BAKWATA yaishauri Serikali ifafanue mashaka katika Mkataba wa Uwekezaji wa bandari

Kifungu kipi hakijafafanuliwa?

Mali ya Umma huo umma umeiendesha kwa ufanisi? Mmefanikiwa nini kwenye kuiendesha nyie umma hadi kuifaidisha nchi?
UMMA ni nini ? Na Nchi ni nini ? Nchi sio ya UMMA (Sasa kama kuna kitu hakinufaishi UMMA kinanufaisha vipi Nchi)?!!!!!

UMMA kuwa mmiliki mpaka uendeshe wenyewe au kumpa mtu mmoja monopoly ? UMMA unashindwa kutoa Lease fupi fupi kwa watu tofauti ? Au kuna Bandari ngapi, zote lazima ziende kwa mtu mmoja ?

Hakuna watanzania wenye HATI Miliki kuliko wenzao kama kuna kelele za watu ambao hawajaridhika issue ni kueleweshena na kuongea kwa Hoja na pale ambapo wanasema upande mmoja hapafai kubadilishwa ili pawe sawa...; Ukiwaziba midomo watu hata kama jambo ni zuri kiasi gani na litakupa pesa kiasi gani UFA unaoujenga sasa Gharama zake za Kuuziba haziwezi kuwa equated na Pesa....
 
Sasa wameungana na Catholics ili wasiwe irrelevant
 
Mama kilemba kapokelewa Dubai konyeshwa tabasabu na waarabu wamemtembeza tembeza dubai ..akalainika akawa anachokumbuka nikuanguka sahihi tu.
😂
Na alisaini mikataba mingi sana. Sasa najiuliza kama mkataba mmoja tu ndio uko hivi, je ile mingine ina hali gani? Naomba zoezi la uvujishaji mikataba liwe endelevu. Mikataba yote ya hovyo ingevuja tu, tujue tulivyouzwa 😂😂😂. Kazi kwenu kamati ya kuvujisha mikataba, naamini hamtatuangusha. 😂😂
Tunawaaminia wazee wakuvujisha 😂
 
Kazungumze na Bakwata wenzako!! Sisi wengine tumeupokea ushauri wao kwa mikono miwili.
 
Binafsi sababu jana sikujua wala sikutaka kuuliza unanizuia kesho kama nitataka kujua ?

Nyie ndio wale sababu kulikuwa na Utumwa miaka mingi mgesema Utumwa uendelee yaani Sababu Mwarabu alichukua watumwa hata kesho akija Mmatumbi tumuache sababu Mwarabu alifanya
 
Wapi FaizaFoxy unalolote la kusema
Huyo bint mkongwe atakwambia kwanza hao BAKWATA siyo chombo kinachotambulika na waislam ni koloni la serikali kuwanyonya waislam but wakati huo huo anai-support serikali inayowanyonya kupitia BAKWATA kwenye issue ya DP World kwa sababu hiyo DP ni ya waislam wenzake waarabu.
 
Waziri mkuu kasha fafanua vizuri sana, kumbe hatukujua tulikua tunapotoshwa tu, hu wekazaji ni mzuri kwa bandari zetu.
Upunguani na unafiki, nadhani ni mambo ya hovyo ambayo hakuna binafamu yeyote mwenye utimame angependa yamkumbe.

Pole sana. Yawezekana siyo mapenzi yako kuwa hivyo.

Wenye akili timamu wanajua kuwa Waziri Mkuu hajafafanua hata hoja moja kati ya zile zinazohojiwa.
 
BAKWATA wako Sahihi kutaka kujua maslahi mapana ya nchi...

Mh.Waziri Mkuu amewafafanulia vyema tu....

Tumeelewa ufafanuzi wake....

#SiempreJMT[emoji120]
 
BAKWATA ndilo baraza letu kuu....

Halitunyonyi bali linasimamia maslahi ya kiimani ya waislamu nchini......

Tanzania haijaingia mkataba na DPW kwa sababu ya kidini....kwani hawaji kutangaza dini bali maslahi ya kibiashara na kiuchumi.....

Hivi tunakwenda shule kusomea upumbavu?!!![emoji1787][emoji1787]
 
Hivi ukomo wa huo uwekezaji ni muda gani?
 
Nani akose usingizi?

Endelea kujifurahisha nyuma ya keyboard wakati wenzako wako kazini kuhakikisha nchi inafaidika kiuchumi
Sasa mbona kutwa kucha wako kwenye vipaza sauti wakitoa maelekezo uchwara ambayo watu hawataki kuyasikia. Wewe mwenyewe chawa hulali sembuse hao unaowatumikia!
 
Hivi kuna mtu muongo Tanzania hii kumzidi Majaliwa ambaye alidanganya Magufuli yuko ikulu kumbe mwili wake unapigwa baridi mortuary!
Dah ile ilikuwa kali ila maskini labda na yeye alikuwa hajui chochote kama sisi tu, si hata bwana chalamila alisema ameongea nae kwenye simu eti anawasalimia
 
Kwa niaba ya serikali anakuja Lord denning na Faizafoxy kutoa ufafanuzi!!
 

Mpaka sasa hawajafafanua chochote ni polojo ndio maana maswali bado yapo ,wmkuu wanajadili faida ,faida zinajulikana tatizo mambo ya mkataba ndio wamekwepa kufafanua vifungu vyenye utata mfano je dubai ni nchi adimfanye naye IGA
 
Sasa mbona kutwa kucha wako kwenye vipaza sauti wakitoa maelekezo uchwara ambayo watu hawataki kuyasikia. Wewe mwenyewe chawa hulali sembuse hao unaowatumikia!
Wanafanya kama sehemu ya demokrasia tu na wala haimaanishi kuwa wanakosa usingizi.
 
Mpaka sasa hawajafafanua chochote ni polojo ndio maana maswali bado yapo ,wmkuu wanajadili faida ,faida zinajulikana tatizo mambo ya mkataba ndio wamekwepa kufafanua vifungu vyenye utata mfano je dubai ni nchi adimfanye naye IGA
Umesoma hata Katiba ya Nchi za Falme ya Kiarabu?

Kwa mujibu wa Katiba ya United Arab Emirates nchi zinazounda umoja huo zinaweza kuingia mikataba na nchi nyingine. Muwe mnasoma wajinga nyie
 
Wewe chawa hamna ambaye hakujui muda mwengine mtulize akili sio kushabikia kila jambo la CCM tu alimradi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…