Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Wanajukwaa! Mmesikia huko
Naona Bungeni ni patamu sana kila mtu anataka akale utamu wa Bunge
=================
Baraza Kuu la Waislamu nchini Tanzania (BAKWATA) kupitia kwa Naibu Katibu Mkuu wake, Sheikh Mohamed Khamis, wameitaka serikali kupunguza gharama za matibabu pamoja na kuboresha maslahi ya walimu ili kuendelea kukuza nguvu za kiuchumi na kujenga jamii iliyoelimika kuelekea mwaka 2050.
Sheikh Khamis ametoa kauli hiyo Jumatatu, Januari 13, 2025, katika Mkutano wa Kamati ya Dini Mbalimbali Kuhakiki Rasimu ya Dira hiyo, uliofanyika Ukumbi wa TEC, Kurasini, Dar es Salaam, ikiwa ni Kundi la Mwisho kufikiwa na Tume ya Mipango kwaajili ya Mapitio ya rasimu hiyo.
Soma Pia: Kesi ya Kikatiba dhidi ya Serikali na BAKWATA imetajwa leo 26.11.2024, Mahakama Kuu
Sheikh Khamis, amehimiza pia umuhimu wa serikali kusimamia ratiba na mapumziko kwa wanafunzi wa shule za Serikali na za binafsi kama sehemu ya kuhakikisha kuwa kunakuwa na ulinganifu wa masomo na mapumziko kwa wanafunzi.
Bakwata wameiomba serikali kutenga viti vya uwakilishi wa Taasisi za kidini kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama ulivyo uwakilishi mwingine kwenye chombo hicho muhimu cha kutunga sheria.