BAKITA yaonya kuhusu maneno kama Famasiala na Fautani

Baraza la Kiswahili nchini Tanzania (BAKITA) limepiga marufuku matumizi ya maneno mapya yaliyozuka hivi karibuni yanayotumiwa na Wasela wengi wa mjini na baadhi ya Watangazaji wa redio ya "FAMCHEZO na FAMASIHARA" badala FANYA MCHEZO na FANYA MASIHARA , Kutumika popote nchini Tanzania .

Marufuku hiyo inaanza mara moja , japo haijafahamika wale watakaokaidi watachukuliwa hatua zipi .
Ila maneno ya kiarabu kama MUBASHARA wanakubali kufuta LIVE lililozoeleka
 
Naona Bakita wamesahau kwamba huwa kuna Lahaja za Msimu.

Wakitaka yasitumike inabidi kuongezea atakayeyatumia atachukuliwa hatua gani bila hivyo si ajabu hayo maneno yakatumika mara mbili ya hapo mwanzo.
 
Hawa BAKITA ni watumishi wa umma wanaolipwa na serikali?
 
Baraza la Kiswahili nchini Tanzania (BAKITA) limepiga marufuku matumizi ya maneno mapya yaliyozuka hivi karibuni yanayotumiwa na Wasela wengi wa mjini na baadhi ya Watangazaji wa redio ya "FAMCHEZO na FAMASIHARA" badala FANYA MCHEZO na FANYA MASIHARA , Kutumika popote nchini Tanzania .

Marufuku hiyo inaanza mara moja , japo haijafahamika wale watakaokaidi watachukuliwa hatua zipi .
Wachafuzi wa lugha wamepigwa pini...😂😂😂
 
Back
Top Bottom