Balile: Kwa miaka sita mfululizo Tanzania ilikuwa na anguko la uhuru wa vyombo vya habari mpaka Rais Samia ulipolidhibiti

Jiwe aliinajisi Sana nchi hii. Hata kama bei ya unga itakuwa sh elfu 60 kwa kilo kamwe siwezi kumkumbuka jiwe.
Si akikubutua kisha akakutelekeza! Sasa utamkumbuka vipi?
 
Kwa nini media zote hazikutangaza wala kuandika habari za watanzania walioandamana huko Marekani kudai katiba mpya, uhuru uko wapi anaousema huyo kibaraka?
 
Balile huwa ni msema ukweli..

Ila sasa uhuru wa vyombo vya habari usitumike kufanya upotoshayna upuuzi mwingine Kwa kisingizio cha uhuru wa vyombo vya habari.
 
Kweli, japo Balile nakumbuka kipindi cha mwendazake alikuwa akimsifia pia, na hakuwahi kukosoa ukandamizaji ule

Kajubi Mwakajanga wa MCT kidogo alikuwa vocal
Wala msimlaumu kwa aina ya mwendo ule ilikuwa ni lazima tuu afanye vile, nawasifu sana ambao mliosimama na msimamo wa kukosoa wazi wazi mnastahili tuzo kwa kweli hahah!
 
Hii kauli ya huyu Balile naona imekuja mapema sana, vyema asubiri zoezi la kumpara Samia lianze tulione mpaka mwisho wake, inawezekana hali ya mambo ikarudi ile ile ya miaka sita iliyopita.
 
Wacha ukweli usemwe tu
 
Hii kauli ya huyu Balile naona imekuja mapema sana, vyema asubiri zoezi la kumpara Samia lianze tulione mpaka mwisho wake, inawezekana hali ya mambo ikarudi ile ile ya miaka sita iliyopita.
Kwa sasa inatosha kusema inatia matumaini. Tusubiri hapo baadae.
 
Sasa huyo Balile mbona anajoifanya haelewi Kiswahili, mama "kadhibiti" au au kaondoa udhibiti uliowekwa na Magufuli, mama karuhusu siyo "kadhibiti". Aache lugha za kijinga, awe mkweli na muwazi tu, asiwe kama panya kuuma na kupuliza.
🤣🤣🤣Kadhibiti hali ya anguko.
 
Huyu jamaa ni mjinga sana. Hakumbuki sifa alizokuwa anampa Magufuli na serikali yake!! Waliompa uenyekiti nao ni wajinga tu!! (Ujinga siyo tusi. Ni hali ya kutokujua jambo. Nyerere aliwahi kufafanua). Sasa kazitoa kwa marehemu, kazileta kwa Samia! Samia naye ajiandae siku akitoka.
 
Uko ndani ya mzinga kiroboto twambie Toka muwe huru nini mmefanya kwa taifa zaidi ya kuwa part of the game
 
Jiwe aliinajisi Sana nchi hii. Hata kama bei ya unga itakuwa sh elfu 60 kwa kilo kamwe siwezi kumkumbuka jiwe.
Ukiona ivo ujue unaishi kwa wazazi wako au ni KIROBOTO unaenyonya mikojo
 
Nakumbuka alivyokuwa anamsifu Magufuri kuwa kila tarifa waliyokuwa wanaitoa serikali ya Magufuri ilikuwa ikiifanyia kazi,tena alitoa mfano wa jinsi walivuliwa wanaiba mafuta bandarini kupitia metal, kuhusu madawa ya kurevya, alisema kitu ambacho utawala wa hawamu ya 4 kilikuwa akifanyiki.Huyu jamaa hovyo kabisa ana msimamo bora mala mia Jeneral Ulimwengu alimkosoa Magu pasipo kujificha na Magu akumgusa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…