Bakhresa, Mo Dewji na GSM wajitosa kuwekeza kwenye SGR

Kwani boss Kafulila anasemaje juu ya hili. Lugha nyepesi ni kuwa mradi not vaible ngoja wajuwaji waje
 
Hapo muwekezaji wa maana ni bakhresa tuu na kwa mbaaali GSM hiyo MO asubiri kwanza haaminiki.
 
Ni aibu kuwa Mtanzania. Namshukuru Mungu kuwa na mataifa mengine mawili naweza ikana. Hivi Tz nzima hakuna watu wenye uzoefu na weledi wa kuendesha chochote? Je Tz nzima watu hawana vichwa ni wana viwiliwili tu? So tunaweza kuiba na janja janja!!!
Ilishindikana tangu Nyerere,tulishindwa ATC, TRC,bandari,ttcl na Sasa udart
 
Ujamaa umetuharibu,
Kwa hio unaona hilo ni baya? Mbona barabarani kuna malory kibao
Nchi hii Nyerere alituchelewesha na anaendelea kutuchelewesha. Kesho atakuja kulalamika huduma mbovu za treni wakati hataki wabia
 
Ni vema ukayafahamu haya mapema kwa faida yako

Bali wadau wengi wanajiuliza kwamba ni kitu gani ambacho Serikali ya Tanzania inaweza kufanya, maana unaambiwa ni afadhali hata mtoto mwenye Polio waweza kumpa Magongo akatembea mwenyewe
Sijakuelewa malalamiko yako ni nini?

Unataka mali ya umma isiwe ya umma au vipi?
 
Sahihi kikubwa ni huduma nzuri na nafuu kwa Watanzania + na kodi stahiki kwa Serikali..
Pamoja na kukubaliana na wewe kwa kiasi fulani; lakini haina maana huduma hizo haziwezi kufanywa kwa ufanisi na mashirika ya kiserikali. Hii dhana potofu ya kufikiri serikali haina uwezo wa kufanya kitu kwa ufanisi. imekuwa mzigo mzito sana katika akili zetu siku hizi.

Ethiopian Airways ni shirika linaloingiza faida kila mwaka, ni shirika la serikali. Hapo Kenya SGR yao inaendeshwa na shirika lao la kiserikali; wamefunzwa vyema na waChina, hadi sasa wanakwenda vizuri
Mashirika mengi ya kiChina yapo kila mahali duniani, yanafanya kazi kibiashara kwa ufanisi.

Sijatamka popote kwamba sekta binafsi isihusishwe, lakini ni lazima pia kujuwa athari zinazotokana na kutegemea kila kitu, hasa maeneo nyeti hiyo sekta. Wananunua serikali kwa manufaa yao, kama tunavyoona inafanyika sasa hivi.

Hizo huduma nafuu unazozililia utazisikia tu, hutaziona.
 
Kama wananchi tutaendelea na ukomdoo huu, umbumbumbu huu, uzombi huu, basi tutarajie Kodi zetu kuendelea kufujwa, mikopo kuendelea kutafunwa na miradi kudumaa.
 
Nchi hii Nyerere alituchelewesha na anaendelea kutuchelewesha. Kesho atakuja kulalamika huduma mbovu za treni wakati hataki wabia
Angalia mbuzi kama huyu hapa. Anachojuwa yeye ni kumlaumu Nyerere tu huku hakuna jingine lolote alijualo.
Tunyeshe ambako Nyerere hakuwepo walivyoweza kuwa tofauti na Tanzania.
Nimekupa jina hilo maksudi, kwa sababu linakufaa sana, na uje hapa kwa moto.
 
Aseee, tutengeneze watoto na wajukuu zetu waingie kwenye mfumo wa siasa za kiccm vinginevyo tutaambulia magugu maji!.

Tuendelee kuwa keyboard fighter behind!.
 
Nashukuru, ushauri wangu huu, Watanzania tujifunze kukubali kuna vitu hatuwezi, tunaposhindwa tukubali kusaidiwa au tukomae? Baada ya Bandari ni ATCL na SGR au Tusubirie? ushauri huu umefuatwa kwa SGR, bado ATCL.
P
 
Huu ni utekelezaji wa ushauri huu Watanzania tujifunze kukubali kuna vitu hatuwezi, tunaposhindwa tukubali kusaidiwa au tukomae? Baada ya Bandari ni ATCL na SGR au Tusubirie? sasa bado ATCL,
Kazi iendelee.
P
 
Kwani Serikali imeshindwa nini mbona imeweka pesa nyingi sana?
Reli ni sawa tu na barabara mwenye Roli au gari yake ruksa kutumia. watakachofanya ni kulipia
Askofu Gwajima pia alikuwa.na mpangia wa kuleta treni yake ya abiria akishirikiana na wawekezaji Toka Japan

Sio kitu kikubwa

Mfano Uganda bakhresa ana treni zake za mizigo anatumia reli ya Uganda

Ni kitu kizuri reli inatakiwa kuwa busy sio Kwa wiki mara moja ndio unaona treni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…