Bado sijaelewa jambo moja: Hivi tunataka kuendesha SGR sambamba na reli ya zamani?

Hapa wameamua kuepusha shari tu baada ya watu kupiga kelele sana kwamba kwann serikali imenunua mwbehewa mitumba halafu siyo mchongoko. Wakaamua yaende reli ya zamani.

Lkn kusudio halikuwa hilo, ukifuatilia hotuba ya rais Samia kabla, maelezo ya Kadogosa kabla na ufafanuzi wa Gerson msigwa baada ya kelele za wananchi.

. Ukiwasikiliza wote hawa hawaongelei kabisa reli ya zamani.
Hata mie ndivyo nilivyoelewa mwanzoni; SGR ingeanza na mabehewa ya zamani, kulingana na Samia. Lakini sasa naona mabehewa ya zamani ni ya reli ya zamani, kitu ambacho naona ni kama jambo jipya

Something is not adding up na hakuna aliye jasiri kusema ukweli
 
Kuna kila dalili kwamba SGR itakapokamilika bado tutakuwa na reli ya zamani ikitoa huduma. Hapo mwanzo nilifikiri kwamba reli ya zamani itaendelea kutoa huduma kwa matawi ya Tabora - Mpanda, na labda Dar -es Salaam kwenda Tanga, Moshi na Arusha, ambako sijasikia lolote juu ya kuwepo kwa SGR.

Lakini kila habari zinapotolewa, sisikii hili likiwekwa wazi. Ninasikia tu kuhusu SGR sambamba na reli ya zamani, na manunuzi yakifanywa kwa ajili ya reli zote mbili.

Kwa nini tuendelee kuhudumia na kuwekeza kwenye reli zote mbili? Ni kupanua wigo wa huduma katika bei, kwamba SGR iwe kwa mabwana na reli ya zamani watwana?

Ninachelea kwamba uwepo wa SGR utafanya reli ya zamani iendeshwe kwa hasara iwapo tutaendelea kuitumia. Nilidhani labda SGR ikikamilika reli ya zamani itauzwa kama vyuma chakavu.

Labda ni ule uswahili wetu tu wa kiafrika, tunaendelea kutaka kumiliki vitu vya zamani, tunashindwa kuvitupa hata kama tumenunua kitu kipya mbadala
Sisi ambao hatujasoma Cuba wala Minaki na tumezaliwa miaka ya 1990 hatujui kitu
 
Binafsi naona ni tija kuoperate reli zote sambamba. Reli iliyopo ni nzima inafanya kazi, ni cheaper kuoperate na inaongeza transit capacity, itaendelea kuissupport SGR mpaka iwe fully operational, inaweka uingiliano/compatibility na reli zingine mf TAZARA pia ni backup ikitokea tatizo kwenye SGR. Sababu zipo nyingi kuendelea kuwa nayo.
 
Mmezoea cheweing gum nyie, wenzenu wa zamani walizoea matobolwa - waulize watu wa Tabora watakuambia utamu wa matobolwa kulinganisha na hizo cheweing gum zenu!
 
Hata mie ndivyo nilivyoelewa mwanzoni; SGR ingeanza na mabehewa ya zamani, kulingana na Samia. Lakini sasa naona mabehewa ya zamani ni ya reli ya zamani, kitu ambacho naona ni kama jambo jipya

Something is not adding up na hakuna aliye jasiri kusema ukweli
Mkuu hebu anzisha uzi juu ya Jambo hili tuone wadau watatoa maoni gani.
 
Binafsi naona ni tija kuoperate reli zote sambamba. Reli iliyopo ni nzima inafanya kazi, ni cheaper kuoperate na inaongeza transit capacity, itaendelea kuissupport SGR mpaka iwe fully operational, inaweka uingiliano/compatibility na reli zingine mf TAZARA pia ni backup ikitokea tatizo kwenye SGR. Sababu zipo nyingi kuendelea kuwa nayo.
Sasa kama reli iliyopo ni nzima inafanya kazi, ni cheaper ku-operate, kwa nini tukaamua kujenga SGR kwa mabilioni ya fedha badala ya kuimarisha hiyo iliyo nzima?
 
Ina maana mama Samia anafanya maamuzi bila kuwashirikisha? Nilipata hisia kwamba hata uongozi wa TRC haukujua kama mabehewa yaliyokuwa yanapokelewa ni mapya au mitumba, ya reli ya zamani au SGR.

Kwa nini wanajikanyaga kueleza na kufafanua vitu vidogo sana hadi Samia atoe ufafanuzi?

Wanatetea matumbo yao na familia zao mkuu, ukienda kinyume na matakwa ya wakubwa unanyooshewa mlango wa kutokea.
 
Sidhani kama nitawalaumu kwa hilo. Hata mie ningefanya hivyo hivyo katika positions zao. Hiyo ndio reality.
 
Kimsingi, sheria ya serikali ya manunuzi hairuhusu kununua kitu cha serikali ambacho ni used

Kwa maana hyo kama na mkuu amebariki hayo manunuzi ya vichwa na mabehewa yaliyokwisha kutumika (used).

Kama Katiba yetu ingekuwa imenyooka na kufwatwa kama mwongozo wa nchi ingepaswa wahusika waachie Ofisi.
 
Si mmelalamika nauli kubwa, tunaacha na hii ya zamani kwa wanaoona nauli ya sgr kubwa.
 
Sasa kama reli iliyopo ni nzima inafanya kazi, ni cheaper ku-operate, kwa nini tukaamua kujenga SGR kwa mambilioni ya fedha badala ya kuimarisha hiyo iliyo nzima?
Tungeweza kuchagua gauge ya upana wowote tunaotaka kma tunaweza kuzalisha, kuhudumia na kumaintain kila kitu wenyewe, mfano Japan wana gauge yao nadhani. Kwetu sisi hii ni imported standard tumechukua kwa kuangalia standard za waliotutangulia. Nna maswali kma wewe na sio mtaalamu wa hii sector lakini nadhani uamuzi wa kuwa na SGR ina support technology mpya mpya nyingi za reli za kisasa, ina uwezo wa kubeba mzigo zaidi na kubwa kabisa ni speed/efficiency. Kuboresha/kuimarisha iliyopo ina limitations.
 
Kwa maana hyo kama na mkuu amebariki hayo manunuzi ya vichwa na mabehewa yaliyokwisha kutumika (used).

Kama Katiba yetu ingekuwa imenyooka na kufwatwa kama mwongozo wa nchi ingepaswa wahusika waachie Ofisi.
Inabidi uwe na akili za mwenda wazimu kudhani kwamba kuna kiongozi yeyote wa Tanzania ataongoza nchi bila kukiuka katiba ya Tanzania; si Mwinyi, si Mkapa, si Kiwete, Si Magufuli, si Samia si yule atakaekuja
 
Kimsingi, sheria ya serikali ya manunuzi hairuhusu kununua kitu cha serikali ambacho ni used
sasa

Sasa Mkuu haya Mabehewa na Vichwa vya Treni si wamekubali wenyewe kwamba ni Used? ama hivi havikununuliwa walipewa?
 
Back
Top Bottom