BAKITA yaonya kuhusu maneno kama Famasiala na Fautani

BAKITA yaonya kuhusu maneno kama Famasiala na Fautani

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
BARAZA la Kiswahili Taifa (BAKITA) limeonya matumizi ya maneno “Famchezo nini, Famasihara nini, na Fautani nini” yanayotumiwa na watu katika majukwaa mitandaoni likisisitiza kuwa maneno hayo sio fasaha wala sanifu.

Limeshauri watumiaji wa Kiswahili kutumia maneno “Unafanya mchezo nini, Unafanya masihara nini na Unafanya utani nini” ambayo ni fasaha na sanifu ikiwa ni sehemu ya kujivunia kiswahili ambacho ni tunu ya Taifa.

1678871287037.jpeg

1678871299428.jpeg

======

BAKITA yakanusha kutoa onyo la matumizi ya maneno hayo

Zaidi Tembelea jukwaa la Jamii check UZUSHI - BAKITA waonya kuhusu maneno Famasiala, Fautani
 
BARAZA la Kiswahili Taifa (BAKITA) limeonya matumizi ya maneno “Famchezo nini, Famasihara nini, na Fautani nini” yanayotumiwa na watu katika majukwaa mitandaoni likisisitiza kuwa maneno hayo sio fasaha wala sanifu...
Ukisikia umangimeza wa lugha ndo huu.

Kuna maneno lukuki ya ajabu ajabu ya kidijitali yametungwa na BAKITA hayana asili ya kiswahili wanatulazimisha tuyatumie.

Sisi hatujapiga kelele. Lakini sisi tunagengeneza slangs zetu wanaanza kutujia juu.

Kwanza kiswahili siyo chao.

Wao wana wajibu wa kukikuza na kukieneza kiswahili.

Pili, kiswahili cha kimvita ndo haswaa chenyewe lakini wao wanatuzungumzisha cha kizaramo.

Watuache
 
BARAZA la Kiswahili Taifa (BAKITA) limeonya matumizi ya maneno “Famchezo nini, Famasihara nini, na Fautani nini” yanayotumiwa na watu katika majukwaa mitandaoni likisisitiza kuwa maneno hayo sio fasaha wala sanifu.

Limeshauri watumiaji wa Kiswahili kutumia maneno “Unafanya mchezo nini, Unafanya masihara nini na Unafanya utani nini” ambayo ni fasaha na sanifu ikiwa ni sehemu ya kujivunia kiswahili ambacho ni tunu ya Taifa.

NWAPONGEZA BAKITA KWA HILI KUBWA WALILOFANYA HII YOTE INALETWA NA HAWA WAZARAMO WA HAPA MJINI AMBAO WENGI WAO HAWAJAKWENDA SHULE NDIO WANAYOLETA HAYA MAUJINGA KUMBE HAWAJUI WANAHARIBU LUGHA YETU MAMA NA ADHIMU YA KISWAHILI NA NDIO MAANA HUWEZI KUWAKUTA HAPO BAKITA KIKAZI NA NDUGU ZANGU WAKURYA NA WASUKUMA WAO WAENDE JESHINI NA WAZARAMO WABAKIE NA VIGOMA VYAO FOOLISH
 
Yaani Tanzania unaweza ukajikuta una shangaa elimu ya kila mtu. Sasa BAKITA watu wa lugha si wanajua kabisa kuna mofimu, misimu, misemo n.k sasa inakuwaje tena?.

Ingekuwa yanatumika rasmi hapo sawa, mfano kwenye hotuba ya raisi tusikie neno Famchezo wewe au kwenye taarifa ya habari hapo tungeshtuka kiasi.

Hayo maneno yanatumika kwenye mizaha au utani bado nongwa. Wanatakiwa kukumbuka ladha ya maongezi hayo ya masihara/utani inaletwa na Fa

Anyway kila mtu na lake.
 
Back
Top Bottom