Bado sijaona kama kuna sababu za nje ya uwanja zinazosababisha Simba kukosa matokeo, tuache kukuza mambo

Bado sijaona kama kuna sababu za nje ya uwanja zinazosababisha Simba kukosa matokeo, tuache kukuza mambo

May Day

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2018
Posts
6,311
Reaction score
9,027
Mimi huwa nafuatilia pia Mechi za Yanga, kiukweli sijaona tofauti kubwa sana ya kiuchezaji au kiupambanaji.

Tofauti pekee ni kuwa Yanga wanafanya juu chini wapate walau Goli moja na kuhakikisha hawaruhusu goli...ukitoa ile mechi yao na Namungo ambapo ilibidi Refa ajiongeze lakini Wazee Wenzetu nao walikuwa wameshikwa pabaya na walikuwa wanapoteza.

Mechi karibia zote Yanga wana strugle kama Simba tu, Vijana wote wanaokutana nao wanawatoa jasho kama tu inavyotokea kwa Simba, hata Mechi ya leo tumeona Mbao walivyodinda utasema Yanga wanacheza na Azam au Namungo.

Mechi ya Kagera Simba wamecheza kwa bidii na waliwazidi Kagera pakubwa lakini changamoto ikawa ni hiyo tu ya kutokufunga bao...nafasi zilipatikana kukakosekana umaliziaji, tuliona Muzamiru aliukosa mpira aliohitaji kugusa tu mpira uingie golini...attempt ya Onyango kwa bahati mbaya aliushika mpira.

Yanga wakipata penati kimbilio lao ni Saydoo, na kwa bahati nzuri hajakosa, hata Simba wangezitumia penati zao vizuri wasingekuwa hapa walipo sasa.

Sasa sijui hawa wanaosema au kudhani kuna sababu za nje ya Uwanja wanayatoa wapi hayo...sana sana ni kuhimizana njia za mkato ambazo ni ujinga tu, Watu wanatakiwa wapambane uwanjani.

Simba bado wana nafasi ya kurudi kwenye traki na wasiruhusu Watu wa nje kuingiza ujuaji wao...ila kama watataka kubadilisha Kocha hapo mimi sina kipingamizi lakini Wachezaji ni Wazuri na wana nafasi wa kuipa Simba ushindi hata kama haitafanikiwa kutetea ubingwa kwa msimu huu lakini walau basi Vikombe vyote vitakavyokatiza mbele waruke navyo.
 
Mimi huwa nafuatilia pia Mechi za Yanga, kiukweli sijaona tofauti kubwa sana ya kiuchezaji au kiupambanaji.

Tofauti pekee ni kuwa Yanga wanafanya juu chini wapate walau Goli moja na kuhakikisha hawaruhusu goli...ukitoa ile mechi yao na Namungo ambapo ilibidi Refa ajiongeze lakini Wazee Wenzetu nao walikuwa wameshikwa pabaya na walikuwa wanapoteza...
Tuliza mshono wewe... huu ushauri ingeutoa muda mrefu tungekuelewa japo kidogo.. Leo wazee wa simba yao wamekaa kwa sabbu walishaona tatizo kwenye timu yao.. ndo maana wakaamua kukutana.. imewafikirisha sana haiwezekani penati 7 ukambulia 2, on target 5 hadi 10 kwa match usipate goli, ball position 68 above kila match then umafungwa au unadraw, wachezaji wazuri kuliko timu yoyote tz then wanasuasua hawajui wafanye nini,

kocha mwenye CV kubwa kuliko yoyote NBC premier league lkn anakosa mafanikio halaf wanoko wanasema kocha wa mnchongo, na mengine meeengi..na huku unaona kabisa match za kimataifa ambazo simba amekuwa akiibeba nchi zimekaribi........ko leo wenye simba yao wamekaa wamejadili wamefikia muafaka wamejipanga jinsi ya kuisimamia timu yao...
 
Tuliza mshono wewe... huu ushauri ingeutoa muda mrefu tungekuelewa japo kidogo.. Leo wazee wa simba yao wamekaa kwa sabbu walishaona tatizo kwenye timu yao.. ndo maana wakaamua kukutana...
Hao Wazee wanafanya nini ni kuleta migogoro tu isiyo na maana.

Mpira ni uwanjani na hakuna cha ajabu kilichotokea mpaka sasa.

Mmeshasahau kwamba mmechukua kombe la Mapinduzi na Yanga wamelikosa?. hao Wazee ndio waliwezesha hilo?.
 
Hao Wazee wanafanya nini ni kuleta migogoro tu isiyo na maana.

Mpira ni uwanjani na hakuna cha ajabu kilichotokea mpaka sasa.

Mmeshasahau kwamba mmechukua kombe la Mapinduzi na Yanga wamelikosa?. hao Wazee ndio waliwezesha hilo?.
Kawaulize timu yako ya utopolo kwa nini match zao zoote wanaingilia mlango wa nyuma ikiwezekana wanavunja kabisa ukuta na wako tayari kulipa faini tff ili mradi tu wasitumie geti kubwa? ukipata jibu nitag...
 
Kwa mtazamo wangu naweza kusema tatizo linaanzia kwa kocha. Hii inatokana na namna timu kwa ujumla inavocheza. Kipindi cha nyuma kabla ya ujio wa kocha Pablo timu ilikua na muunganiko mzuri kati ya mabeki na viungo hali ya maelewano kwa timu nzima ilikua vizuri kufikia hatua kwamba unaweza ukampanga forward yeyote mbele na akatupia magoli ya kutosha mfano mzuri ni msimu ulioisha Chriss Mugalu, Meddie Kagele pamoja na John Bocco walikua na idadi kubwa ya magoli.

Ujio wa kocha pablo ulipaswa kuonesha mabadiliko hasa sehemu ya midfield kwa kuwepo uelewano mzuri baina yao na washambuliaji lakini pia na mabeki kitu ambacho kwa sasa inaonekana pablo ameshindwa kuimarisha safu ya kiungo.

Wakati Mugalu majeruhi Meddie Kagele na John Bocco hawakuweza kufunga idadi nzuri ya magoli hivyo tumaini pekee lilibaki kwa Mugalu lakini pamoja na mugalu kupata nafasi bado hali imeendelea kua ileile. Hii inaleta taswila kwamba kocha hajatambua plani zinazoweza kumpatia matokeo katika hali yoyote ile.

Mara kadhaa ameonekana kumuamini mkude pamoja na mzamiru na mara nyingine amekua akimuamini zaidi kanoute ila bado hawajaweza kuleta uwiano mzuri katika safu ya viungo.

Binafsi ninaweza kusem pamoja na kwamba kuna makosa baadhi yanayotokana na wachezaji lakini lawama zaidi ziende kwa kocha kwani yeye ndie mwenye jukumu la kuhakikisha wachezaji wanakua katika viwango bora ikiwa ni matokeo ya mbinu pamoja na mipango ya kocha hivyo pablo ajitathimi.
 
Kwa mtazamo wangu naweza kusema tatizo linaanzia kwa kocha. Hii inatokana na namna timu kwa ujumla inavocheza. Kipindi cha nyuma kabla ya ujio wa kocha Pablo timu ilikua na muunganiko mzuri kati ya mabeki na viungo hali ya maelewano kwa timu nzima ilikua vizuri kufikia hatua kwamba unaweza ukampanga...
Unajua kila mtu anatoa maoni yake kufuatana na mtazamo wake na ndo maana hadi sasa hakuna anayejua tatizo hasa la kudrop kwa simba ni lipi?

Ili msiendelee kupata shida nawashauri mtulie simba hii inarudi kwa kasi ya ajabu. Vitu vodogodogo vilivyokuwa vinasumbua vimerekebishwa.. ko tulieni huku mkijua ustaarabu wa mpira wa kitanzania unaanzia msimbaz......mambo mazuri yanakuja
 
Tatizo ni Manara, nasema tatizo ni Manara. Hamasa hakuna na mikakati imepwaya.
Toka Manara aondoke Simba, Simba imepwaya ndani ya uwanja na nje ya uwanja. Na toka Manara ahamieYanga, hamasa ya Yanga iko juu.
 
Tatizo walilonalo Simba ni la kisayansi na ni ngumu kwao kutoboa Kama hawajalitambua tatizo, Ata wafanye vikao kila wiki.

kwakua ki sayansi uharibifu uliopo ni mkubwa wataendelea kuteseka na wasipo angalia watatiana bakora.

Mimi nafurahi kwakua kwa kukosa kwao utulivu wa kutafakari Mambo wataendelea kuteseka. Msimu huu Kisayansi ni ngumu Simba kushika nafasi mbili zajuu na wakijitahidi Sana labda ya tatu au nne.
 
Kwa mtazamo wangu naweza kusema tatizo linaanzia kwa kocha. Hii inatokana na namna timu kwa ujumla inavocheza. Kipindi cha nyuma kabla ya ujio wa kocha Pablo timu ilikua na muunganiko mzuri kati ...
Mkuu msitafute mchawi, wachezaji wa simba wamechoka, umri umeenda ule mnyumbuliko haupo tena. Humuoni Chama anavolazimisha tu mwili, ila kiukweli siyo yule Chama wa awali
 
Ilikuwa Kosa kubwa Sana kumfukuza Da Rosa kwa ajali ndogo tu ya kutolewa Champion.

Hii inanikumbusha Yanga walivyomtimua Kaze wakati ilikuwa dhahiri Kuna kitu hakikuwa sawa huko kwenye uongozi na si benchi la Ufundi
 
Kawaulize timu yako ya utopolo kwa nini match zao zoote wanaingilia mlango wa nyuma ikiwezekana wanavunja kabisa ukuta na wako tayari kulipa faini tff ili mradi tu wasitumie geti kubwa? ukipata jibu nitag...
Mkuu mimi nilianza kuishabikia Simba tangu nikiwa dogo shule ya msingi, enzi izo nilivutiwa na kina Sunday Juma, Zuberi Magoha, Idi Pazi, Zamoyoni Mogela, Malota Soma, Lila Shomari n.k, ....hayo majina nilikuwa nikiyasikia redioni naburudika sana, hatukuwa na TV bado kama sasa, .huenda labda hata hukuwa umezaliw....hivyo sijawahi kuwa shabiki wa Uto.

Ila miaka ya katikati hapo niliachana kushabikia Mpira wa bongo kwa sababu hizihizi za imani za kijinga nisizoziunga mkono, lakini nikarudi tena miaka ya 2010 hivi mpaka sasa.

Tucheze mpira tuache ujinga wa nje ya uwanja.
 
Unajua kila mtu anatoa maoni yake kufuatana na mtazamo wake na ndo maana hadi sasa hakuna anayejua tatizo hasa la kudrop kwa simba ni lipi?...ili msiendelee kupata shida nawashauri mtulie simba hii inarudi kwa kasi ya ajabu. Vitu vodogodogo vilivyokuwa vinasumbua vimerekebishwa.. ko tulieni huku mkijua ustaarabu wa mpira wa kitanzania unaanzia msimbaz......mambo mazuri yanakuja
Ndio maana kichwa cha habari nimesema sioni tatizo, yote yanayoendelea ni mambo ya kawaida kabisa.

Wachezaji watulize tu akili, hivi kukosa goli la wazi kuna ajabu gani haswa mpaka Watu muone ni miujiza?.

Huyo Mayele ambaye hata mimi ni Simba lakini namkubali ameshakosa Magoli ya wazi mengi tu na mengine wala usingeamini kama angekosa.
 
Mimi huwa nafuatilia pia Mechi za Yanga, kiukweli sijaona tofauti kubwa sana ya kiuchezaji au kiupambanaji.

Tofauti pekee ni kuwa Yanga wanafanya juu chini wapate walau Goli moja na kuhakikisha hawaruhusu goli...ukitoa ile mechi yao na Namungo ambapo ilibidi Refa ajiongeze lakini Wazee Wenzetu nao walikuwa wameshikwa pabaya na walikuwa wanapoteza...
Mkuu unatakiwa uamini! Yaani GSM wanatuharibia mpira wetu. Ona kila mechi wanawapa wachezaji jezi za kuwagawia mashabiki! Ona kila mechi Yanga inashinda, halafu sisi simba tunafungwa! 🥵

Yaani siyo fair hata kidogo! Halafu Moo ametulia tu! Yaani tajiri namba 17 Afrika anasumbuliwa na GSM ambaye hata kwenye 100 bora hatajwi! Ameshindwa hata kumhonga yule Afisa wa TFF ili asimshtaki Babra!!
 
Back
Top Bottom