Bakwata uislaam huo mmeutoa wapi? Kumbukeni moto ni mkali sana mtaenda chomwa

Bakwata uislaam huo mmeutoa wapi? Kumbukeni moto ni mkali sana mtaenda chomwa

Soma kwanza aya uelewe kisha uulize maswali ya msingi,tatizo hata aya zenyewe hamsomi. Aya iko wazi, sasa nashangaa unavyouliza swali au kujenga hoja mufilisi namna hii.

Ahsante.
Kama hivi ndivyo unavyomnasihi muislam mwenzako sipati picha asiyekuwa muislam unamnasihi vipi!

Nakubali kama ulivyosema kwamba sina hoja ya msingi, aya zenyewe sizisomi na huwa nauliza pasipo kuzielewa.

Nakutakia kila la heri.
 
Kama hivi ndivyo unavyomnasihi muislam mwenzako sipati picha asiyekuwa muislam unamnasihi vipi!

Nakubali kama ulivyosema kwamba sina hoja ya msingi, aya zenyewe sizisomi na huwa nauliza pasipo kuzielewa.

Nakutakia kila la heri.
Ahsante.

Tuko pamoja.
 
Bakwata haikuanzishwa na waislaam, bakwata ni ya CCM
Hata CCT na wenyewe ni mali ya CCM! Hawa utawasikia wakifungua midomo kama Ikulu yupo mtu asie wa imani yao, lakini akiingia wa imani yao, kimya kabisa! Miaka hii kwa mfano, ushawasikia wakikemea yanayoendelea?! Ushaisikia ile miwalaka iliyokuwa inatolewa awamu iliyopita? Kule kupigwa risasi kwa risasi, na zile maiti zilizokuwa zinaokotwa kwenye viroba ingekuwa Ikulu kuna asiye wa kwao, ungeona makemeo yao!

Viongozi wa dini Tanzania hii ni wanafiki sana; hakuna cha Waislamu wala Wakristo. Kinachowaponza sana wale wa Kiislamu kiasi cha kuonekana ni CCM sana ni ile hali yao ya kuchanganyika sana na jamii jambo ambalo kwa viongozi wa Kikristo sio sana. Matokeo yake, wanapokuwa na mahaba na chama, mahaba hayo yanaonekana wazi wazi kuanzia kwenye ngazi za mtaa!
 
Hapa nazungumzia uovu wa hawa bakwata sio masuala ya dini nyingine... .
Nikuulize wewe ulianzisha hii mada ili kuwaponda BAKWATA au kuwatetea wanawake?

Maana umesema maneno ya haqi ukikusidia batili.
 
TANBIHI: Mods naomba uzi huu msiufute na mkiuhamisha basi nifahamisheni mmehamishia wapi?

Nayaandika haya nikiwa na uchungu mkubwa rohoni mwangu. .. Nikiangalia wale walio pewa mamlaka ya usimamizi wa sheria ya Allah wanafanya mambo mazito ya kumuasi Allah na kudhulumu watu...

Kwanza nibainishe MIMI SIO MTU WA KUENDESHWA NA MIHEMKO YA KIHARAKATI... SINA CHUKI JUU YA BAKWATA NA NAWAHESHIMU SANA KWA SABABU NDIO CHOMBO TEGEMEWA CHA KUWASEMEA WAISLAAM NCHINI NA KUISIMAMISHA SHERIA YA ALLAH. .. LAZIMA TUKITII NA TUKIHESHIMU BILA SHAKA. .. NA NAKITII NA KUKIHESHIMU CHOMBO HIKI. ..

Bakwata Mashaa Allah, Allah amejaalia lwa serikali hii kuruhusu WAISLAAM kujihukumia mambo yao msingi ya kijamii yenyewe na MIFUMO YA KIDOLA ikazitambua na kuzirasimisha sheria hizo(NDOA, TALAKA NA MIRATHI). . . NA HUKUMU ITAKAYOTOLEWA NA BAKWATA KWENYE MASUALA HAYO MAHAKAMA ZA NCHI HAZIWEZI INGILIA.. .

TUMSHUKURU ALLAH KWA HILO.. . Ni jambo mlilolipigania kwa muda mrefu kupata mahakama ya Qadhi, ili waislaam tujihukumie mambo yetu wenyewe bila kuingiliwa kwenye ibada hizo. ..

Kumbe bhanaa wenzetu BAKWATA na BAADHI viongozi Wake waliliangalia kwa jicho la kimaslahi(LA KIUPIGAJI) . .. MCHENI ALLAH NYIE WATU.. . ADHABU YA ALLAH NI CHUNGU. ..HAMTOOKOKA NA VIREMBA VYENU WALA VYETI VYENU VYA THANAWY MLIVYOVIPATIA TANGA...

Mathalani. .. KWENYE MASUALA YA NDOA. .. SIKU ZOTE UKIONA SUALA HILO LIMEFIKA KWA QADHI UJUE MLETAJI NI MWANAMKE(MKE). ..

Kwa sababu Kisheria MWANAUME hapati shida amepewa Mamlaka, YAKIMKERA ANAACHA TU(TALAKA). ..

Ila mwanamke hana uwezo wa kutoa Talaka, Suluhisho lake ni kwa Qadhi...

Na kwa mfumo wenu wa uendeshaji QADHI MMEMUWEKA KUANZIA WILAYA kisha MKOA kisha TAIFA. ..

LAKINI wa kumpata huyo QADHI sasa ndio unaleta ukakasi. ..

Binti akiwa na tatizo kwenye ndoa yake na Mumewe anabidi aanzie shauri lake BAKWATA KATA ili lifike kwa QADHI WA WILAYA. ..

Huko KATA sasa ETI BINTI MASKINI ANATOZWA KUANZIA SH. 15,000/- Ili tu shauri lake lifunguliwe na lisikilizwe. ..

Tujue kabisa OFISI YA BAKWATA KATA HAINA MAMLAKA YA KUSIKILIZA NA KUIAMUA KESI ILI WATAPOTEZA TU MUDA WAKO ILA MWISHO WA SIKU UTAPEWA BARUA UENDE BAKWATA WILAYANI. ..

Ukifika BAKWATA WILAYA kabla hawajakusikiliza lolote... NENDA KADEPOSIT SH. 30,000/-...

ILA KUMBUKA MWENYE MAMLAKA YA KUSIKILIZA NA KUAMUA NI QADHI NA SI BAKWATA(Si sheikh wa wilaya wala katibu wake). . . Ila hela yako wanaitaka...

Kwahiyo mwisho wa siku lazima upelekwe kwa Qadhi. ..

Sijajua na hadi kufika huko kwa Qadhi nako inabidi utoe kiasi gani!

KINACHONIUMA ROHO SIO HELA WANAYOIPIGA. ..

Ila ni HUYU MWANAMKE aliyepeleka Kesi huko. .. KUMBUKA KISHERIA YA KIISLAAM MWANAMKE ANATAKIWA AKAE NYUMBANI NA WATOTO ALEE FAMILIA NA AMTII MUMEWE TU. .. Suala ya kufanya kazi limeruhusiwa kwa mwanamke ila INATILIWA NGUVU ZAIDI ASIFANYE KAZI. ..

ANAYEMHUDUMIA MWANAMKE NI MUMEWE. ..

SASA FIKIRIA Mwanamke amegombana na Mumewe anayemhudumia. .. Ikafikia hatua anahitaji msaada kutoka kwenu BAKWATA. .. LAKINI NINYI MNAMCHAJI OVER SHS. 45,000/- ILI APATE HUDUMA NA MSAADA WENU ILI APATE HAKI YAKE. ..

Sasa hiyo hela anaitoa wapi MDHAIFU HUYU. ..? BADALA YA KUMSAIDIA KUMPA HAKI YAKE MNAMUONGEZEA MATATIZO?

UISLAAM WENU MMEUTOA KWA SHEITWAANI GANI?

MBONA HATA HAMUMUOGOPI ALLAH... HIVI HATA MTUME ANGEKUWA ANAFANYA HUU UPUMBAVU WENU. .. HUU UISLAAM USINGEFIKA HAPA ULIPO. ..

MTUME AMESEMA "ZICHENGUENI HAKI ZA MADHAIFU WAWILI HAWA, NAO NI WANAWAKE NA MAYATIMA".

Lakini ninyi mnashiriki kuwakandamiza. ..

Mcheni Allah ndugu zangu. ..

MTAFANYA WAUKIMBIE UISLAAM NA WAULALAMIKIE UISLAAM KWA TAMAA ZENU ZA MAISHA YA DUNIA YASIYO CHOCHOTE. ..

MNATUPELEKA WAPI NYIE WATU MSIOMUOGOPA ALLAH. ..

MNA TOFAUTI GANI NA WAPIGA DILI WA RICHMOND NA WALA RUSHWA. ..

NYINYI MTACHOMWA KWA KUDHULUMU MALI ZA WATU KWA KUZILA PASIPO HAKI. ..

KAMA MLITAKA KIPATO MNGEKUWA NA SUBRA MKAMSIKILIZA HUYO DHAIFU ALAFU MWISHO MTWANGENI HIZO GHARAMA MWANAUME. .. ILA MWANAMKE MNAMUONEA ANAZIPATA WAPI?

AKIWA HANA MAANA YAKE AKAENDELEE KUMUASI ALLAH KWA ZINAA KWA MLOLONGO WENU KWA KUDHULUMU WATU. ..

mwisho:
NITOE TANBIHI NYINGINE... UISLAAM NA SHERIA ZAKE HAZINA SHIDA KABISA WALA HAZINA KASORO.. .

NA UKIZIFUATA NA ZIKASIMAMISHWA VIZURI KWA UADILIFU UTAUPENDA NA KUUFURAHIA UISLAAM. .. UTA ENJOY NA KUJIVUNIA KUWA MUISLAAM.

ILA HAWA WAPIGA DILI HAWA NDIO WANAOUCHAFUA UISLAAM...

NIMUOMBE MUFTI.. . BARAZA LAKO UNALOJITAHIDI KULISAFISHA NA KULIRUDISHA KWA UMMA... KUNA WATU WA MASLAHI WANAKUANGUSHA.. . WANALICHAFUA BARAZA KWA TAMAA ZAO ZA MATUMBO... MIJITU IMEJAZA VITAMBI NJAA ZIMEWAJAA HAWANA HOFU YA ALLAH... ADHABU YA ALLAH YAWANGOJA WASIPOTUBU. .. ALLAH AWAONGOZE. ..

NB: MODS TAFADHALI UZI HUU USIFUTWE MUHIMU SANA KWA UMMA...
BAKWATA ipo kisheria kushughulikia masuala ya Kiislam pia ina majukwaa mahsusi ya kuwasilisha na kutatua mikwamo inayowasibu waislam. Kikwazo kuna makundi ya Kiislam yaliyo na maslahi binafsi wameamua kupinga kila jambo lifanywalo na BAKWATA. Mwasilisha mada unapaswa uende ofisi ya BAKWATA iliyo karibu nawe kuwasilisha dukuduku husika
 
BAKWATA ipo kisheria kushughulikia masuala ya Kiislam pia ina majukwaa mahsusi ya kuwasilisha na kutatua mikwamo inayowasibu waislam. Kikwazo kuna makundi ya Kiislam yaliyo na maslahi binafsi wameamua kupinga kila jambo lifanywalo na BAKWATA. Mwasilisha mada unapaswa uende ofisi ya BAKWATA iliyo karibu nawe kuwasilisha dukuduku husika
Fact, ila ahlu jazba wal- balaa hawatokuelewa.
 
Wewe ndiye unaona hana sehemu nyingine ya kulalamikia ila hapa.

Je unauhakika kuwa hao wahusika wapo humu? na kama unauhakika kwa nini asiwa PM ili ujumbe uwafikie.

Nauliza tena kunafaida gani ya yeye kutuambia haya aliyosema, zaidi ya kutufanya kuzidi kuwaona wapigaji?

Hebu soma comments za wadau ujionee.
Hapa ndiyo pazuri hadi sheikh Alhdi wapo wanasoma maoni ya wadau.
 
Wewe ndiye unaona hana sehemu nyingine ya kulalamikia ila hapa.

Je unauhakika kuwa hao wahusika wapo humu? na kama unauhakika kwa nini asiwa PM ili ujumbe uwafikie.

Nauliza tena kunafaida gani ya yeye kutuambia haya aliyosema, zaidi ya kutufanya kuzidi kuwaona wapigaji?

Hebu soma comments za wadau ujionee.
Nidyo, nyie ni wapigaji hivyo muache upigaji. Msiwadhulumu wenzenu.

Uislamu ni mzuri ila nyie ndio mnauchafua

Hapa ni jukwaa sahihi kabisa na lengo la mtoa mada ni kutujuza na kuwaelimisha wanawake kuwa Bakwata Kata hawana mamlaka hivyo waende tu kwa kadhi wa Wilaya na wakiambiwa kuhusu hela wahoji kama hawana wafanyeje!
 
Back
Top Bottom