Balozi Sefue, Madaraka ya Rais na Katiba Mpya: Je, Tunaelewa hoja yake ya msingi?

Asante Mkuu wangu Mchambuzi kwa kunielewa.
UCHANGA wa Taifa! Tunapozungumza Uchanga moja kwa moja tunagusa Ukomavu. Je, vigezo gani vitumike? Binafsi naona hivi viwili;-
1. Uwezo wa Taifa Kujiendesha lenyewe! Uchanga ni utepetepe, kama ni mtoto hawezi hata kukaa chini mwenyewe. Ukomavu ni KUJIMUDU, kama ni mtoto ni yule anayeweza kukaa ama kusimama mwenyewe pasi kushikiliwa! Sasa sisi kama Taifa, kipi tunaweza kujidai nacho kuwa tunajimudu nacho? Je, ni siasa zetu hizi za kusikiliza mzungu anatakaje? Ama Uchumi wetu huu wa kuamuliwa na mzungu? (copy and paste style) Hata tamaduni zetu wenyewe hatuwezi kuzifanya zisimame, TUMEKOMAA NINI? Je, sisi si kama mtoto amtegemeae mamaye kumkalisha ama kumsimamisha?
2. Uzoefu: Hapa tunaweza kupima uchanga ama ukomavu wa Taifa kwa kuangalia Umri! "Ukiona nyani mzee ujue amekwepa mishale mingi". Miaka 50 si haba kuitwa mkomavu! Maana ndaniye, kama Taifa tume-experience mengi mno...njaa, magonjwa, na hata vita, sera na mifumo tofauti tofauti, itikadi mbalimbali, imani, sayansi na teknolojia n.k...vyote tumevishuhudia! Je, yatosha kusema TUMEKOMAA kwakuwa tu UMRI WETU umeruhusu kushuhudia MAMBO MENGI? Binafsi ninahofu kigezo hicho, kwani inaweza tokea ya mfyatua tofali la udongo, anayesubiri wiki moja kwenda kunyanyua tofali kujengea, kumbe kuna mwenye HILA naye ambaye tangu siku ya kwanza amekuwa akilimwagia maji tofali lisikauke hadi siku ya saba. Ole kwa mnyanyua tofali, akidhani limekomaa na kulinyanyua kwa pupa kwakuwa tu limeshafikisha wiki, LITAMPASUKIA MIKONO na kubaki mdomo wazi! Na hiyo ndio Tanzania. "UKOMAVU WA TAIFA UTAPIMWA NA FIKRA ZA WATU WAKE KATIKA KUAMUA NAMNA BORA YA KULI-TREAT TAIFA LAO WENYEWE, KULINGANA NA MAZINGIRA NA NYAKATI ZAO WENYEWE" tukifikia hapo, ni sahihi kusema tumekomaa!
*Mkuu wangu Mchambuzi, nimefurahi sana kueleweka kuhusu Demokrasia na anguko lake. Inquality, poverty, ethnic, religious polarization, fragmentation, e.t.c kama vyanzo vya anguko la Demokrasia...vyote hivyo vinadhihirisha "IRRELEVANCE OF DEMOCRACY" katika mataifa yetu Afrika! Mfumo usiosadifu jinsi tulivyo utatufikisha wapi? Mfano wa kutosadifu kwa huu upuuzi, INQUALITY haikuanza leo, tangu ukoloni. Tunajua kwamba yapo maeneo ambyo yalipata huduma za kijamii mapema sana, mfano shule na hospitali. Lakini yapo maeneo pia ambayo yalipata kujua shule na hospitali miaka 10-20 baada ya uhuru. Leo demokrasia inataka watu hao wawili tofauti, wa-be treated sawa! Kama ni fursa ya ajira washindanishwe, biashara, uongozi, kula, kuvaa na kulala kwao kuwekwe kwenye sahani moja wajinyakulie. Tumesahau kuwa kipindi A anaenda shule B alikuwa shambani analima ama udongoni amejilaza na maumivu ya kichwa! No Consideration, na watu wanakenua meno. Itaachaje kuzua machafuko?
Hapa umenena maneno mazito sana mkuu wangu, katika nchi changa, "Wanasiasa wanatafuta kuungwa mkono by exploiting nationalism and unity exaggreting internal threats kwa umma" cha kusikitisha zaidi system imewaruhusu kufanya hayo kwa madai ya uhuru wa kuropoka! TUNAENDA WAPI NDUGU ZANGU? Hakika hilo linadhihirisha uchanga wetu. Maana katika ukomavu wa taifa kinachopimwa ni FIKRA za watu wake sio umri! Kama wenyenchi wenyewe wanashindwa kutofautisha kujenga na kubomoa nchi, kipi kilichokomaa kwao? Labda tuite UCHANGA ULIOKOMAA.
Katiba Mpya na matumaini ya watanzania hii ni HATARI lakini salama, maana wengi wataamka na kujua thamani yako katika maendeleo yetu. Niliwahi kusema hivi, katiba ni maafikiano yanayorasimisha SERA juu ya mfumo fulani kutoka Falsafa/Itikadi fulani. Mifumo iliyopo leo imeoza na ndiyo hiyo ifungayo zoezi la kupata katiba mpya. Hakuna misingi mikuu ya kulijenga taifa, ndio maana tunahitaji "REFORMATION OF STATE, OUR OWN STATE" Mkuu Mchambuzi ulishanena hili, leo limerudi tena, hapo ndipo napoichukia JF maana litapita tena. Upi uwe mwisho wa kelele hizi tupigazo?
Mungu wetu yu tayari kutushindia vitani.
Anaita sasa!
 
Mchambuzi
Napenda kukubaliana nawe katika hoja hizi kutokana na unyambulishaji wako katika post zilizotangulia. Nina shaka pia. Kabla ya kuja mkoloni tulikuwa na nini kabla ya Taifa? Historia nimeisahau kidogo, ila nakumbuka kuwa kulikuwa na himaya (Empire) kadhaa katika Afrika hii. Tutofautishe Empire na State? Ninaamini kuwa jamii tofauti ndani ya eneo ambalo lilikuja kuitwa Tanganyika na mkoloni zilikuwa na mifumo yao ya kiutawala na kiuchumi. Kutaja chache kina Mangi Meli, Mangi Mareale, Chifu Mkwawa, Chifu Rumanyika, Mtemi isike, na himaya nyingi kadhaa ambazo zilikuwa zinajijenga na kujitanua kiutawala na kiuchumi kwa njia za vita na zinginezo. Binafsi naamini kuwa state formation zilianza hata kabla ya mkoloni. Mkoloni alipoingia akavuruga state zilizokuwa na kutengeneza za kwake kwa lengo la kurahisisha kutawala. Kwanza walichofanya ni kuwagawa wananchi waliokuwa katika state fulani na ndio maana tunashuhudia leo wamakonde Msumbiji na Tanzania. Wamasai Kenya na Tanzania. Wajaluo kenya na Tanzania. Wahaya Uganda, Rwanda na Tanzania. Hili unalizungumziaje Mchambuzi
 
Last edited by a moderator:
Sina uhakika na muelekeo wa mjadala, ndio maana toka awali sikutaka sana kuzama kwenye hili suala la uchanga au ukubwa wa taifa letu....

Kitu pekee kinachonikera katika mjadala wa uchanga na udogo wa taifa letu ni kuwa mara zote umetumiwa na watawala wetu katika kukwepa majukumu, kuhalalisha uzembe wao na kuwachagulia wenyenchi nini ni sahihi kwao kwamba watu wenyewe hawajui nini kinawastahili.

Suala la uchanga (kwa maana toka tulipokuwa huru) halina mashiko tena, sababu kuna mifano ya nchi ambazo zimepata uhuru mbele yetu na kugubikwa na migogogro kedeked ila bado leo hii yameweza kuwa ni mataifa ya maana sana.
Pia kwa kurejea mfano wa EMT kuna nchi hadi miaka ya mwisho ya 60 tulikuwa tunalingana nayo kiuchumi na nyingine kuzizidi ila leo kwenye ulimwengu uliotamalaki usasa na teknolojia ya kurahisisha kila kitu wametuzidi sana .....

Kwa mifano hii ni rahisi sana kuiua hiyo hoja ya uchanga wa taifa, sababu je kama taifa tungeendelea na ile speed ya miaka ya 70 kabla ya vita ya Uganda (naweka pembeni suala la vita baridi ya mataifa makubwa), kweli leo hii tungeendelea kulia lia na uchanga wa taifa??

Hivyo suala la uchanga ni la kuliweka pembeni sababu linatoa mjumuisho wa vitu tu, twende kwenye masuala mahususi na ya moja kwa moja kwamba ni nini kinachopelekea tujione wachanga leo hii??

Sawa kama hayo tunayoyaita "mataifa makubwa" yamepitia zaidi ya miaka 200 toka uhuru wake, je na sisi tunahitaji miaka 200 kweli ili tuje kujiita taifa kubwa, kweli??

Nadhani hapo utaona kuwa suala la ukubwa wa taifa sio miaka mingapi au vizazi vingapi vimepita ila ni kujielewa kama taifa dira yenu kuwa mnataka kujenga taifa la namna gani na kuamua kuanza kujenga hilo taifa kwa kuanzia misingi na mifumo ya kuachiana vizazi na vizazi ili kukamilisha hilo taifa mnalolitaka, hichi ndio kitu ambacho hakipo au hata kama kipo basi hakieleweki mpaka sasa kwenye nchi hii....

Ila tu kwa kurejea kwenye mjadala halisi, kwa mambo na kasi ya dunia ni ngumu sana kupona kama tutaendelea na kumrundika kazi kubwa zote Rais.
Ni lazima tugawanye uongozi na mamlaka yake kwenye mamlaka nyingine na kuziunda tusihofie kuumia kutokana na huo "uchanga" labda maumivu yatazaa ukomavu kama nchi na kusonga zaidi.

Turudi kwenye maswali manne uliyouliza, nadhani nitarejea!
 
Last edited by a moderator:
Raia Fulani in relation to bandiko namba 82:

Asante kwa kuendeleza mjadala huu muhimu, hasa kuhusiana na suala zima la State and Our Society in Tanzania vis a vis Government. Kama nilivyokwisha jadili huko nyuma, A STATE huzaliwa kutokana na mahitaji ya makundi mbalimbali ndani ya jamii husika, na kwa kawaida mahitaji hayo huwa na mahusiano na masuala makuu matatu: Kwanza ni suala la Usalama wa jamii husika na mali zao; Pili ni suala la Ustawi wa maisha ya wanajamii husika; na Tatu ni suala la kutatua the constant conflicting demand on scarce resources – yani the common economic problem of Scarcity - unlimited wants versus limited resources available to meet such wants; Hilo ni moja;

Pili, a State pamoja na taasisi zake is supposed to act rational na wenye nafasi za utumishi katika state husika wanatofautiana na wanajamii wengine kwa maana moja kubwa kwamba – watumishi hawa wana mamlaka ya kufanya kazi ya kuongoza na kusimamia masuala yote ya msingi katika jamii – kisiasa, kiuchumi na kijamii, sasa whether mamlaka hayo yanatokana na matakwa ya wanajamii au yanatokana na matumizi ya mabavu, hili ni suala linalo relate na moja ya hoja zangu za msingi katika mjadala huu – yani uwepo wa problematic state in Tanzania.

Katika historia ya ulimwengu, STATES zimekuwa zikitofautiana sana, hasa machimbuko yake, na kuna wanazuoni kadhaa ambao wamejadili hili kwa kina kwa mfano Marx, Webber, na Durkheim. Kwa ufupi, Marx anaelezea state kama matokeo ya class relations; Webber anaeleza kwamba ni matokeo ya organization (kwa kutumia dhana za domination, power and authority), na Durkheim kwamba ni matokeo ya division of labor ndani ya jamii husika. Tutawajadili mitazamo yao kwa kina baadae iwapo itabidi, hasa to relate na mazingira yetu Tanzania kabla ya ukoloni na baada ya ukoloni.

Vinginevyo STATES za awali (the world all over) zilianza kama rudimentary states – hasa kama tu mwendelezo/extension ya household ya mfalme au chifu. Kama ulivyojadili hapo juu, ni kweli kwamba kabla ya uhuru, Tanganyika (baadae Tanzania) kulikuwepo na tawala za kichifu zenye mifumo yake ya uchumi, siasa na utawala lakini hakuna jamii hata moja ya kabla ua ukoloni ambayo ina fit well na theory za Webber, Marx na Durkheim. Tukiachana na hilo, jamii za kichifu kama tunavyoelewa kupitia historia zilikuja kuharibiwa na wakoloni katika kipindi ambacho jamii hizi zilikuwa zinaimarika zaidi na pengine kukaribia kiwango kinachoelezwa na wanazuoni hao hapo juu. Na baada ya uhuru, sisi wenyewe kupitia Mwalimu Nyerere tukaamua kufutilia mbali utawala wa kichifu, ingawa ilikuwa kama ni self contradictory kwani kwa upande mwingine, Ujamaa ulilenga kurudisha values zote ambazo ziliharibiwa na ujio wa ukoloni.

Matokeo yake ni muendelezo wa a problematic state kama nilivyojadili huko nyuma ambapo kwa upande mmoja, kuna STATE yenye a few formal institutions (hasa civic institutions) zenye kuunganisha wananchi in a collective way, lakini kwa upande mwingine, kuna informal and community based institutions ambazo zinapingana na dhana ya uraia (collectivity approach of state formation) unaojengwa na civic and formal institutions ambazo kimsingi zinaendesha shughuli zake kwa mtindo wa communities za makabila haya, dini ile n.k. Mbaya zaidi ni kwamba kwa ujumla wake, watanzania wengi wapo more loyal to these informal institutions kuliko civic institutions. Pengine hii inachangiwa na ukweli kwamba Nyerere hakuwekeza juhudi katika kugeuza watanzania kuwa Raia kwanza mara tu baada ya uhuru lakini huu ni mjadala mwingine.

Hata viongozi wetu wengi wapo more loyal to informal and community based institutions kwani hizo ndio zinawazaa kama wabunge, madiwani, marais n.k. Civic institutions zinakuja kukamilisha tu mchakato wa informal institutions. Na kibaya hapa pia ni kwamba Civic institutions zimegeuzwa kuwa sehemu ya viongozi kuchota mali na kuipeleka kwenye community zao ambako kuna more loyalty. Huu ni mwendelezo wa imani kubwa ya wananchi wengi kwamba kama vile ilivyokuwa serikali ya kikoloni (kuwa alien to common man), serikali baada ya uhuru nayo ni ya aina hiyo, haipo kwa faida ya wengi, kwahiyo dawa ni kuchagua viongozi makini waende huko Dar-es-salaam kukamata madaraka kasha wakwapue state property kuja kutuendeleza kimiradi na kimfuko pia.

Such antagonism inachangia sana uwepo wa a problematic state in Tanzania na since independence tumekuwa na a state ambayo ni weak, soft and fragile kama nilivyojadili awali. Ni kutokana na hali hii, baada ya uhuru Mwalimu aliamua kugeuza former colonial state kuwa a party state, lakini miaka sita baadae, akaona haifai, hivyo azimio la arusha na ujamaa vikazaa a developmental state, ambayo haikuweza ku deliver sustainably, hivyo ikauwawa na kupisha a contracting state ambayo ndio tunayo sasa kwa miaka 28 (tangia mwaka 1985), na such a state imeshindwa kabisa to deliver the goods to the common man. The STATE is now on the verge of becoming a failed state politically and democratically, kwani tayari economically (on the micro level which matters more than macro level), Tanzania is already a failed state.
 
jouneGwalu ,

nashukuru sana kwa mchango wako namba 83; naelewa hoja yako ya msingi juu ya madhara ya kujitambulisha sisi kama taifa changa, lakini nakubaliana zaidi na wewe kuhusu jinsi gani watawala wanatumia hii kama loophole kukwepa majukumu yao. Lakini pamoja na hayo, suala la Tanzania kuwa taifa changa (a young state) lipo pale pale na sina uhakika kama umepitia hoja zangu zinazojadili kwanini nimekuwa na mtazamo huo. Pia jingalafalsafa ameuliza zwali la msingi sana kwenye bandiko namba 81 kwamba kama taifa, tumekomaa nini? Natarajia kusikia mawazo yako juu ya hili.

Vinginevyo nakubaliana na wewe kwamba kuna umuhimu wa kumpunguzia madaraka rais, ingawa kuna maeneo mengine nadhani sio lazima yapunguzwe bali yadhibitiwe ipasavyo.

Mwisho nikushukuru kwa kutambua maswali yangu manne katika bandiko namba moja sehemu ya hitimisho, wengi wamekuwa wakiyakwepa maswali haya, hivyo kupelekea mjadala mara nyingine kukosa dira. Nitashukuru iwapo utarejea na kujadili maswali husika.

Zakumi, tunakukosa huku, pole na mafua.

EMT, nguruvi3, raia fulani, bongolander, kichuguu, ningependa kusikia mawazo yenu kuhusu swali la mwenzetu jingalafalsa kwenye bandiko namba 81 anapohoji kwamba:

Je, Tanzania kama Taifa tumekomaa nini?
 
JouneGwalu #83, nakubaliana nawe kabisa kuwa neno uchanga linatumika kama kitisho na ukweli kuwa hapa tulipo hatuna uchanga tena. Kwanza sisahihi kusema sisi ni wachanga baada ya kujitawala miaka 50.

Nchi kama Marekani ilikuwa changa katika miaka 50 kwasababu haikuwa na template ya kukomaa.
Sisi tumepata uhuru mwaka 1961 kukiwa na model na template zote mezani, hatuna sababu ya kutembea wakati wenzetu wanakimbia.

Lakini pia tujiulize ni uchanga upi? mwaka 1961 nchi za Asian Tiger ikiwemo China zote zilionekana third world pengine kwa uchanga wake. Leo nchi hizo hazipo kundi moja na sisi. Je, wenzetu waliwezaje kuvunja uchanga miaka 50 na sisi tusubiri miaka 200 kama USA?

Mchambuzi, nakubaliana nawe kuhusu formal institution na informal and community based institution.
Ni kweli kuwa sisi tupo zaidi katika informa and community base institution.
Sababu za sisi kuwa loyal ni matokeo ya wananchi kukataa tamaa na civic institutions.

Mahali popote ambapo pana weak civic institutions jamii hutafuta mbadala uwe wa heri au wa shari.
Hiyo ndio natural justice inavyo dictate.

Ni kwa muktadha huo hapa tulipo tunapaswa kwanza kuimarisha forma institutions na hapo ndipo unapoungana nani na Raia Fulani tunaposema ili ku-shift mtazamo wa wananchi kutoka katika community based then tuanze na marekebisho hapo.

Nimesoma maoni ya viongozi katika tume ya katiba mpya. Hakuna hata mmoja aliyeridhika kuwa kuna uhuru wa institutions anayoongoza katika utendaji, ubunifu na uongozi kwa ujumla.

Jana Gavana wa BOT amezungumza kidiplomasia sana kwa kusema BoT inaingiliwa katika utendaji na serikali na hapa ana maana Rais kwasababu katika serikali hakuna anyeweza kumwingilia Gavana kama si rais peke yake. Ameomba BoT ipewe nguvu za kikatiba.

Ni maoni kama hayo yametolewa na CAG, Tume ya uchaguzi, wastaafu viongozi n.k.
Hii maana yake ni kuwa uongozi wa nchi haupo katika institutions bali kwa mtu mmoja.

Sasa Gavana anayeangalia uchumi wa nchi kama anadhani hawawezi kutenda kwasababu ya kufungwa mikono, kwanini tudhani kuwa tukisubiri miaka 200 tutakuwa tumekomaa.

Hakuna mtoto anayekomaa akiwa amebebwa asiyepewa fursa ya kutambaa au kutemebea hata kama kuna nyakati atakuwa katika matatizo. Ukomavu ni kitu comprehensive ambacho kina both side, negative na positive.
Kinachoangaliwa ni jinsi gani ya ku-overcome challenges zitokanazo.

Ni kwa msingi huo ndio maana nasema rais apunguziwe madaraka ili uongozi wa nchi uwe katika istitutions zilizo huru.
Ukiangalia hoja za kwanini rais asipunguziwe madaraka, nyingi zimezama katika usalama na stability ya nchi.
Ninachouliza ni kuwa mbona kun-abuse ya nguvu hizo na bado hakuna security concern?
 

Kwanza kabisa nakubali tatizo la kuchanganya kati ya state na government. Kuna mpaka watawala walioko madarakani wanaamini kuwa the current government is "sovereign". Wamekaa madarakani kwa muda mrefu kiasi cha kuwafanya kuamini hivyo. Wameachana na dhana kuwa ipo siku serikali hiyo itaondoka madarakani na kuiachia serikali nyingine. Ni "sovereign state" aka "state sovereignty" na siyo government sovereignty. In addition, hata maana ya state sovereignty imebadilika sana in the contemporary world.


Kwa hoja kama hii unaweza pia kusema kuwa Afghanistan is a very young state kwa kuwa bado ni vulnerable, guarantee ya substance ni ndogo, ni problematic state and it can actually be said that is already a failed state?

The government there can't physically control its territory, has no, or only a limited, monopoly on the legitimate use of force, cannot adopt and enforce decisions binding for the whole country, is unable to provide basic public services, and cannot represent the whole country in the international community. That state is a failed or failing one regardless of how young or old it is.


Naweza kukubaliana na wewe, lakini I believe hivyo ulivyoodhoresha sivyo tuu vinavyotumika ku-determine a legitimate government. At the end of the day and particularly in the contemporary world, suala kubwa ni kuwa na legitimate government. A government can have a legislature, judiciary and executive lakini kama haina legitimacy kutoka kwa wananchi then haitakuwa na effective control of the State.


I think a state is more than a geographic entity. Kwa mfano, tukija kwenye State recognition under international law, nilishaandika sehemu nyingine in the context of Zanzibar kuwa any territory can recognise itself as a State under its own internal laws. But self-recognition does not mean that such territory has achieved a Statehood under international law.

At the end of the day, it is not what a territory thinks it is, but what other States think it is. Kwa mfamo, Somaliland inajitambua kama State, but other States do not recognise it as such. Other countries regard Tanzania as a state.


Accordingly, a territory must satisfy the criteria set by international law in order to be recognised as a State. These criteria are for State recognition; not recognition of governments. Criteria for state recognition under international law.


  1. A permanent population. There must be some people to establish the existence of a State but there is no a specification of a minimum number of people and again there is no a requirement that all of the people be national of the state.
  2. Territory. The second qualification is territory where the permanent population live on. However, there is no a necessity of having well- established boundaries as the international Court of Justice said in the North Sea Continental Shelf cases, "... there is... no rule that the land frontiers of a state must be fully delimited and defined". The well-known example is the uncertainty of the land frontiers of Israel when it was admitted as a State.
  3. Government. A State requires a government that functions as a political body within the law of the land. But it is not a condition precedent for recognition as an independent State.
  4. Capacity to enter into international relations with other states. The fourth and last qualification is about independence. In other words independence is indicated by the criterion of capacity to enter into international relations with other states.

Hapo unaweza kusema kuwa Tanzania haina hizo criteria ili kutambuliwa as a State?

State building ina theory mbili na sijui unamaanisha ipi. Theory ya kwanza ni kwamba state building ni shughuli inayofanywa na external actors wakijaribu kujenga au kuimarisha taasisi ambazo ni dhaifu kwa sababu ya vita or failing state. Mifano inaweza kuwa Afghanistan na Iraq.

Theory ya pili ambayo imepata umaarufu mwaka 2007 baada ya kusainiwa kwa mkataba baina ya nchi zinazotoa misaada kwenye nchi ambazo zimeathirika na vita au weak States. Katika mkataba huo nchi zilizoendelea zilikubali kuunga mkono state building as their "central objective" in conflict affected countries.

Of course the second theory can be criticised because state building may also be viewed as an indigenous, national process driven by state-society relations. The endogenous view believes that countries cannot do state-building outside their own borders.

But I believe that state-building takes place in all countries and at all times. Hadi leo Marekani pamoja na utajiri wao they still build their state. Kwa hiyo, sidhani kama state building inaweza kuchukuliwa as an excuse to ku-justify uchanga au maendeleo duni ya taifa.


You may be right, because on other hand, kuna tofauti kati ya state building na nation building. Nation-building (nation referring to the population itself, as united by identity history, culture and language) is defined as the process of encouraging a sense of national identity within a given group of people. This a definition relates more to socialisation than state capacity.

The basis of the two concepts is different. The term nation emphasises the consciousness of unity whilst the state emphasises political unity. So, a state may lack the feeling of oneness among its people and yet remain a state.

Sasa tangia kupata uhuru Tanzania ilikuwa inafanya state building or nation building? What Mwalimu Nyerere was trying to do? Building a state or a nation?


I beg to differ with you on this. As I said above, a problematic state does not make that state a young state. Vinginevyo tutakuwa tunatumia uchanga huo ku-justify matatizo yanayotukabili kama taifa. Inabidi ifike mahali tukubali kuwa tumeshakomaa vya kutosha kutatua matatizo yanayotukabili. Tuache kutumia excuse ya uchanga to try to justify our level of development.

Nitakupa mfano hai. Singapore ilipata uhuru mwaka 1965. Sisi tulipata uhuru mwaka 1961. Lakini Singapore has experienced exceptionally rapid growth, low inflation, and a healthy balance of payments. Kwa nini Singapore wameweza lakini sisi tumeshindwa pamoja na kwamba wao ni "wachanga" zaidi yetu?
 


Ngoja niingize mtazamo wa kihistoria kuhusu madaraka makubwa ya rais. Madaraka makubwa ya rais sio wazo lilotokana na watanzania au waafrika.

Kihistoria, viongozi wa Urusi na China walijilimbikizia madaraka makubwa ambayo waliyatumia katika mapinduzi ya viwanda na mabadiliko ya kijamii.

Mabadiliko makubwa yaliotokea Urusi na China yaliwashawishi viongozi wa nchi changa za kiafrika katika miaka ya 60, 70 na 80 kujilimbikizia madaraka hili na wao waweze kufanya mabadiliko.

Utawala wa kidemokrasia ambao nchi nyingi za kiafrika zilirithi kutoka kwa watawala wake una matatizo yake. Moja ya matatizo hayo ni nguzu za bunge na mahakama.

Hivyo viongozi wengi wa kiAfrika kuanzia Nkwame Nkrumah, Julius Nyerere etc etc walikimbilia kujilimbikizia madaraka hili wawe kama Joseph Stalin wa Urusi au Mao Tse Tung wa China. Nia zao zilikuwa ni kutumia madaraka kuleta mabadiliko haraka kwa jamii.

Matatizo yaliopo ni kuwa viongozi pamoja na kujilimbikizia madaraka hayo, hawakuwa na ujuzi wa kutumia madaraka hayo kuleta mabadiliko ya kweli. Chukua mfano wa vijiji vya ujamaa Tanzania. Hile ilikuwa ni amri ya rais. Katika nchi yenye uhuru wa bunge na mahakama, nguvu zisingeweza kutumika kuwahamisha watu kinyume cha matakwa yao.

Ukweli wa mambo viongozi wa Tanzania hawana utamaduni wa kutumia madaraka yao hili kuleta mabadiliko ya kijamii.Kuanzia baba wa Taifa mpaka JK hakuna aliyeweza kutumia madaraka yake zaidi ya longolongo. Je kuna umuhimu gani kuendelea kuwapa madaraka watu wanaoshindwa kuyatumia? Chukua mfano kuhamisha makao makuu kutoka DSM kwenda Dodoma.
 
EMT,

cc: nguruvi3, bongolander, zakumi, jounegwalu na wengineo

Tumekuwa na mjadala mzuri sana kuhusu Government Vis a Vis State, ambao umezaa pande kuu mbili. Upande wa kwanza ni ule ambao unajadili kwamba sisi kama Taifa tumekomaa kwahiyo hoja ya kutokomaa isitumike kama kisingizio cha kwanini sisi kama taifa bado ni maskini lakini muhimu zaidi, isiwe ndio sababu ya msingi kwanini Katiba ijayo isimpunguzie madaraka Rais wa nchi. Upande wa pili wa hoja ni ule ambao unajadili kwamba sisi kama taifa, bado ni wachanga, huku msisitizo mkuu ukiwa ni juu ya umuhimu wa kutofautisha baina ya State na Government. Hoja hii inajadili kwamba linapokuja suala la kuunda serikali, kwa hili tumekomaa kwani tumekuwa tunafanya hivyo kwa miaka zaidi ya hamsini, lakini linapokuja suala la Serikali inaundwa kuendesha State ya aina gani, kwa kweli ni bayana kwamba hatujawa consistent, hivyo we don't qualify kujitazama kama tupo matured. Nimekuwa nikilind hoja yangu hii kwa kujadili kwamba linapokuja suala la State, tangia uhuru tumekuwa katika kipindi cha majaribio throughout kwa mfano from Party State (1961 – 1966); Developmental State (1967 – 1985); na hatimaye Contracting State (1986 – hadi sasa yani 2013); Na katika kipindi chote hiki, tumekuwa tunaunda serikali, lakini serikali haijawahi kuwa consistent na aina ya taifa linalojengwa, na hapa ni rahisi sana kuona jinsi gani maana ya dhana Taifa Kukomaa au State Maturity inapwaya.

Kumekuwa na hoja nyingi zinazohusisha mifano ya mataifa kama vile Singapore na nyinginezo (mfano rejea mijadala ya EMT) ambayo yalipata uhuru wake katika kipindi kinachokaribiana na Tanganyika/Tanzania (1960s), na hoja inajengwa kwamba wenzetu hawa (tofauti na sisi) wamefanikiwa kupiga hatua kubwa sana katika maendeleo kama Mataifa. Ni kwa mantiki hii, hoja inajengwa kwamba Tanzania kama Taifa sio wachanga. Hivyo tuache kutafuta visingizio juu ya umaskini wetu. Naona uzito mmoja tu katika hoja hii, nao ni watanzania (hasa viongozi) kuacha kusingizia uchanga wetu kwamba ndio sababu sisi bado maskini au ndio sababu kwanini bado tunahitaji Rais mwenye full executive powers. Pamoja na umuhimu wetu kuwa na mtazamo huu kama taifa, lakini tusikwepe ukweli kwamba nchi kama Singapore na nyinginezo wameweza kufikia walipo sasa kutokana na kuwa CONSISTENT KWA MIAKA ZAIDI YA HAMSINI juu ya Taifa la namna gani wanataka kujenga, na wao walitumia dhana ya kupanga ni kuchagua kwa umakini sana.

Tofauti ya Tanzania na nchi kama Singapore licha ya kwamba tulipata uhuru katika kipindi kimoja ni kwamba wao wamekuwa consistent na aina gani ya STATE wanajenga, kwani tofauti na sisi, Singapore na wengine tangia uhuru (1960s) hawajapata major interruptions katika ujenzi wa taifa. Sisi tumekuwa ni mabingwa wa kuhama (au kuhamishwa) kwa mfano kutoka option ya kuwa a Party State (miaka sita), baadae kuhamia a Developmental State (miaka kumi na nane) na baadae tena kuhamia kuwa a Contracting State (miaka 28 sasa). Ni katika muktadha huu ndio swali la mwenzetu Jingalafalsafa linakuwa na uzito wa kipekee kwamba Tanzania kama State Tumekoma Katika Nini? Tukitazama dhana ya Ukomavu au Maturity and then apply it katika muktadha wa mjadala wetu, ni dhahiri kwamba we are not matured as a state. Na kamwe hatuwezi kuwa matured bila kuwa na consistency juu na aina gani ya STATE tunayotaka kuijenga.
 

Mkuu mchambuzi unajua kuna baadhi ya mambo tunatakiwa kuyaangalia in simplest terms. Tuyaangalie kwa jicho la kawaida let us not be professorial or philosophical.

Hapa Tanzania kuna kundi la watu ambao bado wanataka kujustify uzembe wao kwa kusema sisi ni wachanga, tunasonga mbele. Lakini ukiangalia nchi kama Rwanda ambayo miaka 20 iliyopita ilianza kwenye scratch, lakini sasa it is way up there kuliko Tanzania. Why?

Kwanini miaka 40 iliyopita, tulipokuwa 'wachanga' wachanga zaidi kuliko sasa, tuliweza kuwa political imperialist kusini mwa Afrika, lakini sasa hata Mtwara inatushinda. We could do that kwenye mazingira ambayo demokrasia haikuwepo, elimu ilikuwa haitoshim, pesa zilikuwa chache.

Kwanini tuwe ovyo zaidi wakati tuna pesa zaidi kuliko zamani, elimu zaidi na uhuru zaidi.

The only explanation iko kwenye uongozi wa nchi. Chama tawala na serikali. Tatizo tunamwangalia tu JK na kumtupia madongo kwa kuwa yeye ndiye serikali mkuu. Lakini ingia chini, Mkuu wa Mkoa, mkuu wa wilaya, etc etc Angalia chama ngazi zote. Angalia nje ya serikali, nje ya CCM, utaona kuwa umejaa uozo tu.

Ni kweli we are operating a plural economy on the platform of defacto singular politics, no doubt hili si sahihi. Kwa kuwa CCM hata ikifanya uchafu kiasi gani kwa mentality ya sasa ya vyombo vya usalama, na mentality ya sasa ya mimi kwanza, chama pili, dini yangu tatu, Tanzania mwisho etc etc.........bado tutakuwa pale pale na kuendelea kurudi nyuma.

I am a strong advocate wa mabadiliko ya katiba, ikiwa ni pamoja na kipengele cha kupunguza madaraka ya rais. Lakini let us be honest hali hiyo haitaweza kuondoa 'uchanga' wa Tanzania. Kimsingi tunatakiwa kuwa na vipengelea vya kuwafanya wanasiasa wawe wanadeliver, sio kama sasa ukiwa mbunge ni kula tu kwa miaka mitano. Ukiwa mkuu wa mkoa kazi yako ni kukaa tu ofisini kufanya kazi za kila siku kuendesha mkoa etc etc nakubalina sana na hiyo quote uliyoweka hapo, hasa hii subquote

The constitution can provide only the organs of the State such as the Legislature, the Executive and the Judiciary. The factors on which the working for these organs of the State depend are the people and the political parties."

Inabidi kuwe na mechanism ya kutaka tuwe na maelendeo, kuhimiza maendeleo, kuhakikkisha tuna maendeleo, na watu wanafanya kazi hiyo. Pia tuwe na mentality ya kufuatilia na kusimamia. Kwa sasa ni kama tuna vichwa vya panzi tunaibiwa leo kwa style ya EPA tunalia kidogo kesho tumesahau, tunaibiwa kwa style nyingine tunacheka. Kwa sasa hakuna ufuatitiaji na ushughulikiaji, ndio maana unasikia kiongozi fulani anaiba pesa na kujaza usiwsi kila mwezi, au anajenga nyumba na kununua magari kila siku.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…