Kwa haraka haraka nimeona comment za wengi humu hawaelewi kiundani hoja ya mtoa mada na uzito wa hiyo hoja. Ni kweli sio lazima kwenda jeshini kama career ila nadhani ni sheria kwa wahitimu wa form six kwenda huko ili wapate kigezo mojawapo cha kuajiriwa serikalini.
Kwa yote mawili ya career ama post form six requirement raia wote wanapaswa wawe na haki sawa ya kushiriki. Serikali haina dini na pia haipaswi kumvua mtu dini yake, so kumlazimisha binti wa kiislamu kuvua dini yake kimavazi na hata kumnyima haki yake ya kuabudu hii ni kinyume na katiba kwa kuwa watu wote ndani ya Tz wana haki ya kuabudu kwa imani zao. Napenda wasiokuwa waislamu waelewe kuwa Uislamu sio kusali tu bali ni mfumo mzima wa maisha ya mtu so hauwezi kumchagulia wewe kipi akifanye katika dini yake na kipi akiache.
Ili kuhakikisha raia wote wamepewa haki sawa nadhani kuna haja ya kuweka option ya usimamizi tofauti (Female only) na huo wa mchanginyo. Mwanamke wa kiislamu na wakikristo wanaweza kuchagua pande ya kujiunga katika hizo, then yule muislamu atakuwa na dharura ya kupunguza katika mavazi (ikiwemo kutovaa babaui) kwa kiwango kinachokubalika katika dini akiwa yupo na wanawake wenzake tu.
Hivi niulize tu, ni percentage ngapi ya female soldiers wanaoshiriki kwenye mapigano ya vita moja kwa moja?