Balile: Magufuli katutenda, deni la nje lafikia shilingi Trillion 78

Transparency. Serikali zinakopa lakini mkopo sio top secret au confidential. Mjadala wa wazi wa bajeti unaoisumbua Marekani (USA) leo unahusu viwango vya kodi na deni la taifa ili kupata pesa ya kuitimiza bajeti inayopendekezwa na serikali ya Democrats. Inaitwa FISCAL RESPONSIBILITY.

Kopa lakini weka uwazi. Watu waelewe unachofanya kuhusu maendeleo yao. Ukiwaambia sisi ni matajiri sana hatuhitaji pesa za mabeberu you’re not being honest. Kuna watanzania wengi walioamini tunatumia HELA TULIZO NAZO (hela ya ndani) kutekeleza miradi mikubwa tofauti na enzi za kina JK na Mkapa.

Waliposikia awamu ya sita imepokea pesa za IMF wameanza kumlilia Magufuli kuwa enzi za kujitegemea alizoanzisha zimekufa! Sasa tunategemea mabeberu! Hiyo ni mass deception. Kwa faida gani? Deni liwe wazi wananchi wajue mzigo wanaobebeshwa na value for money ikoje.
 
Endelea kufundisha wanafiki wakuangalia upepo unavumaje. "sitanii"

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Njaa inamsumbua, hawa ndo wanato sifa zisizo na tija,
Wasubili hata miaka ifike mitatu ndo wasifie,
Hizo ni teuzi wanata tu hakuna kingine.

Wangejua kwa sas huku mtaani palivyo pagumu, unashinda kwenye biashara huoni mnunuzi na watu ndo wameachwa na pesa zao lakini shida tupu.

Kinachofata ni watu kufilisika bila kunyanganywa mali yako.
 
Wandishi wetu wengi ni wanafiki sana. Atakuwa anawinda cheo cha Msigwa huyo. Anachokisema sasa kilishazungumziwa hapa JF.

Ukubwa wa deni la serikali na mikopo kutoka benk za kibiashara vyote vilizungumziwa hapa.

JPM alikuwa ana agenda yake ambayo kwa bahati mbaya imeshindwa kufanikiwa. Hizo propaganda zilizokuwa zikiendelea kipindi kile zilikuwa calculated. Akina Kabudi, Polepole na Bashiru hawakuwekwa pale kwa bahati. Ukiangalia their past ndiyo utajua kwa nini waliwekwa pale......!!
 
Mbele ya mazuzu yule ni raisi bora sababu aliruhusu kila mtu aibe kwa nafasi yake na kuzorotesha judiciary organ of the government ikageuka channel ya kuipiga hela serikali!

Hata huyu mama atapendwa sababu sio mfuatiliaji kabisa! Watu wanajipigia pesa kwa kwenda mbele na mavikao na seminars all cameras off!!!
Ndo maana alipoenda nchi za ulaya wakamuuliza kwa nini nchi yako licha ya kuwa na rasilimali nyingi ni masikini akajibu hata mimi sijui! Huoni huyo alikuwa Rais Mpumbavu sana!
 
Viongozi wengi ni Madokta wasomi, wasaidie kuondoa Changa moto mbali mbali ikiwemo hizo ulizozitaja Mtoa mada .

sasahivi kuna uwazi mfano ukienda website ya Dart wataonyesha hatua waliyofikia Dart phase 2 na wanasema wameshapokea ela ya mkopo wa kujenga phase 3 na phase 4 . Mradi ukisuasua anajulikana nani aulizwe.
 
Nina mpango wa kuandamana na mikwaju mikubwa na mirefu kwenda chato kulichapa kaburi la jambazi aliyepewa heshima asiyostahili
 
Naona mbinu zimewaishia mnaanza kuhangaika na marehemu. Yeye ndo aliwashauri mkusanye tozo nje ya kodi ambazo tayari zimelipwa? yeye ndo kawashauri mfanye anasa kwenye matumizi ya serikali kwa kutumia magari ya kifahari na kuzunguka na misafara kana kwamba mnaongoza dunia? we can't buy this..........pambaneni tu na hali zenu, kama vipi mnasepa tu mapema mnaachia wenye uwezo na vipaji vya kuongoza.
 
Jamaa wana mimba za chuki kweli na zinawasumbua mpaka watakapojifungua! Ina maana kudharau uwanja wa Chato ni kana kwamba Chato yote na Geita kuna maskini wa pesa ambao hawawezi kupanda ndege?
 
Kwa taarifa yako hizo unazoambiwa ni fedha za kujenga madarasa kutokana na tozo ndio rejesho la vaccine ya Uviko19 na usitegemee eti ipo siku serikali itakuwa na transparency kwa kila jambo. Bora hata JPM alisema fedha zetu za ndani na kimantiki alikuwa sahihi kama unakopa kujenga then unalipa from inner source hizo fedha ni zako baada ya kukamilisha mkopo (na ndio maana deni huwa lako) hizo ni tofauti na msaada wa mashimo ya vyoo. Kinadharia anaweza kuwa hakuwa sahihi na hilo ni swala binafsi na pia ki protocol... Kitu ambacho unakishangilia sasa ni mama kukopa fedha za Uviko then hakwambii nani atazilipa na kutoka chanzo gani?.

Angalia kupanda kwa bidhaa za petrol angalia Chuma angalia ushuru wa imported products kuanzia mafuta ya kula mpaka utaelewa tu.
 
Jamaa anahisi wenye pesa ya kupanda ndege wanapatikana Dar tu. Uwanja wa ndege ni mradi utakaonufaisha umma! Watu wakiweza kula flight moja kwa moja toka chato mpaka duniani huko ni achievement kubwa sana!
Wewe unatabia ya kuona watu wa Chato na Geita hawana hela ya kupanda ndege! Nakujulisha tu huko vijana wanapesa kuliko hata huko uliko! Tembea chi hii ni kubwa usikariri maisha!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…