BAKWATA waiomba serikali kutenga viti vya uwakilishi wa Taasisi za kidini Bungeni

BAKWATA waiomba serikali kutenga viti vya uwakilishi wa Taasisi za kidini Bungeni

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Wanajukwaa! Mmesikia huko

Naona Bungeni ni patamu sana kila mtu anataka akale utamu wa Bunge
=================

Baraza Kuu la Waislamu nchini Tanzania (BAKWATA) kupitia kwa Naibu Katibu Mkuu wake, Sheikh Mohamed Khamis, wameitaka serikali kupunguza gharama za matibabu pamoja na kuboresha maslahi ya walimu ili kuendelea kukuza nguvu za kiuchumi na kujenga jamii iliyoelimika kuelekea mwaka 2050.

Sheikh Khamis ametoa kauli hiyo Jumatatu, Januari 13, 2025, katika Mkutano wa Kamati ya Dini Mbalimbali Kuhakiki Rasimu ya Dira hiyo, uliofanyika Ukumbi wa TEC, Kurasini, Dar es Salaam, ikiwa ni Kundi la Mwisho kufikiwa na Tume ya Mipango kwaajili ya Mapitio ya rasimu hiyo.

Soma Pia: Kesi ya Kikatiba dhidi ya Serikali na BAKWATA imetajwa leo 26.11.2024, Mahakama Kuu


Sheikh Khamis, amehimiza pia umuhimu wa serikali kusimamia ratiba na mapumziko kwa wanafunzi wa shule za Serikali na za binafsi kama sehemu ya kuhakikisha kuwa kunakuwa na ulinganifu wa masomo na mapumziko kwa wanafunzi.

Bakwata wameiomba serikali kutenga viti vya uwakilishi wa Taasisi za kidini kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama ulivyo uwakilishi mwingine kwenye chombo hicho muhimu cha kutunga sheria.

Snapinsta.app_472178713_1115590686801577_3319013233486887963_n_1080.jpg
 
Baraza Kuu la Waislamu nchini Tanzania (BAKWATA) kupitia kwa Naibu Katibu Mkuu wake, Sheikh Mohamed Khamis, wameitaka serikali kupunguza gharama za matibabu pamoja na kuboresha maslahi ya walimu ili kuendelea kukuza nguvu za kiuchumi na kujenga jamii iliyoelimika kuelekea mwaka 2050.

Sheikh Khamis ametoa kauli hiyo Jumatatu, Januari 13, 2025, katika Mkutano wa Kamati ya Dini Mbalimbali Kuhakiki Rasimu ya Dira hiyo, uliofanyika Ukumbi wa TEC, Kurasini, Dar es Salaam, ikiwa ni Kundi la Mwisho kufikiwa na Tume ya
 

Attachments

  • 1728759764686.jpg
    1728759764686.jpg
    154.8 KB · Views: 2
Ya Mungu na ya Kaisari yote wanataka duh! Kwakuwa huko waliko hufanya kazi Kwa kujitolea basi wakienda bungeni iwe ni Kwa kujitolea siyo kudai malipo yoyote kutoka serikalini.
 
Bakwata ni taasisi iliyokwisha feli!

Hawa ndiyo wanafanya waislamu wote tuonekano hamnazo hapa Tanzania.

Kusimamia mali za waislamu mmeshindwa. Kazi majungu, fitina, uchawi, kupiga hela za waislamu na misaada inayotoka nchi za nje.

Wanachosimamia wao ni mwezi tu!
 
Na sisi washabiki wa Simba na Yanga tunataka uwakilishi Bungeni kwasababu sisi tanabeba na kuwakilisha makundi yote nchini kwa mfano;
a) Watoto wadogo mitaani utasikia wana mechi ya Simba na Yanga mitaani kwao!
b) Wafungwa magerezani wana mechi za Simba na Yanga hadi maafande na familia zao qanahudhuria!😁😁😁😁!!
c) Kwenye kambi za jeshi na Polisi Kuna mechi za Simba na Yanga!😄😄😄😄!
d) Mashuleni kwa wanafunzi kuna mechi za Simba na Yanga Kiasi kwamba walimu nao unawakuta wamegawanyika kwa ushabiki wa timu zao! 😂😂😂😂!!
e) Maofisini kuna ushabiki wa Simba na Yanga hadi wakati mwingine unaweza ukaingia benki kutoa ten ukakuta teller ni Ubaya Ubwela mwenzako au Mzee wa Kalkuleta mwenzio akakuongeza ten jengine!🙆🙆🙆🙆!
Hapo sasa sijataja makanisani, misikitini, matambikoni, Bungeni (ahahahahaha Bungeni), Baraza la Mawaziri, nk!!

Kwakweli washabiki wa Simba na Yanga tunastahili kuwa na uwakilishi Bungeni!

Niungeni mkono kwa hili wajameni ili niwe MWAKILISHI WA KWANZA WA SIMBA NA YANGA BUNGENI! 🙏🙏🙏🙏
Naahidi kuwa mwakilishi mzuri wa Simba Sports Club!😎😎😎😎
 
Masheikh wana nongwa
Bakwata ni Taasisi ya kijinga sana!

Nimeona wanaishauri serikali iwazuie vijana na betting.

Hekima ya dini yenyewe inakutaka kama umezuia mlango huu basi onyesha mlango mwengine wa kupitia.

Badala ya wao waishauri serikali iwezeshe kukuza taasisi binafsi ili nazo ziweze kuajiri kwa wingi ili kusaidia kupunguza ukosefu wa ajira.

Ishauri serikali iwezeshe kwenye nyanja nyengine ili vijana waweze kujiajiri na kulitumikia taifa. Wawezeshwe kwa njia rafiki kwenyw kilimo, ufugaji wa wanyama na samaki n.k

Baada ya haya angalau ndiyo utoe na ushauri wa masuala ya betting.

Wao wanakuja tu na tamko, serikali zuieni betting. Hii taasisi ina watu wana akili kweli?

Kama watu wanaficha msaada kama tende zifike kwa waislamu wenzao, yaani tende kitu kidogo tu! Huwa wananishangaza sana!

Ashakum si matusi! Ila hii taasisi ni mavumbi matupu!
 
Bakwata ni Taasisi ya kijinga sana!

Nimeona wanaishauri serikali iwazuie vijana na betting.

Hekima ya dini yenyewe inakutaka kama umezuia mlango huu basi onyesha mlango mwengine wa kupitia.

Badala ya wao waishauri serikali iwezeshe kukuza taasisi binafsi ili nazo ziweze kuajiri kwa wingi ili kusaidia kupunguza ukosefu wa ajira.

Ishauri serikali iwezeshe kwenye nyanja nyengine ili vijana waweze kujiajiri na kulitumikia taifa. Wawezeshwe kwa njia rafiki kwenyw kilimo, ufugaji wa wanyama na samaki n.k

Wao wanakuja tu na tamko, serikali zuieni betting. Hii taasisi ina watu wana akili kweli?

Kama watu wanaficha msaada kama tende zifike kwa waislamu wenzao, yaani tende kitu kidogo tu! Huwa wananishangaza sana!

Ashakum si matusi! Ila hii taasisi ni mavumbi matupu!
Most def
 
Taratibu nchi inakwenda kidini kama Lebanon.

Baada ya ubunge, nafasi ya urais, makamu, waziri mkuu na spika, mkuu wa majeshi nmk zitagawiwa kwa makundi ya kiimani

Mfano nchini Lebanon kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe nyadhifa kuu za serikali kufuatana na makubaliano yaliyotiwa katika katiba, mgawanyo hupewa kama ifuatavyo:

rais lazima awe Mkristo wa dhehebu la Maronite, waziri mkuu Muislamu wa dhehebu la Sunni, na spika wa bunge Muislamu wa dhehebu la Shia.

Huku ugawaji wa viti vya ubunge vilivyopo bungeni ni 128 na unafanywa kwa msingi wa mgawanyo sawa.

Wabunge wa Shia huwa wanampokeo na kusikiliza Iran inawaambia nini, huku wabunge wa Christian Maronite wanapelekwa kwa kufuata itikadi za kanisa la Orthodox linataka mambo gani na huku wale wa Sunni mawazo yao yanamuliwa Riyadh Saudia

Nchini Lebanon jeshini kila dhehebu la imani tofauti linajaribu chini juu kutoa nafasi za ajiri kwa mtu wa mrengo wao wa dhehebu pia serikalini ni hivyo hivyo watumishi hawaajiriwi kwa sifa na weledi bali ni kigogo gani ametia mbinyo watu wake waajiriwe hii imesababisha pia watu kuajiri wengi kuliko inavyotakiwa ili mradi kila dhehebu wafaidike

VIONGOZI WASHINDIKIZA MSIKITI KUJENGWA ENEO LA COCO BEACH

Eneo la kudumu limeendelea kugubikwa na mipango mibovu baada ya jengo la kudumu la msikiti kuanza kujengwa sambamba na vibanda vya mihogo na kilevi.

Hakuna anayekataa watu kuswali, lakini wangeweza kutenga maeneo ambayo sio ya kudumu kama ilivyokuwa awali kuruhusu waislamu au wakristo wanaohitaji huduma hiyo

View attachment 2950662
ENEO LA WAZI LA BURUDANI NA KUPUMZIKA LAMEGWA

December 2024
Dar es Salaam, Tanzania

MASJID TAWHID COCO BEACH DAR ES SALAAM WAZINDULIWA


View: https://m.youtube.com/watch?v=tyQ5IqkrxWk
Hatimaye mradi umekamilika, msikiti wazinduliwa na waumini sasa waanza kuswali.

Hafla ilihudhuriwa na watu mashuhuri wakiwamo waziri wa mambo ya ndani wa Tanzania Eng. Hamad Yussuf Masauni, balozi wa Turkiye nchini Tanzania Dr. Mehmet Güllüoğlu pamoja na viongozi wa madhehebu mbalimbali ya kiislamu

1736798892363.jpeg

1736798925732.jpeg

1736799750355.jpeg



TANGANYIKA PACKERS KAWR DSM

ENEO LA KIWANDA KIKUBWA CHA UMMA CHAGEUZWA ENEO LA KANISA, KAWE TANGANYIKA PACKERS DSM
1736799041615.jpeg

. Kiwanda cha Tanganyika Packers kilijengwa katika kitongoji cha Kawe jijini Dar es Salaam mwaka 1949, na ujenzi wake uliashiria ujio wa viwanda vya kusindika nyama kibiashara nchini. Nyama ya ng'ombe (ya kipekee ilikuwa aina ya corned) ilitumwa ndani na nje ya nchi mbali kama Ulaya.
Picha katika hadithi hii

Katika nusu ya pili ya karne ya 20, kiwanda cha Kawe kilisindika mifugo 550 kwa siku (200,000 kwa mwaka) kwa zamu mbili. Tanganyika Packers Ltd ilitaifishwa mwaka 1974 na kuwa sehemu ya Mamlaka ya Maendeleo ya Mifugo ya serikali. Miaka miwili baadaye ilipoteza cheti chake cha kimataifa cha usafi na mauzo ya nje yalikoma

Ngazi za kupanda hadi ghorofa ya pili ya kiwanda ni hatari sana.​

Ni kama nusu ya hatua, msingi wao wa awali uliondolewa kwa zaidi ya miongo miwili ya uozo. Nilijaribu kuchukua picha kwenda juu - kabla ya karibu kuanguka nyuma chini ya ngazi. Nikaitupia kamera yangu pembeni hadi nilipofika juu. Uamuzi mzuri.
Picha katika hadithi hii

Hatari haina kuacha kwenye ngazi, na unapaswa kuwa makini unapotembea. Kiwanda cha Tanganyika Packers kina urefu wa ghorofa tatu. Kuanzia pili kuna mashimo kila mita tano hadi 10. Sina hakika kazi yao ya asili ilikuwa nini - mifereji ya maji, labda? Katika kichinjio kilichotelekezwa akili yangu inaelea kwenye mambo meusi zaidi.
Leo, mashimo haya ya sakafu ni kamili kwa ajili ya kutunga picha, na aina mbalimbali za vitu vilivyo chini.
Picha katika hadithi hii

Picha katika hadithi hii

Kuhusu kuta, ni jumba la sanaa, na kuna michoro ya rangi na vitambulisho vya grafiti kila mahali. Rangi ni tofauti ya kuwakaribisha kwa wazungu waliofifia na njano
 
Jamani hii sio nchi ya kidini japokuwa serikali inafahamu uwepo wa dini.
Kama Sheikh anataka kuwa Mbunge atafute chama akagombe
 
Maneno gani haya unazungumzia mbele ya Baba askofu tena kwenye ukumbi wa TEC

Zalau kabisa
 
Na walivyokuwa wapuuzi waliyozidi kiwango mfano hai kipindi cha Magu alipokuja mfalme wa Morocco.

Magu kawapigia pande waombe msaada, wao wananyanyuka wanaomba msikiti mpaka Magu aliwashangaa!

Akawaambia nyinyi badala ya kuomba mjengewe taasisi za elimu kama vyuo nyinyi mnaomba mjengewe msikiti?

Mimi mwenyewe muislamu mwenzao nikabaki nimeshangaa! Hapa Dar kuna misikiti mingapi?

Kwenye dini kuna kitu kinaitwa amalin swaaliha! Yaani fanya jambo jema lililostahiki kwa mazingira husika.

Unaweza ukafika mahali ukajenga msikiti, sawa utapata thawabu, lakini lile eneo shida yao si msikiti. Shida yao ni maji! Hivyo unatakiwa ujenge visima vya maji.

Bakwata badala ya kuomba wajengewe mashule n.k wao wanaomba wajengewe msikiti. Hatukatai msikiti, lakini swali hapa Dar kuna misikiti mingapi?

Leo wamekuja wanataka uwakilishi bungeni!!!!!

Kwa heshima ya Mufti kwa vile ni kiongozi wetu wa kiislamu sitaki niizungumze vibaya zaidi. Ila hii taasisi ni 🙌
 
Back
Top Bottom