Bakwata uislaam huo mmeutoa wapi? Kumbukeni moto ni mkali sana mtaenda chomwa

Soma kwanza aya uelewe kisha uulize maswali ya msingi,tatizo hata aya zenyewe hamsomi. Aya iko wazi, sasa nashangaa unavyouliza swali au kujenga hoja mufilisi namna hii.

Ahsante.
Kama hivi ndivyo unavyomnasihi muislam mwenzako sipati picha asiyekuwa muislam unamnasihi vipi!

Nakubali kama ulivyosema kwamba sina hoja ya msingi, aya zenyewe sizisomi na huwa nauliza pasipo kuzielewa.

Nakutakia kila la heri.
 
Kama hivi ndivyo unavyomnasihi muislam mwenzako sipati picha asiyekuwa muislam unamnasihi vipi!

Nakubali kama ulivyosema kwamba sina hoja ya msingi, aya zenyewe sizisomi na huwa nauliza pasipo kuzielewa.

Nakutakia kila la heri.
Ahsante.

Tuko pamoja.
 
Bakwata haikuanzishwa na waislaam, bakwata ni ya CCM
Hata CCT na wenyewe ni mali ya CCM! Hawa utawasikia wakifungua midomo kama Ikulu yupo mtu asie wa imani yao, lakini akiingia wa imani yao, kimya kabisa! Miaka hii kwa mfano, ushawasikia wakikemea yanayoendelea?! Ushaisikia ile miwalaka iliyokuwa inatolewa awamu iliyopita? Kule kupigwa risasi kwa risasi, na zile maiti zilizokuwa zinaokotwa kwenye viroba ingekuwa Ikulu kuna asiye wa kwao, ungeona makemeo yao!

Viongozi wa dini Tanzania hii ni wanafiki sana; hakuna cha Waislamu wala Wakristo. Kinachowaponza sana wale wa Kiislamu kiasi cha kuonekana ni CCM sana ni ile hali yao ya kuchanganyika sana na jamii jambo ambalo kwa viongozi wa Kikristo sio sana. Matokeo yake, wanapokuwa na mahaba na chama, mahaba hayo yanaonekana wazi wazi kuanzia kwenye ngazi za mtaa!
 
Hapa nazungumzia uovu wa hawa bakwata sio masuala ya dini nyingine... .
Nikuulize wewe ulianzisha hii mada ili kuwaponda BAKWATA au kuwatetea wanawake?

Maana umesema maneno ya haqi ukikusidia batili.
 
BAKWATA ipo kisheria kushughulikia masuala ya Kiislam pia ina majukwaa mahsusi ya kuwasilisha na kutatua mikwamo inayowasibu waislam. Kikwazo kuna makundi ya Kiislam yaliyo na maslahi binafsi wameamua kupinga kila jambo lifanywalo na BAKWATA. Mwasilisha mada unapaswa uende ofisi ya BAKWATA iliyo karibu nawe kuwasilisha dukuduku husika
 
Fact, ila ahlu jazba wal- balaa hawatokuelewa.
 
Hapa ndiyo pazuri hadi sheikh Alhdi wapo wanasoma maoni ya wadau.
 
Nidyo, nyie ni wapigaji hivyo muache upigaji. Msiwadhulumu wenzenu.

Uislamu ni mzuri ila nyie ndio mnauchafua

Hapa ni jukwaa sahihi kabisa na lengo la mtoa mada ni kutujuza na kuwaelimisha wanawake kuwa Bakwata Kata hawana mamlaka hivyo waende tu kwa kadhi wa Wilaya na wakiambiwa kuhusu hela wahoji kama hawana wafanyeje!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…