Tetesi: Balozi Dkt. Wilbroad Slaa afichua siri mpya ya mikakati ya Mbowe kushinda uenyekiti. Apewa mapesa zaidi na Rais Samia na M/kiti CCM kummaliza Lissu

Sasa hivi Fitna namba moja Tanzania ni Slaa.
 
Hivi huyu Padri kwan alieudi lini CDM!?
Ameshikilia liferaft,survival tactics.
Serikali ilishamstaafisha Ubalozi,pili ikamnyanganya title ya kuitwa Ambassador.
Roman Catholic Church nao kama yupo nje ya ulingo.
Serikali ya Mama Samia imeishampika teke.
Kwanini nae asitafute njia ya kutafuta angalau mkate wa kila siku?
 
Siasa ngumu na haileweki. Siamini huyu ndiye Slaa aliyesema Lissu amejipiga risasi alipopewa ubalozi na Magufuli.
 
Kama taarifa ya Slaa ni kweli, naona damu itamwagika siku ya uchaguzi wao. Na msajili ameishaandaliwa kukifuta Chadema.
 
Dr apewe maua yake, huyu mzee ni muhimu sana kwenye taifa hili
 
Hatuna uhakika kama kapewa. Ila ikiwa ni kweli ametoa hiyo 12B kwa mtu mmoja, je Zanzibar kapeleka bilioni ngapi ?
Si unaona Zanzibar ilivyopiga hatua kubwa ya maendeleo katika miaka mitatu hii shule za msingi za gorofa hadi vijijini halafu mambwiga ya CCM yanataka kumpa mitano tena. Kodi za Watanganyika ndiyo zinaijenga Zanzibar.
 


Siasa za kidemokrasia katika nchi za Demokrasia ni dhahiri wananchi wanajigawa katika pande mbili .Upande wa giza na upande wa nuru yaani Wema na ubaya .

Kwa sasa wetu wanamtaka Lisu ili siasa za Tanzania zihame kutoka kwenye siasa za upande wa wapigaji tu na anayeonekana kinyume na ufisadi anauawa au kushughulikiwa kisasa. Hii imejenga taifa la watu waovu na uovu unaonekana ndio dili. Rushwa imekua ni kama fasheni kwenye nchi hii. Watu wanaofanya biashara halali wanadharaulika ,watu wanaosema na kukemea ufisadi wanaitwa wabangaizaji . Yaani tumerudi zama za giza za kutukuza mali na kudharau haki na hekima . Mtu mwenye pesa hata akitema pumba kama Mbowe anaonekana ana busara .

Mbowe amesababisha mauaji na ulemavu wa watu wengi sana hapa Tanzania lakini hajawahi kusemwa serikali wala kukamatwa kwa tuhuma za kusababisha mauaji isipokuwa ni wakati wa JPM tu ndio alihukumiwa na kupigwa faini kwa kusababisha mauaji ya Akwiline . Familia ya Akwelini ilitakiwa ufungue Kesi ya madai dhidi ya Mbowe baada ya hukumu kuonyesha kuwa Mbowe na wenzake walisababisha kifo cha Akwiline.


Mbowe kama anafikiria kuwa damu za wenzake ndio mtaji wake basi akimlazimisha ushindi wa Rushwa ndio mwisho na anguko la Chama chake na SACCOs yake .kwani Atakua alepoteza watu wengi na hivyo kupoteza Ruzuku kubwa .
 
Wajumbe ni wa hovyo.....Mchana wanamkubali Mbowe mwenye mabilioni ila kura kwa Lissu


Na tuwaambie tu wajumbe kuwa wasimuogope Mbowe maana akishindwa ndio basi anapoteza mvuto kabisa lakini wakimuonea huruma wajue uchaguzi mkuu watapata shida sana kunadi sera zao kwa wananchi
 

Uongo mbaya mmezidiwa kweli kweli
 

Hizo pesa zingeweza kusaidia bima ya afya kwa watoto, wazee, wakinamama wajawazito.
 
Mbowe, usitumie cheo Kama dhamana ya matakwa yako, utasababisha ajali Kama ya MV BUKOBA
 
Hii vita ni ngumu mno, tunaomkubali Lissu na haya yanayoendelea yanaleta mashaka.

Lissu akifanikiwa kuivuka hii vita itakuwa historia, upinzani ni mkubwa sana.

Hii ni vita ya Lissu na serikali!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…