Nsanzagee
JF-Expert Member
- Jun 28, 2023
- 2,209
- 4,769
Najua,
Wengi wenu badala ya kujikita kwenye hoja, mtanijadiri na tena siyo tu kunijadiri, ila ni kwa kutoa matusi!
Ni kweli hatuwezi kuwa na mtazamo sawa, na hii inakuja ili kutufanya tuonekane ni wanadamu na mambo yetu ili yawe sawa, tunahitaji kuwa na migongano ya kifikra na hatimaye kwenda sawa
Naam!
Mh makamu mwenyekiti Chadema bwana Tundu Lissu, tangu aondoke nchini kwa matibabu huko Ughaibuni, na baada ya kukaa huko kwa mda mrefu akitibiwa, alirejea nchini kwa ajili uchaguzi mkuu 2020
Hata hivyo, hakuja na familia yake, nadhani kwa kipindi hicho, haukuwa wakati sahihi wa kuuliza juu ya kwa nini kaiacha familia yake ulaya kwa sababu kuu moja kwamba, bado alikuwa kwenye matazamio ya kiafya
Mpaka hii leo, tunazungumza miaka mitano mingine inakaribia kupita tokea uchaguzi wa 2020 alipokuwa mgombea wa nafasi ya Urais kupitia chama chake, bado shida ya matazamio inaendelea?
Jambo hili halimfanyi kutokueleweka na kuaminika vizuri kwenye nyanja za kisiasa?
Kuhusu Sheria za Nchi au Katiba inasema nini kuhusu wagombea mbalimbali wa nafasi hasa ya Urais inapotokea mgombea mmoja wapo familia yake haikai nchini!
Jambo lingine la pili, Vuguvugu ambalo chadema wanaonekana kuliamsha ni la wananchi wenyewe kuingia mtaani kudai katiba, yaweza kuwa ni mbinu nzuri, Je, wananchi wanapofika mahali wajiulize, waanzishaji wa vuguvugu hili, wao ni kama wahamiaji tu nchini, likitokea la kutokea, wao wanapanda pipa na kwenda makwao ulaya, Chadema hawaoni kuwa jambo hili linawarudisha nyuma wanavuguvugu wa katiba?