EMT,
Nianze na suala la uchanga wa taifa; Bandiko hili linalenga zaidi kuchokoza mada based on mjadala wako kwenye bandiko namba 73;
Nikianza na suala la
uchanga wa taifa, hoja zangu katika hili zinatokana zaidi na kutatizwa kwangu na tabia ya watanzania wengi kuchanganya dhana mbili kama vile ni kitu kimoja – dhana ya
‘state' and ‘government'; Nilijadili dhana hizi kwa undani kwenye uzi mwingine ufuatao
https://www.jamiiforums.com/great-t...wa-rais-kikwete-mjadala-wa-nadharia-tete.html
Tukirudi kwenye mada husika, iwapo tutakuwa tutaangalia Tanzania kama nchi iliyokuwa chini ya ‘S
overeign GOVERNMENT' for the past 52 years, then hoja kwamba Tanzania sio Taifa Changa, ni hoja yenye mashiko; Lakini tukiamua kujadili Tanzania ‘A
s a STATE', mtazamo wangu ni kwamba we are still very young; Mifano ya Kenya, Rwanda n.k, hasa juu ya jinsi gani wamepiga hatua katika kipindi cha miaka 50 bado hakibadili ukweli kwamba
as states, nchi hizi bado zipo very vulnerable and things may reverse at any time - hakuna guarantee of sustenance; Kenya, Rwanda, Tanzania, zote ni
problematic states, one step away from being
failed states; Suala la Tanzania
being a problematic state pia nilishajadili kwa kirefu katika uzi mwingine huko nyuma;
Nikirejea sehemu ya mjadala wangu huo nilisema kwamba - Kwa upande mmoja – A Government (Serikali) ni taasisi ambayo jukumu lake kubwa ni kutunga na kutekeleza sheria na sera mbalimbali ndani ya jamii husika; Muhimu pia ni kwamba taasisi hii ina nguvu na mamlaka ya kutawala eneo husika la kijiografia pamoja na wakazi wanaoishi eneo hilo; Mamlaka na nguvu hii imegawanyika katika maeneo makuu matatu:
Legislative (Bunge) – nguvu ya kutunga sheria na sera mbalimbali;
Executive – nguvu ya kurututisha utiifu wa sheria (enforce law);
Judiciary (Mahakama) – nguvu ya kufafanua au kuanisha Sheria mbali mbali ili kuongoza shughuli za kila siku katika uendeshaji wa serikali - kisiasa, kiuchumi na kijamii;
Kwa upande mwingine, nilijadili kwamba maana ya ‘State' ni ‘a geographic entity' ambayo ina fiscal system yake mahususi, ina Katiba Yake na Soveregnity (freedom from external control);
Katika haya mawili (
state vis a vis government), we certainly have an aged government but the story is different when it comes to Tanzania as a state;
Ili nieleweke vizuri zaidi natokea wapi na wasiwasi wangu kuhusu hoja kwamba Tanzania sio Taifa changa, pengine niulize swali lifuatalo: Je, kwa miaka 52 iliyopita (tangia uhuru wa kisiasa), Tanzania imekuwa ikifanya kitu gani kinachofanania na
State Building? Kwani bila ya uangalifu, tutaendelea kupuuza juu ya umuhimu wa kurudia juhudi za state building, hasa strengthening of formal and civic institutions za kuendesha maisha ya kisiasa, kijamii na kiuchunmi; Hivi sasa, informal and community based institutions ndio zinaendesha nchi, huku formal and civic institutions zilizopo zikitumika tu kama rubber stamps; Iwapo kuna mtu anaweza ku-point kwamba tumekuwa katika harakati za state building kwa mifano hai, basi hivyo ndivyo tutaweza kupata hoja zenye mashiko kwamba sisi sio wachanga kwani when it comes to this and that,
we have mileage;
Vinginevyo naendelea kuamini kwamba we have hardy done much to build Tanzania as a State, instead, we have been busy forming new governments for the past 50 years; State building efforts zilifanyika katika kipindi kidogo sana na zikafa (1967 – early 1980s); it is in this light that I am strongly convinced kwamba as
a STATE, Tanzania bado ni wachanga sana (not necessarily experience in forming governments for political leadership and administration purposes)';
The following table might help nieleweke zaidi:
| Mwaka | Main Feature | Main Objective |
| 1961 – 1966 | Party State (TANU) | To establish order |
| 1967 – 1985 | Developmental State (TANU/CCM) | Progress |
| 1985 – Present | Contracting State | Control |
Kufuatana na the table above, - baada ya uhuru, the ultimate objective ya mwalimu na TANU was to create and sustain a new order; Ingawa Mwalimu was optimistic about the future, he had no experience of exercising power; He was anxious to secure his own position at the helm of the "
inherited colonial state', thus the rise of TANU (later CCM) as the Party State;
In 1967 throughout 1985, Mwalimu's objective shifted from ORDER to DEVELOPMENT; he (and TANU) realized that he had to show wananchi that he and TANU) had abilities to develop the country; it is in this context that Nyerere developed an interest in grabbing control of the State for the purpose of guiding progress – kwahiyo hapa the
party state was replaced by th
e Developmental State;
From 1985 to the present – hapa we see the World Bank and IMF taking over; Serikali imeondolewa katika suala zima la State building, na suala hilo kuachia nguvu za soko, huku serikali ikifanya facilitation and to a smaller extent, regulation; The bottom line ni kwamba throughout this period, our
government have become increasingly dependent on policy advice and funding for economic reforms from external sources;
Ukitazama kwa ukaribu vipindi hivi vitatu, as a STATE, Tanzania is still in its infancy stage kwani katika miaka 52 ya uhuru, ni kwa miaka 18 tu (1967 – 1985) ambapo we had home grown policies and vision; For the remainder of the period, some other forces have been in control;
Kwahiyo hoja zangu za msingi juu ya kwanini sikubali moja kwa moja kwamba sisi sio wachanga kama Taifa ni based on arguments kuu mbili hapo juu – kwanza ni dhana ya problematic state, pili ni mjadala wangu kuhusu evolution yetu kama Taifa kutokea party state – to developmental state to contracting state; Na hoja nyingine ya kuongezea hapa ni kwamba – bado tunaishi under the first generation of leaders, and I believe kwamba it is also an important variable or unit of analysis katika kubaini uchanga au ukomavu wetu kama Taifa;
Hoja zako kuhusu parliamentary form of government vis a vis presidential form of government nakubaliana nazo kimsingi, ila nina machache ya kuchangia nikipata muda baadae;
Cc:
JingalaFalsafa,
Nguruvi3,
Raia Fulani,
jouneGwalu,
Bongolander,
Kichuguu,
Ogah,
Mkandara,
Mzee Mwanakijiji