Ndugu mbumbumbu, mpira ni mchezo wa wazi , ukicheza vizuri utasifiwa na ukiharibu uta ambiwa pia. Bakari ni mchezaji wa Yanga na Captain wa timu, Leo hakuwa na mechi mzuri.
Ukiachana na ilo la mawasiliano na kipa, Kuna mpira aliucheza na aka anguka na hakujua ulipo jamaa wa Ahly aliupitia na kutoa pasi iliyo mkuta mchezaji wa Ahly akiwa yeye na Diara bahati kipa akafanya save ya kibabe ikawa Kona.
Kwenye mipira ya Kona yeye ndiye mrefu kwenye ukuta wa Yanga, lakini katika mipira zaidi ya sita amefanikiwa kucheza mmoja.
Anahitajika kurudisha kujiamini haraka Sana kwakua soka analijua.