Baada ya Magu jumapili hii akiwa kwenye nyumba ya Bwana kuwakumbusha wakenya kuwa, mwaka huu watachemsha mawe wakimtibua, naona Kenyatta kamtuma balozi wao kuomba POO kwa mzee baba na wananchi kwa ujumla. Maana wameshamjua mzee baba kwa jeuri, akiamua kaamua.
Kenya itahitaji tena tuwalishe mwaka huu, maana kiangazi kiliwapiga, nzige wakaja wakavuna vichache vilivyokuwa vimestawi, na kama haikuwatosha, mafuriko sio tu yanabeba mashamba huko, mpaka wenye mashamba.
Na hii kujishaua kuwa watanunua ugali toka Ethiopia, ni kujitekenya na kucheka wenyewe. Ethiopia shibe yao tu mbinde, hiyo njaa ya jirani yao wataimudu?
Hivyo watake wasitake, ugali wao uko kwetu.
Sijui kwanini Kenyatta mgumu wa kuelewa. It´s been almost miaka 5 sasa ya Magu, hajamuelewa tu? Au maji machafu yamemharibu sio tu macho bali kichwa pia? Alishindwa kumjulisha Magu uamuzi wa kufunga mipaka kabla ya kukurupuka? Ayaa bana, ngoja aendelee kumchezea mzee baba sharubu, yakimkuta yakumkuta, asijekusema hakupewa tahadhari.