Bajeti 2021/22: Wadau tunakataa kodi ya Majengo kulipwa kwa LUKU

Kodi inalipwa na watanzania ambao ndo hao walalahoi. Watu milioni 60 wakichangia kidogo kidogo sanaa ina maana kubwa kuliko watu 300,000 wakilazimishwa kulipa kodi kubwa na kufungia account zao pale wanaposhindwa.
 
Kodi ya nyumba analipa mpangaji maana katika kipindi cha upangaji nyumba ni ya mpangaji kama ilivyo kwa ardhi yote ya serikali ila mpangaji analipia kodi pia.
 
sio kila jambo linapaswa kupingwa.Unapiga kelele kuhusu kodi ya majengo wakati pesa yenyewe ni hela mbuzi 12,000/= kwa mwaka haina effect yeyote kwa mpangaji.Kama nyumba inawapangaji wa 5 inamaana watalipa chini ya 2000 kwa mwaka mzima.Wapangaji kuna siku wanakaa bila kulipa kodi mfano anapokaribia kuhama wengi wanaomba siku 3 au wiki ndio wanaondoa vyombo.
 
Kodi inalipwa na watanzania ambao ndo hao walalahoi. Watu milioni 60 wakichangia kidogo kidogo sanaa ina maana kubwa kuliko watu 300,000 wakilazimishwa kulipa kodi kubwa na kufungia account zao pale wanaposhindwa.
Ni kweli ila walalahoi ndio wanapewa mizigo mingi kuliko hao watu laki tatu

Selikari inahitaji kuweka kodi zinazo endana na watu wake sio kuleta mrundikano wa kodi zisizo utabiri
 
Kuna wakati unajiuliza hivi hawa tunaita wasomi wa uchumi wanajua uchumi wa wananchi wao kweli au wanajua kuwa wote wamejenga na wana uhakika wa kula Milo mitatu kama wao

Mungu awape akili mpya hizi zilizo tumika wazitupe kule
akili wanazo sema maarifa ndo hawana kibaya zaidi wengine walikotoka umeme umeenda baada ya mradi wa rea
 
Yaani ni uduwanzi wa kiwango cha 5G!
Kushusha kodi bia, kamari kisha kuongeza LUKU na 100 au 200 kwa kadi za simu kwa siku
 
Yaani ni uduwanzi wa kiwango cha 5G!
Kushusha kodi bia, kamari kisha kuongeza LUKU na 100 au 200 kwa kadi za simu kwa siku
Unataka kodi ilipwe na walevi tu?

Hii ikipitishwa ndo maana halisi ya uzalendo utaipata.
Uzalendo haupimwi kwa kufurahia matajiri kuwa mashetani, unapimwa kwa kujitolea kwa nchi yako kama wanajeshi wanavyojitolea huko mipakani kukulinda wewe utoe maoni humu kuikosoa serikali.
 
Wandugu tunahitaji kukusanya kodi. Sio ili imnufaishe Mwigulu au Mama Samia. Kila siku tunasema hawa wenzetu walioteuliwa au kuchaguliwa kuwa viongozi hawana uwezo wa kuongeza wigo wa kodi. Kila siku wanazunguka mlemle. Sisi wenye mawazo ya wigo mpana wa kodi tunayakalia kichwani, utadhani tunasubiri uteuzi au hadi vyama vyetu vitakapochukua nchi.

Sasa wameleta hili - kodi ya majengo. Njia rahisi sana ilikuwa ni kuuboresha huu mpango wa kodi, lakini kama haufai kabisa, tuwape maeneo mengine yenye wigo mwingine wa kukusanya kodi na pia tuwape njia nzuri zaidi ya kukusanya kodi ya jengo, maana ni lazima tulipe.

Hata hivyo, ingawa kodi ya jengo anapaswa kulipa mwenye jengo, bado mwisho wa siku kama kweli mwenye jengo alikuwa analipa kodi, basi mlipaji halisi alikuwa anayetumia jengo husika.
 
Toa altenatives acha kulalamika..
Hakuna alternatives zaidi ya Serekali kupunguza matumizi kufukuza wabunge wasio na vyama vya siasa kurudisha pesa zinazopote hakutakua na kodi mpya
 
Mk
Uroho tu wa kukusanya kila kitu.
Mkuu sasa tufanye nini? Ili huu UROHO usiwepo. Kama tumekubaliana kuwe na Serikali ya Mtaa na Serikali Kuu, sasa kwa nini Serikali Kuu inachukuwa kila aina ya madaraka/mamlaka ya Serikali za Mitaa? Serikali Kuu ina maeneo mengi na tena makubwa ya MAPATO (bandari, migodi, kilimo, viwanda, Utalii etc) lakini bado wataka na kodi za: choo za stand, machinjio, majengo, tozo za wachinga etc) ambazo kimsingi ni za Serikali za Mitaa. Wabunge na Madiwani tatueni suala hili.
 
Naamini litafanyiwa kazi. Hata pesa za mabango ziondolewe huko serikali kuu.
 
Dah! Yan ulipe pango ulipie umeme na bado kodi ya jengo umlipie? Sa mwenye nyumba atakuwa anagaramia nini kwenye nyumba yake?
 
Tufunge mkanda tulipe ili taifaletu lisonge mbele,mbona ktk mambo ya anasa tunachangia kwahiari. Kwakweli ktk hili namuunga mkono Mwigulu licha yakua namie nimpangaji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…