Na kwa kweli sijui kama utapata jibu kutoka kwa wahusika kueleza haya uliyoweka hapa.Kuna kila dalili kwamba SGR itakapokamilika bado tutakuwa na reli ya zamani ikitoa huduma. Hapo mwanzo nilifikiri kwamba reli ya zamani itaendelea kutoa huduma kwa matawi ya Tabora - Mpanda, na labda Dar -es Salaam kwenda Tanga, Moshi na Arusha, ambako sijasikia lolote juu ya kuwepo kwa SGR.
Lakini kila habari zinapotolewa, sisikii hili likiwekwa wazi. Ninasikia tu kuhusu SGR sambamba na reli ya zamani, na manunuzi yakifanywa kwa ajili ya reli zote mbili.
Kwa nini tuendelee kuhudumia na kuwekeza kwenye reli zote mbili? Ni kupanua wigo wa huduma katika bei, kwamba SGR iwe kwa mabwana na reli ya zamani watwana?
Ninachelea kwamba uwepo wa SGR utafanya reli ya zamani iendeshwe kwa hasara iwapo tutaendelea kuitumia. Nilidhani labda SGR ikikamilika reli ya zamani itauzwa kama vyuma chakavu.
Labda ni ule uswahili wetu tu wa kiafrika, tunaendelea kutaka kumiliki vitu vya zamani, tunashindwa kuvitupa hata kama tumenunua kitu kipya mbadala
Kama kutakuwepo na ushindani kati ya hizi reli mbili kuendeshwa kwa pamoja, maana yake ni kwamba hapatakuwepo na ufanisi katika zote mbili, kwa sababu hakuna pato litakaloweza kupatikana kufanikisha uendeshaji wa zote mbili kwa pamoja.
Na kama ulivyoelezea vizuri kabisa, juhudi za kuimarisha 'meter gauge' zingehamishiwa kwenye hayo maeneo ambako bado hapajawa na mipango ya kujenga SGR, ili reli hiyo ifanye kazi vizuri zaidi katika maeneo hayo.
Haya tunayoyaona sasa hivi ni kama kuchanganyikiwa, na kutotoa uamzi wa moja kwa moja kifanyike kitu gani. Kuchanganyikiwa huku kunachagizwa na wafadhiri toka nje, kama WB wanaoendelea kutoa vipesa mjinga kwa hiyo reli ya zamani. Hapa wahusika bado wana mirija yao, na hawataki kuiachia wakati pesa hiyo bado inatiririka.