Bakari Kazungu: Acheni kuwasingizia Heche na Mnyika kuhusu mauaji ya Ali Kibao

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutoka mkoani Tanga, Kazungu Bakari Kazungu, amewatolea uvivu vijana wanaojiita wanaharakati, Joseph Yona na Ahmed Kombo, kufuatia tuhuma zao nzito dhidi ya viongozi wa CHADEMA, akisema kuwa kauli zao hazikidhalilishi tu chama tawala bali pia zinaumiza familia ya marehemu Ali Kibao.

Akizungumza, Kazungu amehoji ujasiri wa vijana hao kumtaja Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika, na John Heche kuwa wanahusika na genge la mauaji ya aliyekuwa mwanasiasa mwandamizi, Ali Mohamed Kibao, aliyeuawa Septemba 2024.

Kazungu amewashangaa vijana hao kwa kujifanya wanajua mambo ya kiusalama na kisiasa kuliko viongozi wakuu wa nchi. Alirejea kauli ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM na sasa Makamu wa Rais wa Tanzania, Dkt. Emmanuel Nchimbi, ambaye aliwahi kumuelezea Mnyika kama mtu asiye na sifa za kufanya vitendo vya kikatili.

“Mnatudhalilisha wanachama wa CCM kwa sababu hamjulikani mnatokea wapi. Nchi sasa hivi ipo kwenye mpango wa maridhiano ili kusafisha tulipokosea, ninyi mnahangaika kuzua taharuki," ameongeza kada huyo.
 
Tatizo la nchi hii ukiwa upande wa mtawala unaweza kusema au kufanya chochote na polisi watakuwa kama hawakusikia au kuona.

Hao mazafakas wangekuwa wamesema Nchimbi na Wasira ndio wanahusika na mauaji ya Mzee Kibao, polisi wangewadaka kesho yake (kama sio siku ileile) na saa hizi tungekuwa tunaongea mambo mengine!
 
Back
Top Bottom