Balozi Hussein Katanga msaidie Rais ipasavyo, teuzi za Wakuu wa Wilaya kuna dosari kubwa

PhD

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2009
Posts
4,692
Reaction score
3,891
Mhe. Balozi Hussein Katanga, Katibu Mkuu Kiongozi, nakuomba na kukusihi sana msaidie ipasavyo Mhe. Rais kutekeleza majukumu yake. Nimefuatilia teuzi za U DC kuna dosari kubwa.

Kuna uwezekano makundi fulani yenye maslahi yanapenyeza ajenda zao katika teuzi hizo na yanakushinda nguvu wewe kama Mkuu wa Utumishi wa Umma.

Mambo ya teuzi za ovyo yalianza zama za mwendazake na sasa mama naye kaanza kuyarudia japo teuzi zake za mwanza zilionyesha matumaini.

Nakusihi sana KMK, msaidie Mhe. Rais teuzi zifanyike kulinda hadhi ya ofisi husika. Vinginevyo hadhi ya Mamlaka ya Uteuzi na Ofisi inashuka.
 
Dosari ni zipi toa ushahidi
 
kwahiyo msipoteuliwa kunaonekana dosari
 
Wakuu wa wilaya na mikoa ni vyeo ambavyo havina umuhimu wowote! Na hizi teuzi za miaka hii ndio imezidi kudhihirika ni vyeo vya ovyo! Labda ndio maana wanateuliwa watu wa 'hovyo'!
 
Rais hajakosea, hivyo vyeo vipo kwa ajili ya kuliwazana wote wanaoipenda CCM na kujipendekeza huko, ni vyeo vya zawadi kwa wote walio na uhusiano na CCM, hili limekuwa likifanyika miaka yote na watangulizi wote wa Samia, tatizo naloliona hapa watu walitaka Samia ateue wanaowapenda wao, na awaache wasiowapenda, hili ndio tatizo.
 
Wanateua watu ambao jamii inajua kuwa walinunuliwa, Watu waliosaliti vyama vyao kwa fedha, wanawaacha watu ambao ni wasafi ndani ya CCM na nje ya CCM.

Uteuzi huu wa akina Nassari na Lijualikali ni wa ajabu sana!

How can you reward a sellout behaviour?
 
Onyesha hizo dosari basi tuzione.
 
Balozi katanga amekuwa Japan muda mrefu, alikuwa anamfahamu Joshua nasari kuwa alifukuzwa ubunge na spika wa CCM na sasa CCM inamteua kuwa DC kupitia CCM? Ninashauri Katiba mpya ipatikane,Rais anayejua tangu mwezi March 2021 Hadi sasa ni July hajamaliza kuteua,Bado maDED Bado madas mwaka unaisha anayejua tu hakuna kazi nyingine. Katibu mpya DC na Rc wachaguliwe na wananchi wa maeneo husika. Badala ya wilaya kuletea mtu wasiye mtujua tena kwa maslahi ya chama Fulani.
 
Siku tukakaa vyeo hivi vya Ukuu wa Wilaya na Mikoa basi tutakuwa tumepiga hatua kubwa sana Katika kukomesha matumizi yasiyo ya lazima na Mzigo kwa serikali yetu. Hivi vyeo plus wabunge wa Viti maalum na wale wa Kuteuliwa na Mzigo usiona ulazima kwa taifa masikini kama letu.
 
Vipi ? Ulivyotaka wewe ndivyo sivyo?
 
Ulitaka ateuliwe shangazi yako ?!!
Acheni mama afanye kazi, hao walioteuliwa Ni watanzania , na isitoshe atakaeenda kinyume mama atampiga tu chini na kuteua mwingine
 
Tuna Nongwa sana Watanzania, hakuna jema litakalofanywa tukashukuru! Mama kateua aliowateua, tunaona kakosea, kwani wale ni wanyarwanda na sio Watanzania wenzetu!? Ulitaka uteuliwe wewe na ukoo wako!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…