Tetesi: Balozi Dkt. Wilbroad Slaa afichua siri mpya ya mikakati ya Mbowe kushinda uenyekiti. Apewa mapesa zaidi na Rais Samia na M/kiti CCM kummaliza Lissu

Tetesi: Balozi Dkt. Wilbroad Slaa afichua siri mpya ya mikakati ya Mbowe kushinda uenyekiti. Apewa mapesa zaidi na Rais Samia na M/kiti CCM kummaliza Lissu

Halafu tujadili hoja yake maana kama mtanzania na CHADEMA kina maslahi ya watanzania huna haki ya kumnyang'anya haki yake ya kujadili siasa za Tanzania.

Kwa hiyo hivyo vigezo vyako vinampoka haki yake? Akuamua kurudi CHADEMA una haki ya kumzuia?
Great mind discusses ideas
Simple mind discuss events and foolish mind discusses people.
Mna vigeugeu sana nyie watu aisee
 
Siyo msukuma wamachame mlikuwa mnaifanya CHADEMA SACCOS yenu, tuonyeshe hayo matusi.

Wapuuzi nyie wakati anakuwa endorsed 2020 alikuwa hajakuwa kichaa na mropokaji? Uropokaji ameanza kwa kutaka kugombea uenyekiti wa CHADEMA?
Vichaa nyie
Wapalestina(wamachame) wamechafukwa kweli kweli .
 
Alipolamba ubalozi hakusema kahongwa.

Alipolipiwa Serena hakusema chochote.

Dr Slaa alishaondoka CDM sijui anawashwa na nini.

Nilisema na nitasema tena na tena Lissu hana wapiga kura.

Lissu ana wadhabiki Club House ambao si wapiga kura.

Lissu kaingizwa chaka,atuliea keshapotea katika ulingo wa siasa.
Kila jambo na wakati wake...

Unajuaje labda alishatengeneza na Mungu wake..?

Pesa zitaliwa na Freeman Mbowe hatakuwa Mwenyekiti nawaambia...

Hizi harakati za kumsaidia huyu jamaa (Mbowe) na kuhakikisha Tundu Lissu hapati uenyekiti hazina tofauti na alivyofanyiwa mwaka 2017 wakati anagombea u - Rais wa TLS...

Aidha hazina tofauti na alivyofanyiwa Boniface Mwabukusi kwrnye uchaguzi wa Rais wa TLS mwaka jana 2024...

Hao TISS, Polisi, na UVCCM chini ya mtu wao kwa jina la Nkuba waliweza kumzuia Boniface Mwabukusi asishinde? Waliweza kumzuia Tundu Lissu asishinde mwaka 2017...?

Kwenye chaguzi ndogo za watu wachache kama hawa wasiozidi wajumbe 2,000 CCM hawawezi kuingiza fitina wala mbinu zao na zikafanikiwa...!!

Wamwage tu hayo wapesa, tutayachukua na hawatapata wanachokitafuta maana MUNGU WA MBINGUNI AMESHAWAKATAA...!!
 
Ukimsikiliza kwa makini anasema Rushwa haina ushahidi ila yeye ni kuchafua watu na kila mtu kwa hoja kwamba amehongwa bila ushahidi wala mazingira yenye mashaka sana...

Chafua kila mtu kwa kutumiwa msg... Dah .. Birds of a feather

TL anaweza vip kuendesha chama kwa kuchafua kila mtu?

Hizi siasa chafu CDM hawa ndio waanzilishi wake, Rushwa na Ufisadi wa uwongo uwongo.... Tabia chafu sana mwanaume kumchafua mwanaume mwenzako kutaka madaraka....

Mnafiki na Mzandiki... Babu mzima hovyo
Nimecheka kwa nguvu vibaya, eti siasa chafu cdm ndio waanzilishi, kwanza una umri gani? Kuelekea uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi hapa nchini wa 1995, makada wa ccm na Nyerere akiwa hai, walikuwa wanazunguka mitaani wakionyesha video za vita ya mauaji ya kimbari ya Rwanda, wakisema mkichagua wapinzani wataleta mauaji kama hayo. Sasa endelea na upotoshaji wako mwingine kwenye waasisi hao wa siasa chafu hapa nchini.
 
Kwani Huyo Slaa amerudi CHADEMA? au ameahidiwa kuwa atarudi, mtu ukiachwa basi achika
Slaaa hata hasiporudi chadema lakini tambua chadema ni mali ya Umma ndo maana wanapewa ruzuku ambayo ni kodi ya wananchi wote wenye vyama na wasio na vyama ni kodi zao ana haki chadema sio mali ya Mbowe Kenge maji
 

View: https://youtu.be/lU_QbyAtMUM?si=Qdt19WOd_IGi962F

Duuh, mimi sikuwahi kufikiri wala kudhani kabisa kuwa kamanda wa anga na mwanaharakati wa siasa za mageuzi Tanganyika ndugu Freeman Mbowe kuwa ni shetani wa CCM - kijani aliyejificha kwenye gwanda la khaki la CHADEMA...!!

Katika VideoAudio Clip hiyo, Balozi Dr. Wilbroad Slaa aliyewahi kuwa katibu mkuu wa CHADEMA kwa miaka 12 (2003 - 2015) na kufanya kazi chini ya uenyekiti wa Freeman Mbowe anafichua siri ya vikao kati ya Freeman Mbowe na Mwenyekiti wa CCM (Taifa) ambaye pia ni Rais wa JMT Bi. Samia Suluhu Hassan...

Dr Wilbroad Slaa anasema, amepewa taarifa na vijana wake ndani ya Idara ya Usalama wa Taifa (TISS) juu ya kikao kati Rais Samia/CCM na Freeman Mbowe kujadili namna atakavyosaidiwa kushinda uenyekiti...

Anaendelea kusema kuwa, Rais Samia amekubali kumuongezea pesa Freeman Mbowe ili kugharamia mikakati ya ushindi wake na kwa hiyo wajumbe wajiandae kula pesa za bure za Samia Suluhu Hassan...

Aidha ameitahadharisha kambi ya Tundu Lissu kufahamu kuwa, Freeman Mbowe atapata msaada toka TISS, polisi na UVCCM wengi wataingia kama wajumbe wapiga kura na watavalishwa magwanda au jezi rasmi za CHADEMA...

Je, wajumbe 1,200 watashindwa kufahamiana na kudhibitiana ndani ya ukumbi? Timu Tundu Lissu fahamuni hili, jiandaeni kwa mapambano. Fanyeni kama TLS walivyofanya kumpigani Boniface Mwabukusi na kuibuka mshindi wa u - Rais wa TLS...

This is crap!
 
Back
Top Bottom