Afrika hata ukienda zako Morogoro .ukatafuta bonde heka 5 ukapanda miwa baada ya miaka 2 sio mwenzetu unakuja kuuza Dar vijjwe vya juice, au unafungua vijiwe vya kuuza juice ya miwa.
.Unapanda minyonyo, mibono,milonge,miarobaini baada ya miezi tu unakamaua mafuta unatengeza sabuni unauza.
.Una kijiwe wilayani cha kufyatua tofauti za kuchoma unachoma kwa oil chafu watu wanajenga KILA siku Mungu akupe nini.
.Unaenda porini unaangua mibuyu kisha unatengeneza unga na mbegu unakamua mafuta unauza.
.Unalima mihogo, mtama unaweka kwenye magodown unasubiria msimu unauza unga, minadani Mungu akupe nini.
. Unanunua marobota ya mitumba Kazi yako kutembea kwenye minada unauza nguo, ukipata pesa unanunua mbuzi unaleta mjini, ukitoka mjini unachukua marobota ya mitumba unarudi nayo.
.Fungua vijiwe vya chai,kahawa,vitafunwa wilayani, vijijini,huku unawawekea tv wachek mpira bure unatoka
Fursa bado zipo tele afrika ni kuchanganywa tu ubongo,maana shida uleta akili.