Habari za Zanzibar
JF-Expert Member
- Dec 18, 2024
- 651
- 433
BALOZI MTEULE WA UJERUMANI AWASILISHA NAKALA ZA HATI ZA UTAMBULISHO KWA WAZIRI KOMBO
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Mahmoud Thabit Kombo (Mb.), amepokea nakala za Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani nchini Tanzania, Mhe. Annett Günther.
Baada ya kuwasilisha nakala za hati hizo, Mhe. Kombo na Balozi Mteule Günther wamefanya mazungumzo yaliyolenga kuimarisha zaidi uhusiano wa muda mrefu na ushirikiano kati ya Tanzania na Ujerumani katika maeneo yenye maslahi ya pamoja.
Katika mazungumzo hayo, viongozi hao wamejadili umuhimu wa kuendelea kuimarisha ushirikiano katika sekta mbalimbali, ikiwemo biashara na uwekezaji, maendeleo, elimu, afya, nishati, mazingira na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.
Aidha, Mhe. Kombo amemkaribisha Balozi Mteule Günther nchini Tanzania na kumtakia mafanikio katika utekelezaji wa majukumu yake ya kidiplomasia, huku akisisitiza utayari wa Serikali ya Tanzania kuendelea kushirikiana na Ujerumani katika kuendeleza maslahi ya pamoja ya nchi hizo mbili.
Kwa upande wake, Balozi Mteule Günther ameeleza utayari wake wa kufanya kazi kwa karibu na Serikali ya Tanzania katika kuendeleza na kuimarisha zaidi uhusiano na ushirikiano uliopo kati ya Tanzania na Ujerumani.