Bahari mpya kuligawa bara la Afrika, Tanzania kuwa sehemu ya Kisiwa

Hamna kitu hapo , ni utafti ili watu wale pesa , Mungu hana mpango wa kufanya uumbaji wowote ashamaliza tangu Enzi na Enzi no hvyo hvyo
 
Yes.. miaka maelfu yajayo.
Lakine never underestimate the nature inaweza kutokea kwa haraka kuliko unavyo dhani tena nguvu za maji zika harakisha hicho kitu ....huo ufa ukipata nguvu ya maji kama ya lake tanganyika kwa hayo maji kuanza kufuata huo ufa basi tujue ilo tukio litafanyika kwa haraka zaidi
 
Wengi mnadhani itatokea kesho asubuhi hahaha. hii kitu inaweza kutokea baada ya miaka billion moja ijayo so kaeni kwa amani
Siyo kweli ...kumbuka kuna ziwa tanganyika kwenye huo ufa ilo ziwa ni kama busta ya kugawanyia hiyo bahari kwa haraka mara maji ya ilo ziwa yakianza kufuata huo ufa kwanguvu kuelekea baharini basi ujue itatokea hiyo bahari kwa hataka sana ...ukitumia akili kuchunguza hekima ya lilipo ilo ziwa utagundua kuna kitu kimetegwa kije kutokea kwa haraka
 
Na ndio Ziwa lenye kina kurefu Duniani which means maji yanaweza fuata huo ufa pendekezwa
 
Umeongea kweli lakini kwenye suala la muda (kutokea kwa haraka) mkuu hapo ni hapana. Plate tectonics sio kitu kinatokea overnight, it takes ages mkuu.
 
Wanajiolojia wamethibitisha kuwa bahari mpya inaundwa barani Afrika ambayo italigawa bara hilo nusu.

Inasemwa kuwa ufa wenye urefu wa maili 35 ulionekana katika jangwa la Ethiopia eneo la Afar mwaka 2005 na pengine ni mwanzo wa bahari mpya kabisa.

Ukurasa wa The Archeologist umeandika kuwa Jarida la Geophysical Research Letters linalotumia data za tetemeko na utokeaji wa nyufa linasema utengano wa bara la Afrika ulianza taratibu takribani miaka milioni 30 iliyopita.

Mataifa 54 barani Afrika yamegawanywa kulingana na wanajiolojia wanaotafiti juu ya tectonics ya sahani za bara hilo. Ufa wa Afrika Mashariki, unaotenganisha nchi za pwani ya mashariki kama Kenya na Tanzania kutoka sehemu kubwa ya bara, unapitia Msumbiji kutoka eneo la Afar kaskazini mwa Ethiopia.

Chanzo: TBC

--------------

Moja kwa Moja kwenye mada.

Wanajiolojia wanasema Bara la Afrika litagawika kutokana na Bahari Mpya inayoenda kujitokeza.

Kwa Mujibu wa Wataalamu hao Kuna ufa unaoendelea kukua na ulioandia Ethiopia unaozidi kuongezeka kadiri ya Miaka inavyokwenda na hivyo kusababisha matetemeko makubwa ambayo yatakuja kupelekea Drifting ya Bara la Afrika na kuzaa Kisiwa Kipya kikubwa kitakachotenganishwa na Bahari Mpya.

Tanzania itakuwa sehemu ya Kisiwa hicho kikubwa sanjali na Nchi zingine za Afrika Mashariki..

My Take.

Mambo haya sio ya kupuuza ila pia hayazuiliki maana maafa yatakayokuja kutokea itakuwa simulizi ya Dunia,hiyo ya Uturuki na Syria ni maandalizi tuu.

Ukiangalia Mwenendo wa Matetemeko na Volcano za mara Kwa mara Kwenye milima ya DR Congo Mashariki na matukio ya hivi karibuni ya mauji uji ya magma liyojitokeza kwenye uso wa Dunia hasa Dar na Shinyanga ni viashiria tuu vya mambo hayo makubwa yanayotisha yatakayotokea Duniani.

Maandalizi pekee ya hali hii ni unyoofu wa Moyo vinginevyo ni vilio na Wala hakuna sayansi ya kuzuia nature,kama tuu mabara yalivyotokea ndivyo itatokea pia miaka ya baadae.
Usichojua ni kwamba tukio hili linakamilika pengine baada ya miaka milioni 500, hata binadamu tunaweza tusiwepo tena
 
Finally DRC will no longer be land locked countries
Elimu ni muhimu sana, by the time hii inakamilika ni nimaka milioni 500 inaweza kuwa imepita, pengine hata binadamu tutakuwa tumeshatoweka duniani kama dinasaurs
 
Ikitokea hivyo Visiwa vyote vya karibu na hiyo ardhi itakayomeguka vitapukutishwa na hilo pande la ardhi litakalojimega,kuna hatari kuna nchi au Wilaya zitafutwa kabisa katika sura ya Dunia kama vile Zanzibar yote,Madagaska,Shelisheli,Mafia n.k
Umeshanganya madesa [emoji1787][emoji1787]
 
Na ndio Ziwa lenye kina kurefu Duniani which means maji yanaweza fuata huo ufa pendekezwa
Nilazima yafuate huo ufa maana ni nyanda za juu ilo ziwa ni busta ya kutengeneza bahari mpya kwa haraka zaidi ....nguvu za hayo maji na yalivyo na kina kirefu pressure yake itakuwa kubwa sana yatakapo kuwa yana fuata huo ufa kuelekea baharini
 
Itachukua millions of years, wakati huo kitu kinaitwa binadamu hakitakuwepo tena kwenye uso wa dunia, ukame na nuclear vitakuwa vimeshatumaliza
 
Umeongea kweli lakini kwenye suala la muda (kutokea kwa haraka) mkuu hapo ni hapana. Plate tectonics sio kitu kinatokea overnight, it takes ages mkuu.
Siyo lazima kutegemea plate tectonics pekee ila maji za ziwa tanganyika yakipata mwanya tu na kuanza kuelekea baharini tayari patatokea mto wenye nguvu kubwa sana na kuligawa ilo eneo kwa hatua ya kwanza ...hivyo itakuwa kama mto nail ila wenye nguvu kubwa kutokana na kupita kwenye bonde la ufa
 
Tujiandae si kuzunguzungu hicho wakati wa kufasiri kwenda Australia na je ma chimpanzee tutaenda nayo?? Maana ziwa Tanganyika tunaliacha.

West Africa wanatamanije, maana wao wangeangukia Marekani na Ile mijamaa inavyopenda majuu
 
Finally DRC will no longer be land locked countries
Drc ni landlocked toka lini? Wana coastline kule Atlantic ocean ina km kama 40..
landlocked-countries-in-africa-2.png
 
Hivi kweli kuna mwisho wa dunia? naona mwisho wa dunia yako ni siku unayokufa wewe.

Kwasababu hii dunia tuliyopo ni kama inaendelea kujiumba upya kila baada ya miaka kadhaa, au niseme inajivua gamba.
 
Wanajiolojia wamethibitisha kuwa bahari mpya inaundwa barani Afrika ambayo italigawa bara hilo nusu.

Inasemwa kuwa ufa wenye urefu wa maili 35 ulionekana katika jangwa la Ethiopia eneo la Afar mwaka 2005 na pengine ni mwanzo wa bahari mpya kabisa.

Ukurasa wa The Archeologist umeandika kuwa Jarida la Geophysical Research Letters linalotumia data za tetemeko na utokeaji wa nyufa linasema utengano wa bara la Afrika ulianza taratibu takribani miaka milioni 30 iliyopita.

Mataifa 54 barani Afrika yamegawanywa kulingana na wanajiolojia wanaotafiti juu ya tectonics ya sahani za bara hilo. Ufa wa Afrika Mashariki, unaotenganisha nchi za pwani ya mashariki kama Kenya na Tanzania kutoka sehemu kubwa ya bara, unapitia Msumbiji kutoka eneo la Afar kaskazini mwa Ethiopia.

Chanzo: TBC

--------------

Moja kwa Moja kwenye mada.

Wanajiolojia wanasema Bara la Afrika litagawika kutokana na Bahari Mpya inayoenda kujitokeza.

Kwa Mujibu wa Wataalamu hao Kuna ufa unaoendelea kukua na ulioandia Ethiopia unaozidi kuongezeka kadiri ya Miaka inavyokwenda na hivyo kusababisha matetemeko makubwa ambayo yatakuja kupelekea Drifting ya Bara la Afrika na kuzaa Kisiwa Kipya kikubwa kitakachotenganishwa na Bahari Mpya.

Tanzania itakuwa sehemu ya Kisiwa hicho kikubwa sanjali na Nchi zingine za Afrika Mashariki..

My Take.

Mambo haya sio ya kupuuza ila pia hayazuiliki maana maafa yatakayokuja kutokea itakuwa simulizi ya Dunia,hiyo ya Uturuki na Syria ni maandalizi tuu.

Ukiangalia Mwenendo wa Matetemeko na Volcano za mara Kwa mara Kwenye milima ya DR Congo Mashariki na matukio ya hivi karibuni ya mauji uji ya magma liyojitokeza kwenye uso wa Dunia hasa Dar na Shinyanga ni viashiria tuu vya mambo hayo makubwa yanayotisha yatakayotokea Duniani.

Maandalizi pekee ya hali hii ni unyoofu wa Moyo vinginevyo ni vilio na Wala hakuna sayansi ya kuzuia nature,kama tuu mabara yalivyotokea ndivyo itatokea pia miaka ya baadae.
Miaka milioni 30 ijayo ni keshokutwa tu. Ndiyo maana tumezidua meli mpya ya baharini pale Muanza.
 
Back
Top Bottom