Balozi wa Marekani: Kwa Miaka 3 Marekani imetoa msaada Tanzania Dola Bilioni 7.5 sawa na Trilioni 25 za Tanzania. Sio Mkopo ni Msaada tu

Balozi wa Marekani: Kwa Miaka 3 Marekani imetoa msaada Tanzania Dola Bilioni 7.5 sawa na Trilioni 25 za Tanzania. Sio Mkopo ni Msaada tu

Jana katika Mkutano wa Kituo cha Demokrasia Balozi wa Marekani kamjibu yule aliyewatishia. Kasema Vitendo vya Ukatili, Utekaji na Mauaji havikubaliwi na Demokrasia yeyote. Si Marekani si Tanzania.

Ameenda mbali kwa kusema kwa miaka mitatu tu Marekani imetoa msaada kwa Tanzania wa dola bilioni 7.5 na hizi sio mkopo ni msaada tu! Kwa msio jua hizi ni karibu na trilion 25 za Kitanzania

Kazi kwenu wananzengo. Mie naongeza popcorn.🤣🤣🤣View attachment 3100891
Hii ndiyo hotuba ya US Ambassador to Tanzania Mr Michael Battle. Ni very strong and bold speech...

Na kusema kweli kamkemea na kupingana kwa 100% na hotuba na msimamo wa Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania...

Kwa lugha rahisi na ya moja kwa moja ni kama kamkemea na kumwambia "KAMWE MAREKANI HAIWEZI KUNYAMAZA JUU YA MAUAJI NA UTEKAJI WA WATU"
 
Wasitishe acha kutisha watu .
Unajitisha mwenyewe kwa kukubali kuwa omba omba wa kujitakia. Ukishakubali kuwa mtu wa kusaidiwa huwezi kuwa na jeuri tena kwa anayekusaidia. Sana sana utaonekana mbwa kibogoyo anayebweka bila tija. Kesho mapema asubuhi tunarudi tena kuwalamba miguu watusaidie walau dawa za Malaria na kifua kikuu, bila kusahau ARV, vyandarua, ujenzi wa vyoo, ujenzi wa masoko, miradi ya afya, lishe, kilimo, elimu n.k.
 
Mabalozi wengi ni wanajeshi wa zamani au mashushushu wa zamani.

Empty

Unawafokea na kuwachamba wanakupa msaada wa matrilioni na mikopo ya matrilioni imf na world bank ni zao. Mashirika na NGO nyingi ni zao, zinazotoa misaada ya matrilioni
hongera kwa kulijua hilo kuhusu mabalozi.
 
Jana katika Mkutano wa Kituo cha Demokrasia Balozi wa Marekani kamjibu yule aliyewatishia. Kasema Vitendo vya Ukatili, Utekaji na Mauaji havikubaliwi na Demokrasia yeyote. Si Marekani si Tanzania.

Ameenda mbali kwa kusema kwa miaka mitatu tu Marekani imetoa msaada kwa Tanzania wa dola bilioni 7.5 na hizi sio mkopo ni msaada tu! Kwa msio jua hizi ni karibu na trilion 25 za Kitanzania

Kazi kwenu wananzengo. Mie naongeza popcorn.🤣🤣🤣View attachment 3100891
Kati ya hizo ni ngapi zimebaki kwao?
 
Unajitisha mwenyewe kwa kukubali kuwa omba omba wa kujitakia. Ukishakubali kuwa mtu wa kusaidiwa huwezi kuwa na jeuri tena kwa anayekusaidia. Sana sana utaonekana mbwa kibogoyo anayebweka bila tija. Kesho mapema asubuhi tunarudi tena kuwalamba miguu watusaidie walau dawa za Malaria na kifua kikuu, bila kusahau ARV, vyandarua, ujenzi wa vyoo, ujenzi wa masoko, miradi ya afya, lishe, kilimo, elimu n.k.
Mbona hwasitishi ...kwani waliitwa ?
 
Ili kukuza demokrasia nchini,ninashauri Trilioni 25 kutoka USA, sasa zipelekwe Moja Kwa Moja kwenye vyama vya uponzani ili viweze kukua zaidi.
 
Mbona Magufuli alikuwa anasema kutwa , hakuna lolote msaada sio lazima ...Wangeacha tungeishi maana hata pesa wanaprint wao ....Hatuwezi kufa njaa ng'o hizo pesa wanakula wachache .

Ukweli ni kwamba hwana ubavu wa kuingilia mambo ya ndani ya nchi yoyote hatutaki machafuko ....Afrika inaweza kuwepo bila ya hao , wanaimarisha uhusiano tu ...Huko kwao kuna homeless si wafute umaskini usome zero .! watu ambao wanafadhili mpaka vita ili wengine wauawe.
Wangekuwa wanaume kweli wangeanza na Putin, kule Ukraine umefanywa unyama kwa miaka miwili mfululizo hawa mabalozi mikia imerudi tumboni hawana chochote wanachoweza kufanya.
 
Kunywa maji utulie kwanza, naona hapa ni lugha gongana tu, hatutofikia muafaka.
Ngoja pesa za kupewa maana kazi hutaki , angalia marinda hayo maana unakosa msimamo kwa mabwana zako 😀 😀
 
Lakini pia wapaswa kujiuliza hiyo hela nyingi hivyo imetumikaje kama ni kweli?
Hata hivyo tunapaswa kuwaza kujitegemea badala muda wote kuwaza misaada!
 
Wangekuwa wanaume kweli wangeanza na Putin, kule Ukraine umefanywa unyama kwa miaka miwili mfululizo hawa mabalozi mikia imerudi tumboni hawana chochote wanachoweza kufanya.
Kwani wamekuita kwenda kuchukua misaada au shida zenu na kukosa akili ndiyo kinawapeleka kwenda kuomba
 
Kwani wamekuita kwenda kuchukua misaada au shida zenu na kukosa akili ndiyo kinawapeleka kwenda kuomba
Hao ni binadamu tu, kisa wanawapa pesa nyinyi wanaharakati wa siasa za bongo haIwafanyi wakawa wamefikia hatua za umalaika, ni binadamu wenye kukosolewa na kuambiwa ukweli pale wanapokengeuka.
 
Back
Top Bottom