Balile: Mzee Butiku aache uwoga atutajie majina ya Wauwaji wa Kibao aone kama hatutachapisha, aache kututukana Waandishi!

Balile mbona unatuanzishia! tulipokee? Utakimbia. Tukio la Ijumaa na Jumamosi vyombo vingi vya habari vilijificha ndani ya magamba yao kama kobe! Vingine mpaka sasa vimeogopa kuandika alivyosema Butiku na hata JF nayo imo mkumboni, mnaandika zaidi upande wa upinzani ila upande wa teuzi mnajichekeshachekesha na ati, ati wanasema nyiingi.
Balile hata wanapoonewa wenzenu mnajificha kuwatetea, mfano tukio la Mbeya, mliufyata mkia kama mbwakoko wa kijijini.
 
Mzee Butiku hakupepesa macho amesema wazi anawafahamu waandishi wanolipwa zile hundi zile.

Pia amewashauri waandishi wasipende kutafuniwa wachangamshe bongo zao.
 
Balile KAPANIKI...Mzee Butiku Mungu akubariki mmebaki wachache wengine bado wamepiga Kufuli kwenye hili baya kabisa kwenye Taswira ya Taifa
Balile aache kutumia misuli badala ya Ubongo. Mzee Butiku alichokisema kuhusu uoga na uchawa wa waandishi na Vyombo vikubwa vya Habari kuwa too much close to the Government Leaders is what also the General Public perceive about our main stream media . Hata hili lilijidhihirisha zaidi wakati wa Sakata la DP na uamuzi wa Vyombo vyote vya Habari kuamua kukaa kimya na kukwepa kuchapisha hata Waraka wa TEC waliokuwa wameutoa kupinga kuuzwa kwa Bandari zetu. Balile hawezi kujivua hizi lawama la udhaifu wa Vyombo vyetu vya Habari badala ya kuwa watetezi wa wananchi wanakuwa wa kwanza kujikomba kwa Viongozi na serikali. Ukweli unauma na Mzee Butiku amepiga kwenye Mshono katika hili. Balile anakumbuka Cartoon maarufu zilizokuwa zinachorwa kwenye Magazeti makubwa ya Kenya kipindi cha Serikali ya Awamu ya 4 wakionyesha namna Waandishi wa Habari na wahariri wa Vyombo vya TZ Wakiwa wanabrush Viatu vya Mh Rasi Kikwete, na hapa walikuwa wanaonyesha ni kiasi gani vyombo vya Habari vya TZ visivyokuwa Muhimili wa 4 tena, bali kuwa tu wasifiaji na chawa wa Viongozi wakuu . Mzee Butiku Viva na Pongezi kwa kuwa mmebakia wachache wenye mioyo na uzalendo kama wewe. Umma wa wa Tanzania unatambua mchango wako , Moani yasiyoyumbishwa na utetezi wako wa mambo yenye maslahi kwa Taifa na ukemeaji wa mambo yasiyostahili kama haya yanayoendelea katika Taifa Letu. Usikae Kimya , maana the Hottest Spot in Hell is always Deserved for Those who choose to remain Silent During Times of Crisis ! .
 
NLIKUWA NAAMBIWA BALILE NI KILAZA LAKINI SIKUJUA KWA KIWANGO HIKI.
Sijui hii Kofia ya Uwenyekiti wa Jukwaa alilipata vipi, maana jamaa huyu Balile hata ukimsikia katika mazungumzo yake kujadili mada huwa ni mweupe na mwepesi kabisa. Mimi nilivyokuwa nasikia jina Balile nilidhani ni bonge la Muandishi mwenye uwezo wa kuchambua na kutoa nondo, lakini baada ya kuwa nimemsikia tangu wakati huo nlimushusha. Aaache wenye weledi na uzelndo na nchi hii wakosoe uongozi yeye kama hawrezi kwa maslahi ya tumbo lake let him shut up. Mzee Butiku is beyond his level na kumbe ndio maana hata katika hili hawezi kumuelewa. Tumsamehe Bure Bwana Balile ni uwezo wake mdogo tu hawezi kumuelewa Mzee wetu. Natamani Generation ya Waandishi ya Calibre ya akina Jenerali Ulimwengu and the Likes.
 

Natafuta namba ya Balile au kama anatumia mtandao wowote. Nimshauri. Miaka hii watu hawana maadili kabisa na hata akili hawana. Yaani Balile wa kumjibu Mzee Bujiku kweli?
 
Sahihi
 
Wengi ni wauza unga tupu
 
Balile hana ubavu wa kuchapisha majina ya wauaji hata akipewa.

Balile kwa sasa aliisha cease kuwa mwandishi wa habari objectively ni mwandishi tumbo. Alipekekwa Dubai na DP World aliporudi akaanza kuandika makala za kuwasifia ili watanganyika turidhike bandari zetu kuchukuliwa na waarabu

Mtu yeyote muelewa na mzalendo hawezi kumsikiliza Balile..
 
NLIKUWA NAAMBIWA BALILE NI KILAZA LAKINI SIKUJUA KWA KIWANGO HIki

Body frame yake na kiwango cha Yellow matter na wrinkes kwenye Ubongo wake haviwiani. Kiasi kikubwa kimepotelea kwenye kupanua mwili badala ya ubongo
 

Acheni kutafuta vichaka. Kamateni watekaji.
 
Kama darasa la saba alimwelewa vizuri Mzee Butiku, yeye mtaalamu wa habari ameshindwaje kumwelewa? Hiyo nafasi alipata kwa hisani ya "kimemo"? Anawaaibisha Waandishi wenzake.
 
mzee butiku aliposema anawajua anamaanisha chadomo msikilize vizur
 
Wewe ulimwelewa Mzee?
nadhani balile alimuelewa zaidi, lakini pia wanahabari wengine walimuelewa sana na ndiyo maana waliokua wakijaribu kumchallenge kwa maswali mawili matatu nae akioanekana kupanic kidogo...

kwan ulitaka kusemaje gentleman kwa faida ya wadau?
 
Mzee Butiku kasema ukweli - waandishi baadhi wananunuliwa pamoja na vyombo vyao vinatumika kuandika propaganda za kutunga. Tuliona kuanzia Bandari, Loliondo nk

Mzee yupo sahihi kuhusu tasnia ya habari TZ - mjirekebishe.
 
Balile KAPANIKI...Mzee Butiku Mungu akubariki mmebaki wachache wengine bado wamepiga Kufuli kwenye hili baya kabisa kwenye Taswira ya Taifa
Katika uovu ambao umefanywa na unafanywa na uongozi wa serikali ya CCM ni kipi ambacho Mzee Butiku amewahi kukemea?

Nyerere aliwahi kusema CCM siyo mama yangu na kama ikikiuka misingi ya kuanzishwa kwake atahama, hii kauli hakuna wazee waliobakia CCM wachumia tumbo mwenye uwezo wa kutamka.

Balile yuko sawa kama kijana aliyechoma picha ya rais alihukumiwa jela na sasa hajulikani yako wapi unataka Balile akapime maji ya mto kwa chelewa? Butiku kama wazee wengine wa CCM mnafiki tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…