Nchi mpaka huu mfumo wa kijani
Ukitoka labda mambo yanaweza kaa
Sawa
Ova
Najua ndivyo wengi wanafikiri, lakini amini nakuambia, usidhani ukiwaleta Chadema au ACT sijui basi hiyo ndio dawa ya maendeleo. Binadamu ni wale wale, wawe CCM, Chadema au ACT hata TLP. Niambie ni nchi gani duniani imepiga hata kubwa ya maendeleo kwa kuwa tu walibadilisha chama tawala. Zambia? Kenya? USA? Uingereza? Brazil? Malawi?
NI kawaida kudhani mchezaji alie benchi atafanya vizuri zaidi, lakini huwezi hata siku moja kuwa na huo uhakika. Inaweza itokee, inaweza isitokee.
Ndio maana siku zote nimesema, siri ya kuifanya angalau Tanznia iendelee, sio lazima Chadema wachukue nchi, bali ni kufanya vyama vya upinzani viwe na wabunge wengi kwa pamoja, ikiwezekana kuliko hata idadi ya wabunge wa CCM
Mie nilisema raisi atakaekuja kuwa mzalendo wa kweli wa Tanzania mwenye kuitakia maendeleo Tanzania ni yule atakaeimarisha upinzani nchini, sio anaeimarisha Chama chake dhidi ya upinzani. Na kwa hili nawakosoa wote waliokuwa maraisi tangu mfumo wa vyama vingi uanze - Mwinyi, Mkapa, Kikwete, Magufuli na hata Samia. Wote wameiangusha sana nchi hii na hakuna mzalendo wa kweli kati yao. Porojo tu zimewajaa lakini sio wazalendo hawa wote, wapigania tonge kwa sababu ni wapigania vyama vyao badala ya nchi yao.
Kama Samia angenisikiliza, ningemwambia kama kweli una uchungu na hii nchi, wapaishe wapinzani, wafanye wawe popular na kuheshimika nchini, wafanye waogopwe na chama chako mara mia zaidi ya ilivyo sasa. Mwinyi kule Zanzibar ana idea kidogo, lakini bado yuko very mediocre