PostGE2025 BAKWATA wafanya Dua kuiombea Tume ya Matukio ya Oktoba 29

PostGE2025 BAKWATA wafanya Dua kuiombea Tume ya Matukio ya Oktoba 29

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Makumbele

JF-Expert Member
Joined
May 9, 2009
Posts
312
Reaction score
1,433

KATIBU wa Baraza la Ulamaa BAKWATA Taifa, Sheikh Hassan Said Chizenga, ameongoza dua maalumu ya kuiombea Tume ya Matukio ya Oktoba 29, akisisitiza umuhimu wa haki, uwazi na maridhiano katika mchakato mzima kuelekea ripoti ya tume hiyo.

Dua hiyo inalenga kuiombea Tume iweze kutekeleza majukumu yake kwa uadilifu, bila upendeleo na kwa kuzingatia maslahi mapana ya taifa.

Hiyo ni sehemu ya mahojiano maalumu ya Daily News Digital na kiongozi huyo mwandamizi wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA)
 
Hii ndo Tanzania viongozi wa dini wa kivyetu vyetu
 
View attachment 3575598

KATIBU wa Baraza la Ulamaa BAKWATA Taifa, Sheikh Hassan Said Chizenga, ameongoza dua maalumu ya kuiombea Tume ya Matukio ya Oktoba 29, akisisitiza umuhimu wa haki, uwazi na maridhiano katika mchakato mzima kuelekea ripoti ya tume hiyo.

Dua hiyo inalenga kuiombea Tume iweze kutekeleza majukumu yake kwa uadilifu, bila upendeleo na kwa kuzingatia maslahi mapana ya taifa.

Hiyo ni sehemu ya mahojiano maalumu ya Daily News Digital na kiongozi huyo mwandamizi wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA)
Alhamdulillah
20260419_100619.jpg
 
Walikua wapi kufanya hivyo tangu mwaka jana?

Naona hizi siku chache hapa kuna watu wanataka kutumika kulisafisha genge la wauaji na genge la Chande.

Nimeona maaskofu, mufti na lile genge la matapeli wa CHAUMMA wanajitokeza kudai wananchi wana imani na genge la Chande , na hakuna aliyewatuma wala kuwauliza hiyo imani ya wananchi ni wapi ilhali ni miezi zaidi ya 5 watu hawajazika ndugu zao.

Dua/sala inasaidia nini wakati familia hazina miili ya ndugu zao waliowaona wakipigwa risasi na maiti zikaenda kuzikwa kaburi la halaiki?

Mambo ni matatu tu wauaji wanatakiwa kuyafanya ili kuponya mpasuko kwenye nchi, moja ni uitishwe uchaguzi huru upya, miili iletwe watu wakazike ndugu zao , na mwisho waliohusika kuua wawajibishwe kisheria.

Kinyume na hapo hii mbegu itaenda miaka mingi sana na kuna siku tutavuna matunda yake.
 
Back
Top Bottom