa na kamati za chama zilizokuwa ndani ya viwanda. Sio uumpe CEO, halafu umuelekeze kupika data, na kushinda kwenye mbio za mwenge.
Sema kwamba pesa husiyoiangaikia haina uchungu ni vizuri tu serikali iendelee kujenga miundo mbinu na wafanyabiashara wapunguziwe riba wakope waanzishe viwanda ,viwanda navyo vinaushindani we uoni ku
 
Lissu alipita hapo kigongo ferry akaubeza huo mradi lakini mhe Magufuli aliusifia na kueleza umuhimu wake. Ngoja tuone tar 28 wananchi watatuambia.

Mimi ninavyofahamu hilo eneo kwa siku linapitisha magari na watu wengi sana. Kuvuka kwa kivuko inakula kama dk 30 mpaka 45.
Jpm atakosaje kuusifia au hujui Magufuri ni nani katka nchi hii.
 
Nimeishia darasa la saba la ukweli, lakini nina uelewa wa kuridhisha wa mambo. Unaweza kuanzia hapo boss.
Nimeuliza taaluma unayoiweza, wewe unajibu darsa la saba. Nasema tena taaluma!!!!
 
Sio jambo baya. Ningeruhusiwa kushauri ningependekeza tumalizane na 200 bn ya korosho kwanza.
 
Vifaa mbalimbali vya plastiki kama mabeseni, ndoo, pipes za maji safi na majitaka. Pia viwanda vya maziwa na ngozi kwani huko kanda ya ziwa ni sehemu ya wafugaji. Unataka nikuongezee matumizi sahihi mengine ya 700b?
Sasa hizo project unazo zungumzia mbona ni ndogo ambazo Mimi na wewe tunaweza kwenda kukopa na kuanzisha hivyo viwanda.
Serikali inapobidi ku invest inatakiwa iwe ni kwenye mega project , ambazo Mimi na wewe hatuwezi ku-invest na inakuwa ktk strategic areas or industry.

Pili management ya viwanda vidogo vidogo kwa serikali ni ngumu kuviongozo huku mkisema serikali isifanye biashara.
 
Nimeuliza taaluma unayoiweza, wewe unajibu darsa la saba. Nasema tena taaluma!!!!

Darasa la saba kuna taaluma gani boss? Ww ulivyomaliza darasa la saba ulikuwa na taaluma gani? Mimi kazi zangu ni za nguvu, kama ujuavyo kazi za nguvu sio taaluma zaidi ya afya njema. Labda kama hujui unauliza nini.
 
Sema kwamba pesa husiyoiangaikia haina uchungu ni vizuri tu serikali iendelee kujenga miundo mbinu na wafanyabiashara wapunguziwe riba wakope waanzishe viwanda ,viwanda navyo vinaushindani we uoni ku

Mkuu ndege moja imenunuliwa kwa 200b+, je ndege hazina ushindan? Hivi hizo 200b+ zingejenga kiwanda cha vifaa vya plastiki kisha kikapewa upendeleo maalum, serekali inunue bidhaa zake kama mabomba, conduit pipes za miradi ya serikali, within 5yrs itakuwa hiyo hela haijarudi? Na kwa vyovyote vile kiwanda cha 200b ni lazima kitaajiri wafanyakazi kwa uchache 500.
 
Lissu alipita hapo kigongo ferry akaubeza huo mradi lakini mhe Magufuli aliusifia na kueleza umuhimu wake. Ngoja tuone tar 28 wananchi watatuambia.

Mimi ninavyofahamu hilo eneo kwa siku linapitisha magari na watu wengi sana. Kuvuka kwa kivuko inakula kama dk 30 mpaka 45.

Kila kitu ni muhimu ndugu.

The problem ni limited resources.

Kilicho muhimu ni vipaumbele (priorities) kipi cha muhimu kianze na kipi kifuate/kisubiri baadaye.

Hebu chukulia mfano juu;

Mgombea wa CCM ndg John Pombe Magufuli alipoona anashambuliwa sana kuhusu kujijengea uwanja wa ndege Chato kijijini kwake.

Kama kujibu hoja hiyo, bila kufikiria na kama mwendelezo wa makosa yake, akaahidi kujenga vingine 11 akichahuliwa tena!

Sasa fikiri haya;

Hivi ujenzi wa viwanja vipya 11 vya ndege kama kile cha Chato ndiyo hitaji muhimu kwa watanzania kwa sasa kuliko maji ambalo ndilo tatizo kubwa karibu 80% ya eneo lote la nchi hii?

Kama ni hivi, basi ni kweli tukutane Oktoba 28, 2020.
 
G Sam,

Usisahau kuwauliza Wananchi na wadau wa Kigamboni, Coco Beach, Ubungo ,Tazara, Buguruni , Furahisha, Mabatini, njia panda ya mloganzila nk umuhimu wa madaraja katika shughuli zao za kila siku. Ukijifungia humu tu hasa ukiwa na nia ovu ya kukosoa kila kitu ni ngumu kupata jibu.
 
Acha kutumia akili za kushikiwa; hakuna kitu kibaya kama kumeza kila neno unaloambiwa na hao waropokaji
Nashikiwa na nani? Naambiwa na nani? Kwa taarifa yako wanaoshikiwa ni nyie mbogamboga Mimi ni free soul na sio member wa chama au kundi lolote la kisiasa japo mlengo wangu ni upinzani ilimradi tu uwe kwenye kutetea maslahi ya wananchi nikiwamo Mimi.
Maoni yangu ni my own thinking and understanding
 
Mkuu ndege moja imenunuliwa kwa 200b+, je ndege hazina ushindan? Hivi hizo 200b+ zingejenga kiwanda cha vifaa vya plastiki kisha kikapewa upendeleo maalum, serekali inunue bidhaa zake kama mabomba, conduit pipes za miradi ya serikali, within 5yrs itakuwa hiyo hela haijarudi? Na kwa vyovyote vile kiwanda cha 200b ni lazima kitaajiri wafanyakazi kwa uchache 500.
Kiwanda bila miundombinu ni bure! Ni kama kuvuna nyanya nyingi sana kijijini kwenu halafu hakuna usafiri wa barabara wa uhakika kuunganisha uzalishaji na soko. Hatua ya kwanza ndiyo hiyo anayofanya JPM yaani miundombinu, umeme wa uhakika, shule ili kupata raslimali watu, awareness, skills nk halafu viwanda. Soma vizuri ilani ya uchaguzi ya CCM 2020-2025 ambayo imeambatishwa. Nasikia kuna vyama vinafanya kampeni bila Ilani wanasubiri wadese ndiyo wapate Ilani zao.
 

Attachments

Si kila daraja lipo kwa ajili ya kupata faida. Mwanza kuna hospitali kubwa ya kanda, unapotumia feri wagonjwa wanachelewa kuvuka na kuhatarisha uhai/afya wao/zao.

Pia kivuko cha feri hakiaminiki si tu kwa usalama lakini pia hata utengemano si muda wote kitakuwa kizima.

Na inawezekana hata kwa mwaka hujawahi kupita katika njia hii ndio maana unabeza.

NOTE: NIMEKUJIBU LAKINI NATAMBUA WAZI UPO MLENGO WA KUPINGA.
Hili wazo ni mfu sana, hiyo billion 700 inaweza kujenga hospitali zaidi ya tano na vifaa vya kisasa wagonjwa wakawa wanatibiwa hapo kuliko kuanza kusumbuka kubeba wagonjwa feri Hadi bugando.

Nyie Lumumba 'ufikiriaji' wenu unatia ukakasi mno
 
Huwa ninafanya kazi za vibarua zinazohitaji nguvu na akili kidogo. Ila nje ya kazi za nguvu, nina ulewa wa kuridhisha wa mambo.
Go for jobs that need more of the brain power!
 
Dunia inavyoenda kasi hivi. Watu wanatandaza reli baharini kutoka jimbo moja hadi jingine.

Wewe unawaza vivuko? Huu ujinga ndo unanifanyaga nisite kupiga kura baadhi ya vyama maana akili zao hazina tofauti na huyu member wao.

..hao hawana shida ya maji, umeme, madarasa, na shida nyingine tulizonazo waTanzania.

..hoja ni kwamba billioni 700 zingeweza kutatua shida nyingi za wananchi wa kanda ya ziwa, badala ya kuzitumia zote kujenga daraja.
 
Hapa ndipo daraja la Tshs bilioni 700, fedha ambazo hata hazikujadiliwa na bunge zinatumika. Eneo ni Kigongo-Busisi. Kwakweli Bunge la Ndugai litajibu haya mbele za Mungu!

View attachment 1570153
Nawaza tu bilioni 700 Tshs ambazo ni hela nyingi sana yani hata Richmond haioni nusu yake. Kama zingetumika kwa mtu kuona mbali. Kuliko kujenga hilo daraja litakalopitisha Hiace na mbaya zaidi kama tozo zitakuwa kubwa maana hili eneo lina watu wa kipato cha chini sana basi wakaamua kuachana na kulitumia wakaendelea na usafiri wao wa feri.

Embu tuangalie kama tungewaza vyema kwa hii bilioni 700
1. Tungechukua tu hapo kidogo tukawanunulia feri za kisasa.
2. Tukatumia hapo fedha nyingine kuboresha maisha ya watu wa eneo hilo kama kuwapa mikopo yenye riba nafuu kisha mzunguko wao wa hela ukawa mkubwa. Yani kiufupi tungefanya mambo mengine mengi sana na hii hela! Ila kwa kuzitumia kwenye huu mradi ni HAPANA!

Yani Magufuli alifanya tu ziara hapo akakumbuka kuwa alikuwa anachunga ng'ombe eneo hilo basi hapo hapo akaamua lijengwe daraja na tena akatamka kuwa wajenge chap chap maana kama atakuja Rais mwingine ataufuta huo mradi! Kumbe hata yeye akilini mwake anajua kuwa ni mradi wa hovyo kupindukia!

Naumia maana gharama za mradi huu unazidi ule wa Kigamboni ambao walau ulikuwa na maana ingawa nao ulishavurugwa vurugwa na kweli fedha zinatumika isivyo kabisa!
Bwana G, wewe ni mkazi wa maeneo ya ukanda huo linapojengwa? Tuanzie hapo.. kama sivyo, basi fanya utafiti kidogo tu utajua hujui ulichoandika..

Hoja ya gharama na mapendekezo yako, hayana mashiko..hebu focus kidogo baada ya kutafiti, utapongeza kinachofanyika. Maana ni namna bora ya kuboresha maisha ya wananzengo husika na wa Tz.

Ila hii ni kama unataka kujua..ila kama ni wale walioambukizwa UGONJWA, hautadadisi.
 
Back
Top Bottom