Bakhresa, Mo Dewji na GSM wajitosa kuwekeza kwenye SGR

Hapo wanaiba nini? Kwani kuleta treni yako ili utoe huduma kuna dhambi gani?
 
Hapo wanaiba nini? Kwani kuleta treni yako ili utoe huduma kuna dhambi gani?
Nashangaa

Reli ni barabara tu mwenye chombo chake Cha kupita humo ruksa Kwa makubaliano tu ya malipo ya kutumia hiyo reli
Tatizo watazania Wengine wamezoea Biashara vidogo vidogo visivyokua hivyo akiona biashara kubwa hivi anashangaa ohh itakuwaje
 
Watanzania angalieni yaliyojiri kwenye Mwendokasi! Mimi naona akikipewa Baresa ni poa ila atoe shares ili nasi tushiriki
 
Nani kawazuia matajiri wasio wahindi,Waarabu na Waislamu wasiwekeze kwenye reli hii?
Taratibu unaiingiza ubaguzi wa rangi na dini kama Lema.
 
Sioni tatizo, kama wanaweza kuwekeza wawekeze tu. Money is Money.
Ilimradi sheria na taratibu za uwekezaji zifuatwe, wasipewe favors.
 
Wamejazwa wajinga kuendesha chombo cha kisasa, unategemea nini zaidi?

Tegemea mashine zote za tiketi na malipo ya kupitia simu kutokufanya kazi ndani ya miezi mitatu.
Hapana.
Sijui kwa nini napishana fikra nawe mara nyingi hivi, hata katika mambo rahisi kama hili hapa, ambapo katika hali ya kawaida kabisa tungeweza kuwa upande mmoja. Mimi hapa sioni "ujinga", bali naona kukosa mwongozo na uongozi wa kuhakikisha hali hiyo uliyo ielezea isiwepo.
Kila mtu atimize wajibu wake kama alivyo pangiwa, na wanaosimamia nao wahakikishe wamesimamia ipasavyo.

Hivi sisi tutakuwa watu wa kuwategemea wengine hadi lini?
 
Serikali imekopa matrilioni zitakazolipwa na tozo za wananchi - halafu leo mabepari wanavamia na kufaidi uwekezaji wa serikali
Kwanini wasijenge hao matajiri?
 
Hadi tukifuta ujinga.
 
HONGERA SANA KUFIKIA MAAMUZI SAHIHI ya kuruhusu sekta binafsi kutoa huduma ya usafiri wa treni kwa kutumia miundombinu ya reli ya serikali. Nilishasema humu ya kwamba kwa mfumo wa sheria za utumishi wa umma zilivyo, ni vigumu sana sector ya umma kutoa huduma y viwango na ya uhakika ya usafiri wa treni, hasa ya SGR. Ingekufa tu mapema sana. Uamuzi huo ni mzuri sana unaenda kuleta ushindani,ubora na uhakika wa usafiri wa treni, hasa SGR.
 
Serikali imekopa matrilioni zitakazolipwa na tozo za wananchi - halafu leo mabepari wanavamia na kufaidi uwekezaji wa serikali
Kwanini wasijenge hao matajiri?
Kwani matabaka katika jamii hujengwa vipi?

Hawa matajiri sasa wanayo serikali yao. Hawa ndio kipaumbele cha serikali. Wao wana sauti nzito zaidi serikalini kuliko hao akina hohehahe.
Hawa ndio wanaoiamrisha serikali ifuate mipango yao, ya kuwafaidisha zaidi kupitia mgongoni kwa hahehoi.
 
Nakuelewa Mzee wa Malumbano ya hoja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…