Balozi Hussein Katanga msaidie Rais ipasavyo, teuzi za Wakuu wa Wilaya kuna dosari kubwa

Balozi Hussein Katanga msaidie Rais ipasavyo, teuzi za Wakuu wa Wilaya kuna dosari kubwa

Wakuu wa wilaya na mikoa ni vyeo ambavyo havina umuhimu wowote! Na hizi teuzi za miaka hii ndio imezidi kudhihirika ni vyeo vya ovyo! Labda ndio maana wanateuliwa watu wa 'hovyo'!
hahaahhh - mkuu mbona ulishaahidiwa kupewa mojawapo ya nafasi hizo kama jamaa yule angeshinda 2015 na ukaanza shona suti
 
Wanateua watu ambao jamii inajua kuwa walinunuliwa, Watu waliosaliti vyama vyao kwa fedha, wanawaacha watu ambao ni wasafi ndani ya CCM na nje ya CCM.

Uteuzi huu wa akina Nassari na Lijualikali ni wa ajabu sana!

How can you reward a sellout behaviour?
Weka ushahidi wa kununuliwa
 
Rais hajakosea, hivyo vyeo vipo kwa ajili ya kuliwazana wote wanaoipenda CCM na kujipendekeza huko, ni vyeo vya zawadi kwa wote walio na uhusiano na CCM, hili limekuwa likifanyika miaka yote na watangulizi wote wa Samia, tatizo naloliona hapa watu walitaka Samia ateue wanaowapenda wao, na awaache wasiowapenda, hili ndio tatizo.
Lileta ada linasema Ujinga huu ulianzia kwa mwendazake!
 
Balozi katanga amekuwa Japan muda mrefu, alikuwa anamfahamu Joshua nasari kuwa alifukuzwa ubunge na spika wa CCM na sasa CCM inamteua kuwa DC kupitia CCM? Ninashauri Katiba mpya ipatikane,Rais anayejua tangu mwezi March 2021 Hadi sasa ni July hajamaliza kuteua,Bado maDED Bado madas mwaka unaisha anayejua tu hakuna kazi nyingine. Katibu mpya DC na Rc wachaguliwe na wananchi wa maeneo husika. Badala ya wilaya kuletea mtu wasiye mtujua tena kwa maslahi ya chama Fulani.
Kazi ya Rais wa JMT kwa asilimia 90 ni KUTEUA na KUTENGUA.

Jiwe mpaka kafa ANATEUA na KUTENGUA.
 
Hata mimi nimehisi hizi teuzi zina mkono wa lile genge.
Kuna kaujinga kanafanyika chini kwa chini bila mama kujua.
Lakini tulishauri awafutilie magenge mbali kwani wao hawatamkubali kamwe hata awafanyie nini.
 
Hata mimi nimehisi hizi teuzi zina mkono wa lile genge.
Kuna kaujinga kanafanyika chini kwa chini bila mama kujua.
Lakini tulishauri awafutilie magenge mbali kwani wao hawatamkubali kamwe hata awafanyie nini.
👍
 
Kwa mtazamo wangu hao maDC na RC hawahitajiki ni matumizi mabaya ya pesa ya umma wamekuwa kama wenyeviti wa CCM wa maeneo hayo maana ni lazima wawe wafia chama. Hawana umuhimu sababu tayari wenyeviti wa CCM wapo katika maeneo hayo. Tuokoe matumizi haya mabaya ya pesa. Kama tunahitaji wachaguliwe na wananchi au zianishwe Sifa za kuwa DC au RC kwakuwa hiyo ni ajira katika ofisi ya umma. Hivi ilivyo hakuna haja ya kuwa nao ndiyo wanaochangia kukwamisha tusipata maendeleo maana kila kitu kwao kimekuwa ni siasa tu.
 
Usimdanganye rais, Umma ukimkataa atapata tabu sana.

Sasa ndiyo nini kwenda kuteua watovu wa nidhamu waliofukuzwa bungeni kama akina Nassari?
Kuna mashabiki na kuna umma. Tutofautishe viwili hivi.

Mama anafanya kazi kwa maslahi ya Umma sio maslahi ya mashabiki
 
Wakuu wa wilaya na mikoa ni vyeo ambavyo havina umuhimu wowote! Na hizi teuzi za miaka hii ndio imezidi kudhihirika ni vyeo vya ovyo! Labda ndio maana wanateuliwa watu wa 'hovyo'!
Tuorodheshee majukumu ya hao viongozi tuone kma hayana umuhimu
 
Back
Top Bottom