Bajeti 2020/21 Watumishi wa Umma mwaka wa 5 hakuna nyongeza ya mishahara wala punguzo la kodi

Fanyeni kazi mbadala muache kulilia nyongeza,Mimi kamshahara kangu ni kadogo sana,nikikata kila mtu atacheka but sitakaa niililie government yetu iti kwanini hakuna nyongeza

Mishahara hata kwa wafanyakazi wa nchi za ulimwengu wa kwanza haijawahi kutoshereza ije kuwa Tanzania?

Piga kazi mbadala na hiyo uliyoajiliwa nayo.

Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app
 
Reactions: a45
bajeti hii ni ya wananchi wote wa tabaka la chini, kati na juu, wakulima na wafanyakazi, wajasiriamali na wafanya biashara wakubwa sote tunanufaika kwa namna moja au nyingine, hata mshara ulio nao unatosheleza mahitaji yako kwa sababu mfumuko wa bei umedhibitiwa sana. kwa kweli serikali ya awamu hii ya 5 inafanya kazi inayo onekana.

natamani sana katiba ibadilishwe Rais Magufuli aongezewe Muda zaidi maaana siamini bada yake kama tutapata mtu wa aina yake labda baada ya miongo kadhaa.
 
Siasa za Kiafrika Zinakera
Hvi N kwel kuwa hujackia punguzo la kodi linalowabeba wenye mishahara midogo kbx yan

N kwel hujackia au ndo kila ktu tunapotosha tuuu????
 
Watumishi wa Umma ni lzm washughulikiwe hasa, kisasi cha kumpigia Lowasa.
 
Jana nilikuwa napitia page za Raia wa Burundi wengi wanaonyesha kufurahia kifo cha Nkurunziza wengine wameenda mbali zaid nakusema azikwe kama ambavyo alikuwa akiwazika wapinzani na watu waliokuwa wakiikosoa Serikali.
Hongera zao tunawaonea wivu kwa kufiwa kwa kweli
 
Maendeleo ya watu si vipaumbele kuliko majengo kwa maana ni rahisi kukumbukwa kupitia majengo kuliko kupitia watu
 
Hapo inabidi kununua 'katambuga' tu mkuu maana ndala haziwezi kuhimili vishindo.
 
Siasa za Kiafrika Zinakera
Hvi N kwel kuwa hujackia punguzo la kodi linalowabeba wenye mishahara midogo kbx yan

N kwel hujackia au ndo kila ktu tunapotosha tuuu????
Jifunze kwanza kuandika vizuri halafu urudi hapa jamvini.
 
Mtu hataishi kwa mkate tuu, hivyo pamoja na kutoongezwa mishahara, lakini msiwe na hasira bali hapo tarehe 25 October,
unachukua...,
unaweka ...
Waaah...
P
Siasa ni ajira kwa miaka ya sasa hata hao wanaojidai kupiga kelele nao tukiwapa nafasi wanaweza fanya madudu zaidi ya aya unayoyaona sahv
 
Mtu hataishi kwa mkate tuu, hivyo pamoja na kutoongezwa mishahara, lakini msiwe na hasira bali hapo tarehe 25 October,
unachukua...,
unaweka ...
Waaah...
P
Kuu
Naona na wewe umekata tamaa,uko desperate
Mayalla kwa Kisukuma ni Njaa
 
Unaoneka wewe si mfatiliaji mzuri wa mambo.

Hujasikia juzi Wakufunzi wa Chuo kimoja wamekamatwa kwa kuhujumu uchumi, wakati kosa ni kufanya kazi chuo zaidi ya kimoja ili kukuza vipato vyao.

Yani Madaktari wasiwe na dispensaries zao, fundi umeme usifanye part time, na IT usiguse kazi ya mtu..

Alafu unaleta story za kipato cha ziada .

Nyie ndo wale Leo niko masikini huulizi nimepataje umasikini, lakini kesho nikiamka tajiri unakuja kunikamata na kuhoji nimetoa pesa wapi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…