Bado ni kitendawili waliofaidi mabilioni ya Justine Kasusura

Bado ni kitendawili waliofaidi mabilioni ya Justine Kasusura

Alifanya hivyo lkn nakumbuka waliomuangusha ni ndugu wa karibu.

Nakumbuka alipokwapua ule mzigo alikwenda nyumbani kwa kaka yake fulani kisha kumkabidhi mzigo wote wa USD 2m kisha yeye kubaki na kiasi fulani cha Tshs na kutokomea zake. Tatizo lilikuwa kwa upande wa mke wa Kaka yake. Kaka yake alikuwa ni miongoni mwa waliokamatwa kusaidia Polisi hivyo mzigo wote ulikuwa mikononi mwa mke wake (mke wa Kaka yake Kasusura).

Yule mama alikuwa mwenyeji wa Arusha, hivyo alikimbilia huko na ule mzigo pamoja na ndugu zake wengine. Wakati huo Arusha kulikuwa na hoteli maarufu ya kitalii ijulikanayo kama Impala. Ule mzigo ulikuwa ukibadilishiwa pale in terms of Tshs.

Walinunua gari fulani minibus [emoji604]. Kazi kubwa ya gari lile ni kuwajaza marafiki zao na kwenda kula BATA. Hapo mkumbuke kuwa Kasusura katokomea gizani huku Kaka yake kawekwa korokoroni. Mama alikuwa huru na Michepuko pamoja na baadhi ya maafisa usalama waliokuwa wameahidi kumsaidia mumewe aweze kutoka korokoroni.

Nakumbuka Yule mama alikuwa na wadogo zake wawili, wa kike na wa kiume wote waliokuwa kwenye ndoa lkn wote waliwatelekeza wenza wao kwasababu ya ulimbukeni wa mpunga mrefu.

Fedha zile hazikuwa tofauti na maji ya mvua yasababishayo mafuriko Jijini. Jua likiwaka kwa saa kadhaa hukauka. Fedha nazo zilikata paap. Walichoka mbaya kisha kuuza lile gari na kurudi Jijini.

Ninachotaka kusema ni kwamba Kasusura aliangushwa na Shemeji yake yaani mke wa kaka yake.
Kama ni kweli basi Mimi naona yeye Mwenyewe Kasusura hakua na plan endelevu juu ya huo wizi wake, kabla hujafanya tukio unapaswa ujue kila kitu ikiwemo wapi utahifadhi hizo pesa na wapi wewe utaenda kuishi ukisubiri vurugu ziishe, hata kukamatwa kwake alikamatwa kirahisi sana japo tusihukumu polisi wetu nao wapo vizuri.
 
Kibunda kikubwa alimpa mzee mmoja wa Kichaga wa pale maeneo ya Airport amtunzie, yeye akitafuta chaka la kujificha, baada kustukiwa ilikuwa kazi ya kuwahonga ma RPC wa mikoa tofauti alikopita wamlinde! Kile kibunda alichokuwa nacho kilipoanza kuisha,kila akikamatwa anapiga simu kwa Yule mzee wa kichaga anatuma,mwishowe yule mzee akaona huu ufala, akamchana amwambia kibunda kimeisha hapo ndipo akakamatwa!..Ma RPC wengi wamekula hiyo hela Wakiongozwa na Kamanda Zombe mmoja waliokula kibunda cha maana...
 
Ni nani aliyefaidi mabilioni yaliyodaiwa kuporwa na Kasusura? Si Kasusura wala Jeshi la Polisi wameweza kujibu swali hili miaka 20 tangu tukio hilo litokee.[emoji848][emoji2827][emoji16][emoji40]
Yule hela anazo bhana alikua anadokoa kidogo kidogo baada ya kutoka jela, hawezi kuplan tukio kubwa kama lile halafu pesa zipotee kizembe zembe tu, lazima kuna sehemu alizichimbia tu
 
Hichi ndiyo hua nawaambia washkaji zangu kwamba 100M ni nyingi ila iwe ya halali ikifikia ikiwa ni 100M ila inabidi ujifiche utaiona si chochote.

Nafikiri mwaka juzi kuna walinzi watatu kama niko sahihi waliiba zaidi ya 200M ila wakakamatwa Mbeya wakiwa wamenunua bodaboda, flat screen ya Sundar. Na nyingine ikakutwa.

.

[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Si bora wangenunua hata flat screen ya LG na IST.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii heading ni majanga ila haijastukiwa na wale wana bado [emoji23]
Screenshots_2023-05-09-07-55-50.jpg
 
Mtu kama huyu Kasurura ni kwamba hakuwa smart, sema dodo lilimdondokea akashindwa kucheza kama pele....

Waafrika wengi weusi hatujui kucheza na pesa vilivyo hasa tunapo piga tukio, wazungu, waarabu, wachina na hawa wasomali hapa afrika akiotea dodo ni ngumu sana kumkamata though wanaintelejensia wao wapo vizuri sana kwenye kuwasachi.

Tukio umepiga miezi kadhaa unaenda guest bubu na kimwana asee hii ni hollshit alafu unaenda lewa na kurudi chakariii, haya ndiyo yale ya Hushpupy yaani he caughted red handed na pesa kibao.

Pesa kwa mtu mweusi haijifichi kabisa showoff na blabla kibao..... bilioni 4.4 za mwaka 2001 yaani nimefanikiwa kutokomea niambia ndugu yangu mwaminifu anichimbie Andaki langu kabisa 😁

Ikishindikana kuchimbiwa Andaki najibadilisha mwonekano wote kabisa, yaani napita hapo JNIA na mkinijua lazima mtoke jasho.
Kama i was Christian i must be a muslim......change the full identities....ndevu za bandia, kama ni mweusi najikoboa kuwa white, milioni $2 si mchezo.
Ikiwezekana, unajibadilisha na jinsia kabisa,,chezea pesaaa ww😂😂😂😂😂
 
Na unajua kwanini Citibank waligoma kwenda mahakamani kutoa ushahidi?

Wao walipaswa kuwa washitakiwa no 1 kwakuwa walivunja utaratibu wa kuhamisha pesa (IMT) International Money transfer act

Hizo pesa zilipaswa kuhamishwa kupitia BOT ama kwa kibali maalum cha serikali kupitia BOT lakini Citibank wakafanya uhuni kwa nia ya kukwepa tozo, kodi na kamisheni za serikali
Jela kuna kila aina ya ujuzi na elimu.. Kasusura baada ya kulijua hili alishikilia hapo hapo
Una maana gn kuwa hela kuna kila aina ya ujuzi? Kuna watu wanaotoa elimu?
 
Back
Top Bottom