Bakhresa, Mo Dewji na GSM wajitosa kuwekeza kwenye SGR

Mashirika ya serikali mangapi tuliyokuwa nayo toka tumepata Uhuru hadi hii leo? Lipi lililofanya kazi kwa faida?
 
Lini Watanzania walimfuta adui ujinga?

BRT imewashinda kuendesha, mtaweza SGR?
Unawadharau waTanzania, huku unasahau wanao wasababishia kudharauliwa?
Ungekuwa umefuta ujinga ungejuwa wapi pa kuelekeza lawama zako, lakini najuwa ujinga ni mzigo mkubwa. kwako.
 
Mashirika ya serikali mangapi tuliyokuwa nayo toka tumepata Uhuru hadi hii leo? Lipi lililofanya kazi kwa faida?
Huu nao ni mjadala unaotaka tutumie muda mwingi kuujadili?
Katika muda huo wakati mashirika hayo yakifa, ni matajiri gani wakubwa walioibuka na kushamiri bila ya kuitegemea serikali hiyo hiyo; kwa kuiibia, au kushiriki katika kuuwa hayo mashirika ya umma!
 
🙋‍♂️👍👌🤝👏👊🙏💐🎁🛡️

⚖️Justice for Asimwe#
 
Mimi naona sawa tu! Kama serikali inaona haiwezi kuiendesha SGR bora itafute wawekezaji!
 

View: https://twitter.com/Sisimizi3/status/1803480214581678486?t=5E4D54qSElTJnCjtgg9LqA&s=19
 
Mi kwa maoni yangu naona bora kwa miaka 5 kwanza Serikali isimamie yenyewe.

Ikifanya hivyo itajua ups and down za SGR na kujua namna ya kufanya.

Katika kipindi hicho wakiona hawaiwezi hiyo SGR wa-outsource makampuni yenye sifa wasimamie na wampe target mfano makusanyo ya Bil100 kwa mwezi baada kwa kuzingatia trend ya makusanyo waliyokutana nayo ndani ya hiyo miaka 5

Tena hyo kampuni itakayopata zabuni, isipewe kila kitu,wazipe zabuni kampuni tofauti tofauti kwa kandarasi tofauti tofauti,mfano Ticketing,service za train,n.k ili kuleta ufanisi na ushindani,na wote wapewe targets.
 
Uko sahihi.

Ila Mimi msimamo wangu ni ule ule,hiyo Sgr ni cosmetic project ya kupigia picha ,haiwezi na haitakuja kurudisha hela achilia mbali kuleta faida.
 
Ni jambo zuri kwani serikali ingekaa kando tu kwenye miradi hii mikubwa maana upigaji ni mwingi kuliko faida
Kama wanawekeza ni sawa tu wawe na shares
 
Hao ni wahujumu au wawekezaji?

Yaani wamiliki wa biashara ya mabasi na maroli ya mizigo ndio wawekeze sgr?

Hao wanakuja kuua treni na kuhujumu Miundombinu!!

The good thing is, 2025 tuna Rais mpya.

Watashindana lakini hawatoshinda.
 
Hakuna jambo linalo kosa mwisho mkuu
Basi nimekuelewa.
Kwamba mwisho unaweza kuwa kila mmoja wetu hii leo atakapofikia ukomo wa maisha yake. Hapo ndipo itakuwa mwisho wa maumivu chini ya CCM, ndani ya Tanzania.

Mimi nisingependa mwisho huo. Mwisho ninaoutafuta ni kuondokana na CCM wakati wa uhai wangu, na itapendeza zaidi isiendelee kuwepo madarakani 2025 chini ya uongozi huu uliopo sasa. Hilo ndilo tamanio langu kuu kwa manufaa ya taifa letu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…