Balozi wa Kenya aishambulia Russia kwa kuyatambua kama majimbo huru ya Ukraine

Qatari Minister of Energy Saad Al-Kaabi:
  • Compensation of Russian gas supplies to Europe is almost impossible
  • I think Russia is responsible for supplying between 30 and 40 percent of supplies to Europe, a country alone cannot compensate that much.
Daaah Koo kumbe ....vikwazo vitakuwa na impact kwa wote
 
Comparison of military.....equpiments of RUSSIA + that of Ukraine + NATO assistance
FB_IMG_16455913538497095.jpg

Source;. Alja Zeera English
 
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilifanya mkutano wa dharura baada ya Rais wa Urusi, Vladimir Putin kusema kwamba sasa anatambua sehemu ya Ukraine kama Urusi na atatuma wanajeshi wake kuwa walinzi wa amani katika majimbo hayo mawili.

Uingereza ilichukua hatua ya haraka kutangaza vikwazo. Urusi ilikemewa na nchi nyingi zikiwemo Mexico, Ireland, Norway, Ghana, na nyinginezo. Lakini ni Kenya ndiyo iliyojitokeza kwa makali yake kwa jinsi ilivyojibu hatua hiyo ya Urusi.

Balozi wake kwa Umoja wa Mataifa, Martin Kimani alitoa hotuba ambayo wengi wamejitokeza kuisifia kama iliyoeleza kwa urahisi na ukali unaostahiki ukiukwaji mkubwa wa sheria za kimataifa ambao Urusi imetekeleza.

"Uhuru wa eneo na mamlaka ya Ukraine yamevunjwa," alisema Balozi Martin Kimani na kuongeza:

"Mkataba wa Umoja wa Mataifa unaendelea kudhoofika chini ya shambulio hilo lisilo na huruma. Kwa wakati mmoja unatolewa kwa heshima na nchi zile zile ambazo kisha zikaupa kisogo katika kutekeleza malengo yanayopinga amani na usalama.... Kenya inasikitishwa sana na tangazo lililotolewa na Urusi la kutambua maeneo ya Ukraine kama mataifa huru.”

Aliendelea kusema kuwa Kenya ina wasiwasi mkubwa juu ya athari ambayo Urusi inaweza kuwa nayo ikiwa itaruhusiwa na UN kushambulia na kunyakua nchi zingine.

Mfano wake ni kwamba mipaka ya Afrika ilikubaliwa na nchi zote za huko, licha ya mipaka hiyo kulazimishwa na wakoloni. Alieleza kuwa mataifa ya Afrika yalifanya uamuzi huo badala ya kuwa na vita visivyoisha.

"Tulikataa upanuzi kwa misingi yoyote, ikiwa ni pamoja na rangi, kabila, au kitamaduni," alisema Kimani.

Baada ya hotuba yake hiyo, maoni yalianza kutolewa huku akisifiwa kwa hotuba yake hiyo. Watumiaji wa mitandao ya kijamii walituma jumbe za kuonyesha 'makali' ya ujumbe wake na jinsi Kimani alivyojieleza na kuwakilisha msimamo wa kenya kuhusu hatua ya Urusi.

Source: BBC
 
Jamaa anatafuta kiki za kimataifa
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] Tony254 MK254 komora096 wapo wapi huu uzi si unawahusu vip ! Mbona nawaona watz tu hapa , wakunya mkuje hapa watu wanawashangaa awajui kuwa nyinyi ni wapiganaji vita wazuri tu wa kurusha MAKOMBORA YA FLYTOILETS LAZIMA WARUSI WATOKE MBIO[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] never mess with FLYTOILETS worries [emoji1787][emoji1787]
 
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilifanya mkutano wa dharura baada ya Rais wa Urusi, Vladimir Putin kusema kwamba sasa anatambua sehemu ya Ukraine kama Urusi na atatuma wanajeshi wake kuwa walinzi wa amani katika majimbo hayo mawili.

Uingereza ilichukua hatua ya haraka kutangaza vikwazo. Urusi ilikemewa na nchi nyingi zikiwemo Mexico, Ireland, Norway, Ghana, na nyinginezo. Lakini ni Kenya ndiyo iliyojitokeza kwa makali yake kwa jinsi ilivyojibu hatua hiyo ya Urusi.

Balozi wake kwa Umoja wa Mataifa, Martin Kimani alitoa hotuba ambayo wengi wamejitokeza kuisifia kama iliyoeleza kwa urahisi na ukali unaostahiki ukiukwaji mkubwa wa sheria za kimataifa ambao Urusi imetekeleza.

"Uhuru wa eneo na mamlaka ya Ukraine yamevunjwa," alisema Balozi Martin Kimani na kuongeza:

"Mkataba wa Umoja wa Mataifa unaendelea kudhoofika chini ya shambulio hilo lisilo na huruma. Kwa wakati mmoja unatolewa kwa heshima na nchi zile zile ambazo kisha zikaupa kisogo katika kutekeleza malengo yanayopinga amani na usalama.... Kenya inasikitishwa sana na tangazo lililotolewa na Urusi la kutambua maeneo ya Ukraine kama mataifa huru.”

Aliendelea kusema kuwa Kenya ina wasiwasi mkubwa juu ya athari ambayo Urusi inaweza kuwa nayo ikiwa itaruhusiwa na UN kushambulia na kunyakua nchi zingine.

Mfano wake ni kwamba mipaka ya Afrika ilikubaliwa na nchi zote za huko, licha ya mipaka hiyo kulazimishwa na wakoloni. Alieleza kuwa mataifa ya Afrika yalifanya uamuzi huo badala ya kuwa na vita visivyoisha.

"Tulikataa upanuzi kwa misingi yoyote, ikiwa ni pamoja na rangi, kabila, au kitamaduni," alisema Kimani.

Baada ya hotuba yake hiyo, maoni yalianza kutolewa huku akisifiwa kwa hotuba yake hiyo. Watumiaji wa mitandao ya kijamii walituma jumbe za kuonyesha 'makali' ya ujumbe wake na jinsi Kimani alivyojieleza na kuwakilisha msimamo wa kenya kuhusu hatua ya Urusi.

Source: BBC
Hatareee
 
Wew nae hujui kitu, hizo sheria za kimataifa na hayo makundi ya jumuiya za kimataifa kwa taarifa yako, hawa wote ni machawa wa Umagharibi+USA kwaiyo agenda yoyote ktk jumuiya hizo zilishabarikiwa na wamagharibi+USA kuwa sheria&kanuni zitafanya kazi kulingana na matakwa ya wao wanavyopenda haijarishi ni muda gan.

Na kwakuwa wanajinadi kusambaza ushawishi ktk mataifa mengi haswa bendera fuata upepo toka afrika, so ni vigumu kwenda kinyume na sheria hizo, maana hata ukipinga bado kwenye kamati zao za kulipima jambo lako hutopata kura nyingi, kwakuwa wengi hufuata agenda za misimamo ya bwana wao USA.

Kaa kwa kutulia kjna bado huijui dunia

Kuna mmoja ambaye alipewa kiti cha kuazima kama ilivyo kenya, yaani mwanachama wa muda wa baraza la usalama, alipinga kitu cha marekani. Marekani alikuwa na kitu chake, akawa anafanya ushawishi wa kukipitisha kwenye baraza. Huyo wa kiti cha kuazima, akapiga kura ya hapana. marekani wakamuambia, hiyo kura yako ina gharama kubwa sana. Itakugharimu sana. Baada ya muda, akashangaa miradi ambayo ilikuwa inafadhiriwa na marekani nchini mwake ikanyimwa fedha, mambo mengi ya misaada yakasitishwa. Mpaka ile nchi ikasema, tungejua wala tusingegombea kupata hicho kiti. 😂 🤣 😛
 
Back
Top Bottom