Bado sijaelewa jambo moja: Hivi tunataka kuendesha SGR sambamba na reli ya zamani?

Kama ulishindwa kuelewa utofauti wa yale mabehewa hata kabla hawajatoa maelezo yao basi we jihesabu sio fala tu bali ni bonge la fala..[emoji6], huo ndo ukweli mchungu unless otherwise uwe unachangamsha genge tu.
Acha uchawa labda akili zitakurudi kidogo
 
Sure. Ndio maana kwa reli ya kaskazini nimezungumzia malori yanayorundikana namanga kupeleka mizigo uganda, south sudan nk.

Hilo la ku clear mizigo nchi kavu inabidi tujifunze kenya maana walitaka mizigo ya uganda, DRC, South Sudan, Rwanda, etc iwe cleared nje ya mombasa sababu lengo kubwa la kujenga SGR yao lilikuwa kuhudumia mzigo wa mombasa. Inaonekana Uhuru alikwama kwa hili baada ya migomo, maandamano ya cargo operators, etc

Sijafuatilia Ruto kama kafanikiwa maana wanasiasa walijiunga kuwaunga mkono cargo operators....

Ila kama ulivyosema huduma ya abiria huwa inakuwa subsidized, huku huduma ya cargo ikitegemewa kuingiza faida...
 
SGR kufika Kigoma itachukua miaka kadhaa ijayo, kwa muda huo MGR italazimika kutumika sambamba.
Pia miundombinu na vifaa vya zamani havitatupwa, vitatumika hadi vichakae, visifae kwa matumizi tena.
 
Hapana bana zote zinaweza kutumika kwa ajili ya usafirishaji. Nilipokuwa china wanazo zote hizo na kila mtu anaenda kupanda kutokana na mahitaji yake. Na wao wameenda zao za kwao ni two way.
 
Sure. Ndio maana kwa reli ya kaskazini nimezungumzia malori yanayorundikana namanga kupeleka mizigo uganda, south sudan nk.
Haya malori yanayokwama Namanga yanakuwa yametoa wapi huo mzigo? Dar es salaam? Hivi ni economical kutoa mzigo Dar kupeleka South Sudan au hata Uganda?
 
Kama ulishindwa kuelewa utofauti wa yale mabehewa hata kabla hawajatoa maelezo yao basi we jihesabu sio fala tu bali ni bonge la fala..[emoji6], huo ndo ukweli mchungu unless otherwise uwe unachangamsha genge tu.
Yaani wewe kwa kuyaangalia tu ukatambua haya sio mapya? Hujitambui wewe. Unashindwa kutofautisha kati ya upya na design.

Nikuulize swali kuona kama una akili za kufikiri. Leo hii 2022, nikuuzia gari Land Cruiser V8 model ya 2010 ambayo haijawahi kuendeshwa toka itengenezwe imekuwa show room, ni mpya au sio mpya?
 
Haya malori yanayokwama Namanga yanakuwa yametoa wapi huo mzigo? Dar es salaam? Hivi ni economical kutoa mzigo Dar kupeleka South Sudan au hata Uganda?
Malori yanatoka dar through namanga kwenda nje ya nchi. Ndio yanayoharibu barabara ya kaskazini. Ukienda namanga utaona.
Na utatuzi wake ni SGR Dar to namanga
 
India ni moja ya mataifa yenye mtandao mrefu zaidi wa reli duniani ikiwa na jumla ya km 65000, katika mtandao huo mrefu kuna track gauge za upana tofauti, zipo Broad gauge, Narrow gauge, Standard gauge na Meter Gauge. Reli zote hizi zinafanya kazi hazijatelekezwa, baadhi ya maeneo yaliyokuwa na meter gauge imebadilishwa kuwa Broad gauge.
USA ndiyo taifa lenye mtandao mrefu zaidi duniani ikiwa na jumla ya km 250,000 katika mtandao huo zipo reli za guage tofauti ikiwemo Wide gauge, Broad gauge nk
Hata wakoloni wetu Waingereza nao wana reli za upana tofauti na zote zinafanya kazi.
Ikiwa hao wakubwa walijenga reli mpya au kubadilisha baadhi na hawakuua za zamani sisi ni nani tutelekeze ya zamani?
Mleta mada unaweza tueleza madhara ya kuwa reli zenye upana tofauti?
Kwa Tanzania kuendelea na matumizi ya meter gauge kuna faida kubwa sana, yapo maeneo muhimu ambayo bado hayajafikiwa na SGR, mfano Tanga, Moshi, Arusha, Mpanda, Singida nk. huko kote kuna reli ya MGR lakini hakuna reli SGR.
Bandari ya Tanga ni moja ya bandari zenye kupokea mzigo mkubwa, kuna tatizo gani ikiendelea kuhudumiwa na MGR?
Hivi karibuni ilijengwa bandari ya Kalema iliyopo mkoa wa Katavi, hii ni bandari ya kimkakati inayotarajiwa kuhudumia jirani zetu hasa Congo kusini, tunajua kwamba Katavi haijafikiwa na mradi huu wa SGR, je bado tu hamuoni umuhimu wa kuendeleza reli ya mkoloni?
Kitu ambacho ningeshauri Serikali yetu ifanye ni kukaribisha wawekezaji binafsi kati usafirishaji wa reli ili kuleta ushindani kwa TRC, hii ndiyo njia pekee itakayo saidia kutoa huduma nzuri kwa wateja, mashirika mengi ya umma yameonyesha ufanisi duni, hata mataifa makubwa kama USA yana makampuni binafsi yanayofanya kazi kwenye mtandao wao wa reli.
Miundombinu ya reli ibaki kuwa mali ya serikali, yakaribishwe makampuni binafsi kufanya biashara ya usafirishaji relini na serikali ichukue tozo kwao, huku ikijikongoja na TRC yake, kwa kufanya hivyo tutashuhudia tofauti kubwa ya huduma kama ilivyo sasa kwenye mawasiano ya simu, TTCL vs Binafsi, ili nia njema ya Serikali ya kukuza sekta ya usafiri wa reli ifanikiwe hakuna namna nyingine zaidi ya kukaribisha sekta binafsi
 
Mtu ametokea kwenye masijala huko na kutoa huduma za chai maofisni leo hii ndo raisi unategemea performance gani labda utokee miijiza
Aisee,hii kali.Lakini hii ni kweli au umedondosha comment hii kihasira hasira tu.Fafanua mkuu, because this is a very serious allegation kwa kiongozi was nchi.
 
Nakuomba tuelewane hapo shida sio kutupa cha zamani mkuu, shida ni jinsi ya uendeshaji wa hizo reli hapo ndipo patakuwa kichaka cha wapigaji kama bandarini tu, hiyo bandari unayo isema ni ya kimkakati itabakia kwenye makalabrasha tu amini nachokiandika, hatuna mipango ya mda mrefu wala usafi wa dhamana ya Nchi.
 
Unamlaumuje aliyekuta mradi uko kwenye ujenzi? Walioanzisha mradi walitakiwa waweke master plan in place onset.
Unataka kusema kwamba wameshindwa kuendeleza mradi kwa sababu wamekosa master plan?hii sababu haina mashiko kabisa
 
Hili ndio jibu sahihi.
Wamejihami baada ya kuona wananchi wameanza kuhoji.
 
Unadhani tukitelekeza reli ya zamani na kubaki na mpya ndio tutakuwa tumekata chaka la wapigaji?
 
Unamlaumuje aliyekuta mradi uko kwenye ujenzi? Walioanzisha mradi walitakiwa waweke master plan in place onset.
Mama kaukuta mradi wa SGR? Si alikua VP awamu ya DK JPM.
Mkurugenzi wa TRC si ni huyo huyo hajabadilishwa.
 
Samahani naomba kuuliza,

SGR inafika Tabora na Kigoma?

Maana taarifa nilizosikia inaishia Dodoma na hapo Dodoma kwenyewe imefika sababu ndo makao makuu ya nchi lakini ilitakiwa iishie Morogoro (sijui kama haya ni sahihi)

SGR si ndo TERENI YA UMEME eeh? Ikifika kigoma nitaenda kutembea kuna ndugu zangu huko
 
Hela ya kununua mapya' unayo!?
Hela huwa haikosekani ila tatizo huwa vipaumbele vya wale wazee wa 10% kama hawapati kitu huwa mazonge ni kawaida.

Magufuli alinyoosha kila kitu, by the time wanakabidhi reli hayo mabehewa yangekuwa yashafika tena yale ambayo tulikubaliana. Ila kwa kuwa kuna uhuni ulifanyika tender ikahamishiwa kwa behewa used za bei rahisi basi mpunga ukaliwa akasingiziwa kuwa yule mshika tender wa kwanza hatayafikisha kwa wakati so wamempa mwengine hio ndio tatizo.
 
Aliyekuambia alikudanganya, SGR itafika Tabora, Mwanza na Kigoma. Kipande cha Dodoma kwenda Tabora ujenzi unaendelea, Tabora kwenda Kigoma mkataba wa ujenzi umesainiwa juzi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…