Balozi Tsere ataka Rais Samia kukaa na Wapinzani kama Kikwete ili kujadili Katiba Mpya

B
Balozi ana hoja na nia njema.
Ila hapa amejichanganya
1.Kukutana ili kupunguza joto.
2.Kukutana kirafiki.
Rais ni taasisi,
Vyama vya siasa ni taasisi.
My Balozi Joto uliloliona ndilo limekufanya utoke,hivyo kushauri likapunguzwe humsaidii Rais.

Kukutana kirafiki ni kuchochea joto Kali zaidi ya hili.
Kukutana Official kutakuwa na suluhu.
NB! Awamu ya 4 ilikuwa friendly
Awamu ya 5 ilikuwa chuma
Awamu ya 6 ni btn 4&5
Tunatokaje
 
Sijui kwa nini Ccm wanaogopa katiba mpya? Na huyu mama kwa vile anataka kugombea 2025 sidhani kama atakuja kukubali hoja ya katiba mpya!
CCM haiogopi katiba mpya.

Katiba mpya inaogopwa na wapinzani chini ya mwamvuli wa UKAWA kwa kususia bunge la Katiba na kuwaacha wajumbe wanaotokana na CCM na wasiotokana na vyama, na wale wa vyama vilivyokuwa havina ushawishi.

Kilichobaki ni kupigiwa kura ya maoni tu ya NDIO au HAPANA.

Atakaepata angalau thuluthi mbili (2/3) ya kura kwa kila upande unaotengeneza JAMHURI ya MUUNGANO wa TANZANIA, huyo ndie mshindi.
 
Subiri Ndugai atakavyokurupuka kutoka huko aliko na kutoa onyo[emoji23][emoji23]
 


#SIASA: Balozi mstaafu wa Tanzania nchini Malawi, Patrick Tsere amesema anamshauri Rais Samia Suluhu Hassan kukaa na wapinzani kirafiki na kujadili suala la Katiba Mpya ili kupata muafaka wa kitaifa kama alivyokuwa akifanya Rais Mstaafu wa Awamu ya nne, Dkt. Jakaya Kikwete.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam juzi, Tsere alinukuliwa akisema “Mazungumzo hayo ya kirafiki tu, yanaweza kupunguza joto lililopo sasa, yaani ni kama ambavyo Jakaya alivyokuwa akifanya, Alikuwa akiwaita kina Mbowe na kukaa nao pamoja si kupoteza ajenda, bali kupunguza tu joto.”

Pia, Balozi Tsere alionesha kutokukubaliana na nguvu inayotumika kuwazuia wanaodai Katiba Mpya na kuongeza kuwa “leo hii hata mtu akisema hebu tupitie kidogo au tuzungumze kuhusu Katiba watu hawataki.”

Chanzo: Serengeti Post
 
Hawa wazee walikuwa wapi kipindi cha Magufuli? [emoji848]
 
Hilo siyo kipaumbele kwa sasa...
Balozi anamzungumzia JK yupi?Yule waliemuita dhaifu au?
Samia alishaonesha njia ya kwenda kwenye katiba mpya hawa wahuni wakawa wanalazimisha siku ile ile uanze mchakato ilhali mh kawaambia nipeni muda kwanza.
Katiba mpya itadaiwa na wananchi na sio hawa wanasiasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…